Dkt. Mwigulu Nchemba: Tundu Lissu aliposhambuliwa, Rais Magufuli alinipigia simu...

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
Mahojiano ya Mbunge wa Iramba, Dkt. Mwigulu Nchemba kupitia Kipindi cha Clouds 360 pale Clouds Tv kwa ufupi..

Maswali muhimu aliyoulizwa:

Kwanini tangu utenguliwe uwaziri wa Mambo ya Ndani na Rais Dkt. John Magufuli, umekuwa kimya sana?

"Unajua ukiwa kwenye nafasi ya uwaziri vipo vitu vingi vya kuvisemea (mambo mbalimbali yanayotokea nchini). Ndio maana sasa hivi nipo kimya. Nimebaki na vitu viwili tu vya kusemea; mambo ya jimboni kwangu na kazi nzuri inayofanywa na serikali yangu"

Kuna tofauti gani ya Uwaziri na Ubunge?

Hakuna tofauti na maisha yangu hayajabadilika. Nilipokuwa waziri kwenye msafara wangu sikutaka magari yasimamishwe ili nipite. Kwa sababu nilikuwa nafahamu kuna wengine walikuwa wanawahi ndege "airport', wengine wagonjwa na wengine makazini sikutaka kuwachelewesha. Nilikuwa mtu wa kawaida (Mtu wa Watu), ndio maana sioni tofauti na sasa nilivyobaki na ubunge pekee".

Rais Magufuli alivyokutumbua Ulijisikiaje? Ulikasirika?

"Nilisema nilipokuwa kwenye mkutano jimboni kwangu Iramba, nilimshukuru sana Rais wangu John Magufuli kwa kunipa nafasi hiyo ya uwaziri. Sisi ni wafugaji, siku baba akikwambia usiende kuchunga utakasirika? Huwezi".

Vipi kuhusu kugombea urais 2020?

"Kwa kazi nzuri anazofanya Rais wetu John Magufuli, kila mwanaCCM anajua na kufahamu. Kwa sasa nipo bize na jimbo langu, sina mpango wa kugombea URAIS".

Ishu ya "Askari'' aliyemtolea Nape bastola.

"Sikuwahi kusema sio askari. Nilisema sio Polisi. Nilimwelekeza IGP kuchukua hatua aliniambia yule jamaa sio polisi. Kuna utaratibu wa kuchukua hatua na sio kila hatua inatangazwa kwenye vyombo vya habari"

Wana-Singida wakikuuliza Tundu Lissu yuko wapi huwa unawajibu nini?

"Wanasingida wote wanajua kilichotokea na wanazo taarifa za maendeleo yake. Wanajua alipo. Tatizo lililopo ni ukinzani wa taarifa zinazosambazwa na kunyoosheana vidole hasa na chama chake. Mfano kwenye uchaguzi mdogo walikuwa wanasema msiwape kura hawa wamempiga mwenzetu. Jambo ambalo sio sawa.

"Tundu Lissu aliposhambuliwa, Rais Magufuli alinipigia simu akanipa maelekezo kuchukua hatua haraka sana na wahalifu wakamatwe haraka sana’’

Zaidi kuhusu ishu ya Lissu tazama kipande hiki;

Hongera Dr Mwigulu kwa kuweka wazi msimamo wa Mhe Rais/serikali punde tu baada ya Lissu kushambuliwa.Watu wanadhani kila hatua ya uchunguzi sharti iwekwe wazi kwa umma wakati kuna taratibu za kiintelijinsia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aulizwe alifanya nini ili kuhakikisha wahusika wanapatikana haraka?
Ndio kusubiri Lissu apone aje kuhijiwa ndio uchunguzi uendelee????
Sio walinzi wala cctv footage,vyote havijahojiwa!
 
Wao wenyewe ndio wametuzoesha kutuambia kila kitu
Ndio maana watu wanauliza, Ili takiwa since day one wasiwe wanaita vyombo vya Habari kutoa maelezo ya mambo ya uchunguzi
 
Kuna mtu anamwamini mwigulu
yule aliyetaka kuwa rais ili awakomeshe upinzani

aiseeee
aibu naona mimi
 
Sijui hizo PhD wanaziokota wapi? Kaulizwa wazee wakikuuliza tundu lissu yuko wapi? Jibu lake ni kituko
 
Aulizwe alifanya nini ili kuhakikisha wahusika wanapatikana haraka?
Ndio kusubiri Lissu apone aje kuhijiwa ndio uchunguzi uendelee????
Sio walinzi wala cctv footage,vyote havijahojiwa!
Naona sass kila mmoja ana umwa tumbo LA kuharisha baada ya kusikia tl ana kwenda ICC.. this country wanaijua wenyewe maCcm
Maana naona hata makatibu tarafa wana haribu kujibu malalamiko ya TL sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa watu makini hii kauli ilitarajiwa. Ni ishara kwamba pamoja na yote binadamu bado anabakiwa na dhamira ambayo wakati mwingine humsuta.Siku hizi kumezuka mtindo wa watu kujitokeza kuzungumzia masuala nyeti ya siasa katika mazingira yanayoashiria kuwa wametumwa. Mifano hai ni hii. Uteuzi wa Katibu wa Mbunge ulipokosolewa Spika mstaafu alijitokea kusikojulikana kutetea kuwa ulifanyika vema! Mjadala wa nyaraka za kichungaji za maaskofu uliposhika kiasi muumini msomi wa kanisa moja alijitokeza kukosoa kanisa lake kwa andishi lisilofanana na usomi wake. Askofu mmoja wa Katoliki alipotoa msimamo wake binafsi kuhusu katiba mpya mwingine akajitokeza eti kufafanua kuwa huo siyo msimamo wa kanisa; ni maoni binafsi ya askofu! Na mengine mengi ya aina hii. Hata hili la Mwigulu liko hivyo hivyo hasa ikizingatiwa kipindi hiki cha sasa. Kwanini aseme leo? Alikuwa wapi siku zote asitufikishie hayo maneno? Na je, kwa unyeti wa tukio lenyewe hii ndiyo njia mwafaka ya kuwasilisha ujumbe mzito kutoka kwa rais wa nchi? Too little too late. Mtu mwelewa utjiuliza nini kimewapta viongozi wetu.
 
Umesikiliza vizuri maelezo yake kuhusu suala la ulinzi Area D?

Nimeweka video. Chukua muda kidogo usikilize mkuu. Ametoa ufafanuzi mzuri tu.
iyo video iko wapi? mie naona anahojiwa juu ya TL anashia sema unaweza tolewa na wasio waungwana sijaona akijibu
 
Hongera Dr Mwigulu kwa kuweka wazi msimamo wa Mhe Rais/serikali punde tu baada ya Lissu kushambuliwa.Watu wanadhani kila hatua ya uchunguzi sharti iwekwe wazi kwa umma wakati kuna taratibu za kiintelijinsia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Acha ujinga wewe, aliyeshambuliwa ni kiongozi wa upinzani, ana wafuasi wake ambao wana haki ya kujua nini kinaendelea kuhusu tukio hilo, unafanya siri kwani ni uchumba huo? Hatua ya kwanza ya uchunguzi makini ni kumhoji muathirika na siyo kutapatapa. yani mmefikia hadi kumyima haki ya mshahara wake halafu unaleta upuuzi hapa? chuki zenu mtalipwa kesho mbele ya Mfalme wa siku ya MALIPO.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom