Dkt. Mwigulu Nchemba: Tundu Lissu aliposhambuliwa, Rais Magufuli alinipigia simu...

Hongera Dr Mwigulu kwa kuweka wazi msimamo wa Mhe Rais/serikali punde tu baada ya Lissu kushambuliwa.Watu wanadhani kila hatua ya uchunguzi sharti iwekwe wazi kwa umma wakati kuna taratibu za kiintelijinsia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona alivyoshambuliwa mwanajeshi mstaafu kila kitu kiliwekwa wazi. Alitembelewa na huduma stahiki alipata, why Lisu iwe siri?
Acheni hizo, Mungu hadhihakiwi
 
Walinzi walikuwa wapi na nani aling'oa CCTV baada ya shambulio?! Nashangaa maswali haya hayajibiwi na wanaowahoji hawaulizi maswali haya.

Sent using Jamii Forums mobile app
"Tulimumu, hii habari ya walinzi walikuwa wapi mbona ni ya kijinga- hivi nani aliwafungulia geti Mh. Lissu na DREVA wake? Na mlinzi wa Mh. LISSU naye alikuwa wapi?
 
"Tulimumu, hii habari ya walinzi walikuwa wapi mbona ni ya kijinga- hivi nani aliwafungulia geti Mh. Lissu na DREVA wake? Na mlinzi wa Mh. LISSU naye alikuwa wapi?
Ajabu!

Yaani mtu unarudi nyumbani, unakuta mazingira ya nje sio ya kawaida (hakuna walinzi, pako kimya), kwanini usichukue tahadhari ukizingatia umekuwa ukipokea vitisho?

Tujifunze kuhoji.
 
Mahojiano ya Mbunge wa Iramba, Dkt. Mwigulu Nchemba kupitia Kipindi cha Clouds 360 pale Clouds Tv kwa ufupi..

Maswali muhimu aliyoulizwa:

Kwanini tangu utenguliwe uwaziri wa Mambo ya Ndani na Rais Dkt. John Magufuli, umekuwa kimya sana?

"Unajua ukiwa kwenye nafasi ya uwaziri vipo vitu vingi vya kuvisemea (mambo mbalimbali yanayotokea nchini). Ndio maana sasa hivi nipo kimya. Nimebaki na vitu viwili tu vya kusemea; mambo ya jimboni kwangu na kazi nzuri inayofanywa na serikali yangu"

Kuna tofauti gani ya Uwaziri na Ubunge?

Hakuna tofauti na maisha yangu hayajabadilika. Nilipokuwa waziri kwenye msafara wangu sikutaka magari yasimamishwe ili nipite. Kwa sababu nilikuwa nafahamu kuna wengine walikuwa wanawahi ndege "airport', wengine wagonjwa na wengine makazini sikutaka kuwachelewesha. Nilikuwa mtu wa kawaida (Mtu wa Watu), ndio maana sioni tofauti na sasa nilivyobaki na ubunge pekee".

Rais Magufuli alivyokutumbua Ulijisikiaje? Ulikasirika?

"Nilisema nilipokuwa kwenye mkutano jimboni kwangu Iramba, nilimshukuru sana Rais wangu John Magufuli kwa kunipa nafasi hiyo ya uwaziri. Sisi ni wafugaji, siku baba akikwambia usiende kuchunga utakasirika? Huwezi".

Vipi kuhusu kugombea urais 2020?

"Kwa kazi nzuri anazofanya Rais wetu John Magufuli, kila mwanaCCM anajua na kufahamu. Kwa sasa nipo bize na jimbo langu, sina mpango wa kugombea URAIS".

Ishu ya "Askari'' aliyemtolea Nape bastola.

"Sikuwahi kusema sio askari. Nilisema sio Polisi. Nilimwelekeza IGP kuchukua hatua aliniambia yule jamaa sio polisi. Kuna utaratibu wa kuchukua hatua na sio kila hatua inatangazwa kwenye vyombo vya habari"

Wana-Singida wakikuuliza Tundu Lissu yuko wapi huwa unawajibu nini?

"Wanasingida wote wanajua kilichotokea na wanazo taarifa za maendeleo yake. Wanajua alipo. Tatizo lililopo ni ukinzani wa taarifa zinazosambazwa na kunyoosheana vidole hasa na chama chake. Mfano kwenye uchaguzi mdogo walikuwa wanasema msiwape kura hawa wamempiga mwenzetu. Jambo ambalo sio sawa.

"Tundu Lissu aliposhambuliwa, Rais Magufuli alinipigia simu akanipa maelekezo kuchukua hatua haraka sana na wahalifu wakamatwe haraka sana’’

Zaidi kuhusu ishu ya Lissu tazama kipande hiki;

Ni muongo, ameona hawezi kupambana Maghufuli, na wakati huo huo akiunyemelea urais!
 
Ajabu!

Yaani mtu unarudi nyumbani, unakuta mazingira ya nje sio ya kawaida (hakuna walinzi, pako kimya), kwanini usichukue tahadhari ukizingatia umekuwa ukipokea vitisho?

Tujifunze kuhoji.
Tahadhari gani na walikuwa wakifuatiliwa? Na si ni hao hao ambao polisi na vyombo vya usalama vilimchukulia kama adui?

Si ndiyo huyu huyu rais alisema ni msaliti na wasaliti huwa hawaachiwi wakasavaivu?

Usiwe kama kichwa kopo.
 
"Tulimumu, hii habari ya walinzi walikuwa wapi mbona ni ya kijinga- hivi nani aliwafungulia geti Mh. Lissu na DREVA wake? Na mlinzi wa Mh. LISSU naye alikuwa wapi?
Kwahiyo kwasababu walifunguliwa geti, basi walinzi walikuwepo! Another kichwa kopo!

Si ungeuliza tu nani aliyefungua geti kama una ubongo na akili huru?
 
Hongera Dr Mwigulu kwa kuweka wazi msimamo wa Mhe Rais/serikali punde tu baada ya Lissu kushambuliwa.Watu wanadhani kila hatua ya uchunguzi sharti iwekwe wazi kwa umma wakati kuna taratibu za kiintelijinsia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sema neno juu ya wale wanaokamatwa na polisi wanapo vaa nguo iloandikwa pray for Lissu
 
Tahadhari gani na walikuwa wakifuatiliwa? Na si ni hao hao ambao polisi na vyombo vya usalama vilimchukulia kama adui?

Si ndiyo huyu huyu rais alisema ni msaliti na wasaliti huwa hawaachiwi wakasavaivu?

Usiwe kama kichwa kopo.

Tujadiliane bila kutukanana mkuu. Unajidhalilisha!
 
Tujadiliane bila kutukanana mkuu. Unajidhalilisha!
Wapi umeona matusi?

Au haujui kuinsult intelligence ni kile kile unachokilalamikia hapa? Yani geti kufunguliwa ndiyo kwamba walinzi walikuwepo maeneo yote?

Ukijadili kishabiki lazima tu utaumbuka!
 
Mimi mwenyewe nilishangaa sana kusikia Lisu anadai raisi hakwenda kwenye TV kutoa tamko wakati hata tweet ya raisi anaikataa anasema ni tweet ya Msigwa, alitaka raisi atoe tamko gani sasa.
 
kuna kitu huwa wakati mwingine sisi kama wanadamu tunasahau.
sisi sote humu duniani ni mali ya MUNGU "WE BELONGS TO GOD" na huyo anayeTUMILIKI anaona mpaka SIRINI.
Haya maigizo yote yanayoendelea anayaona ni suala la muda tu UKWELI UTAJULIKANA.
Nishauri jambo hili kwetu kama wanadamu,tusijaribu kwa namna yeyote hata kwa ushawishi wa aina gani hata kwa fedha KIASI GANI kujaribu kuutoa UHAI wa binadamu mwenzako.
DAMU ya mtu haijawahi KUNYAMAZA hata siku moja!!
MBARIKIWE SANA
 
Kwahiyo kwasababu walifunguliwa geti, basi walinzi walikuwepo! Another kichwa kopo!

Si ungeuliza tu nani aliyefungua geti kama una ubongo na akili huru?
jmushi1, afadhili MIE kichwa kopo kuliko WEWE BILA KICHWA
 
Huyu si alisema tukio la TL sio jambo la ajabu wala sio wakwanza kutandikwa risasi?

Nikashangaa sana hakujali kabisa kwamba yule ni jamaa yake wa Singida.

Nafikiri walijua atakufa tu asingerudi tena. Sasa kila aliyehusika akiwaza jamaa atarudi akiwa mzima wanakosa amani.

Ni namna ya kutaka kuonyesha yupo na ana msaada. Njaa mbaya sana.
 
Back
Top Bottom