Dkt. Nchemba ahani msiba wa hayati Cleopa Msuya

Dkt. Nchemba ahani msiba wa hayati Cleopa Msuya

Samson Kwayu

Member
Joined
Jun 9, 2022
Posts
29
Reaction score
105
IMG-20250509-WA0009.jpg

20250509_182014.jpg
IMG-20250509-WA0010.jpg
IMG-20250509-WA0015.jpg
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefika kuhani msiba wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, na ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (1973–1975) na Waziri wa Fedha na Uchumi (1986–1989), Hayati David Cleopa Msuya, nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na familia ya Hayati Msuya, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa, Hayati David Cleopa Msuya atakumbukwa kwa mchango mkubwa alioutoa katika uongozi wake wakati wa uhai wake ikiwemo kuweka misingi imara ya usimamizi wa uchumi wa nchi akiwa Waziri wa Fedha na nafasi nyingine alizozishika na kwamba wataenzi mchango wake huo kwa kuhakikisha kuwa uchumi unazidi kuimarika kwa manufaa ya wananchi.
 

Attachments

  • IMG-20250509-WA0015.jpg
    IMG-20250509-WA0015.jpg
    440.3 KB · Views: 21
  • IMG-20250509-WA0016.jpg
    IMG-20250509-WA0016.jpg
    377.6 KB · Views: 26
Rais Samia umekubali mradi wa mwendokasi ukufie mikononi mwako?
Mwendokasi sasa inaishia Kimara badala ya kufika Kibaha na Mbezi kama iliyokuwa zamani.
 
Hao pichani ni wajukuu 🤔 ni Upanga sehemu gani ?? Special hire hazitoenda upareni nipate lift kina mshana na mfinanga pamoja na mvungi
 
hivi msuya si ndio aliyesema kilamtu atabeba msalaba wake, akaanzisha ada mashuleni, akaondoa chakula vyuoni, akaanzisha ada vyuoni, au kuna mwingine?

si ni huyuhuyu, customs na bandarini walijaa wapare na wachagga? alihudumu miaka miwili tu ila chamoto tulikiona
 
Back
Top Bottom