Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 918
- 1,994
Hongera Dr Mwigulu kwa kuweka wazi msimamo wa Mhe Rais/serikali punde tu baada ya Lissu kushambuliwa.Watu wanadhani kila hatua ya uchunguzi sharti iwekwe wazi kwa umma wakati kuna taratibu za kiintelijinsia.Mahojiano ya Mbunge wa Iramba, Dkt. Mwigulu Nchemba kupitia Kipindi cha Clouds 360 pale Clouds Tv kwa ufupi..
Maswali muhimu aliyoulizwa:
Kwanini tangu utenguliwe uwaziri wa Mambo ya Ndani na Rais Dkt. John Magufuli, umekuwa kimya sana?
"Unajua ukiwa kwenye nafasi ya uwaziri vipo vitu vingi vya kuvisemea (mambo mbalimbali yanayotokea nchini). Ndio maana sasa hivi nipo kimya. Nimebaki na vitu viwili tu vya kusemea; mambo ya jimboni kwangu na kazi nzuri inayofanywa na serikali yangu"
Kuna tofauti gani ya Uwaziri na Ubunge?
Hakuna tofauti na maisha yangu hayajabadilika. Nilipokuwa waziri kwenye msafara wangu sikutaka magari yasimamishwe ili nipite. Kwa sababu nilikuwa nafahamu kuna wengine walikuwa wanawahi ndege "airport', wengine wagonjwa na wengine makazini sikutaka kuwachelewesha. Nilikuwa mtu wa kawaida (Mtu wa Watu), ndio maana sioni tofauti na sasa nilivyobaki na ubunge pekee".
Rais Magufuli alivyokutumbua Ulijisikiaje? Ulikasirika?
"Nilisema nilipokuwa kwenye mkutano jimboni kwangu Iramba, nilimshukuru sana Rais wangu John Magufuli kwa kunipa nafasi hiyo ya uwaziri. Sisi ni wafugaji, siku baba akikwambia usiende kuchunga utakasirika? Huwezi".
Vipi kuhusu kugombea urais 2020?
"Kwa kazi nzuri anazofanya Rais wetu John Magufuli, kila mwanaCCM anajua na kufahamu. Kwa sasa nipo bize na jimbo langu, sina mpango wa kugombea URAIS".
Ishu ya "Askari'' aliyemtolea Nape bastola.
"Sikuwahi kusema sio askari. Nilisema sio Polisi. Nilimwelekeza IGP kuchukua hatua aliniambia yule jamaa sio polisi. Kuna utaratibu wa kuchukua hatua na sio kila hatua inatangazwa kwenye vyombo vya habari"
Wana-Singida wakikuuliza Tundu Lissu yuko wapi huwa unawajibu nini?
"Wanasingida wote wanajua kilichotokea na wanazo taarifa za maendeleo yake. Wanajua alipo. Tatizo lililopo ni ukinzani wa taarifa zinazosambazwa na kunyoosheana vidole hasa na chama chake. Mfano kwenye uchaguzi mdogo walikuwa wanasema msiwape kura hawa wamempiga mwenzetu. Jambo ambalo sio sawa.
"Tundu Lissu aliposhambuliwa, Rais Magufuli alinipigia simu akanipa maelekezo kuchukua hatua haraka sana na wahalifu wakamatwe haraka sana’’
Zaidi kuhusu ishu ya Lissu tazama kipande hiki;
Aulizwe alifanya nini ili kuhakikisha wahusika wanapatikana haraka?Hongera Dr Mwigulu kwa kuweka wazi msimamo wa Mhe Rais/serikali punde tu baada ya Lissu kushambuliwa.Watu wanadhani kila hatua ya uchunguzi sharti iwekwe wazi kwa umma wakati kuna taratibu za kiintelijinsia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umesikiliza vizuri maelezo yake kuhusu suala la ulinzi Area D?Walinzi walikuwa wapi na nani aling'oa CCTV baada ya shambulio?! Nashangaa maswali haya hayajibiwi na wanaowahoji hawaulizi maswali haya.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera Dr Mwigulu kwa kuweka wazi msimamo wa Mhe Rais/serikali punde tu baada ya Lissu kushambuliwa.Watu wanadhani kila hatua ya uchunguzi sharti iwekwe wazi kwa umma wakati kuna taratibu za kiintelijinsia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe mwenye kujua tuwekee wazi hapa hatua za kiuchunguzi zilivyo.Upinzani wa Bongo bwana yaani ni kupinga kila kitu hata chenye ukweli ili mradi aliyesema awe CCM tu.Lakini mtu huyo huyo akizungumza maneno yale yale akiwa upinzani atasapotiwa kwa nguvu zote.Kawadanganye maboya wenzio
Wauaji sasa wameanza kujipambanua. Mungu atawaibua tu. Mungu wetu tunayemtumikia hajawahi kutuangusha. Subiri Lissu akirudi aje kuwataja wote waliohusika kumpiga risasi kwa lengo la kumuua.cc Ansbert Ngurumo
What if you are wrong?Wauaji sasa wameanza kujipambanua. Mungu atawaibua tu. Mungu wetu tunayemtumikia hajawahi kutuangusha. Subiri Lissu akirudi aje kuwataja wote waliohusika kumpiga risasi kwa lengo la kumuua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Naona sass kila mmoja ana umwa tumbo LA kuharisha baada ya kusikia tl ana kwenda ICC.. this country wanaijua wenyewe maCcmAulizwe alifanya nini ili kuhakikisha wahusika wanapatikana haraka?
Ndio kusubiri Lissu apone aje kuhijiwa ndio uchunguzi uendelee????
Sio walinzi wala cctv footage,vyote havijahojiwa!
iyo video iko wapi? mie naona anahojiwa juu ya TL anashia sema unaweza tolewa na wasio waungwana sijaona akijibuUmesikiliza vizuri maelezo yake kuhusu suala la ulinzi Area D?
Nimeweka video. Chukua muda kidogo usikilize mkuu. Ametoa ufafanuzi mzuri tu.
Hongera Dr Mwigulu kwa kuweka wazi msimamo wa Mhe Rais/serikali punde tu baada ya Lissu kushambuliwa.Watu wanadhani kila hatua ya uchunguzi sharti iwekwe wazi kwa umma wakati kuna taratibu za kiintelijinsia.
Sent using Jamii Forums mobile app