Dkt. Mwigulu Nchemba: Tundu Lissu aliposhambuliwa, Rais Magufuli alinipigia simu...

Huhitaji hata kuuliza maswali, body language ya Mwigulu Nchemba inatoa majibu yote,
 
Mahojiano ya Mbunge wa Iramba, Dkt. Mwigulu Nchemba kupitia Kipindi cha Clouds 360 pale Clouds Tv kwa ufupi..

Maswali muhimu aliyoulizwa:

Kwanini tangu utenguliwe uwaziri wa Mambo ya Ndani na Rais Dkt. John Magufuli, umekuwa kimya sana?

"Unajua ukiwa kwenye nafasi ya uwaziri vipo vitu vingi vya kuvisemea (mambo mbalimbali yanayotokea nchini). Ndio maana sasa hivi nipo kimya. Nimebaki na vitu viwili tu vya kusemea; mambo ya jimboni kwangu na kazi nzuri inayofanywa na serikali yangu"

Kuna tofauti gani ya Uwaziri na Ubunge?

Hakuna tofauti na maisha yangu hayajabadilika. Nilipokuwa waziri kwenye msafara wangu sikutaka magari yasimamishwe ili nipite. Kwa sababu nilikuwa nafahamu kuna wengine walikuwa wanawahi ndege "airport', wengine wagonjwa na wengine makazini sikutaka kuwachelewesha. Nilikuwa mtu wa kawaida (Mtu wa Watu), ndio maana sioni tofauti na sasa nilivyobaki na ubunge pekee".

Rais Magufuli alivyokutumbua Ulijisikiaje? Ulikasirika?

"Nilisema nilipokuwa kwenye mkutano jimboni kwangu Iramba, nilimshukuru sana Rais wangu John Magufuli kwa kunipa nafasi hiyo ya uwaziri. Sisi ni wafugaji, siku baba akikwambia usiende kuchunga utakasirika? Huwezi".

Vipi kuhusu kugombea urais 2020?

"Kwa kazi nzuri anazofanya Rais wetu John Magufuli, kila mwanaCCM anajua na kufahamu. Kwa sasa nipo bize na jimbo langu, sina mpango wa kugombea URAIS".

Ishu ya "Askari'' aliyemtolea Nape bastola.

"Sikuwahi kusema sio askari. Nilisema sio Polisi. Nilimwelekeza IGP kuchukua hatua aliniambia yule jamaa sio polisi. Kuna utaratibu wa kuchukua hatua na sio kila hatua inatangazwa kwenye vyombo vya habari"

Wana-Singida wakikuuliza Tundu Lissu yuko wapi huwa unawajibu nini?

"Wanasingida wote wanajua kilichotokea na wanazo taarifa za maendeleo yake. Wanajua alipo. Tatizo lililopo ni ukinzani wa taarifa zinazosambazwa na kunyoosheana vidole hasa na chama chake. Mfano kwenye uchaguzi mdogo walikuwa wanasema msiwape kura hawa wamempiga mwenzetu. Jambo ambalo sio sawa.

"Tundu Lissu aliposhambuliwa, Rais Magufuli alinipigia simu akanipa maelekezo kuchukua hatua haraka sana na wahalifu wakamatwe haraka sana’’

Zaidi kuhusu ishu ya Lissu tazama kipande hiki;

Wanasiasa waoga hawawezi kusema ukweli wanaojua bali yale boss wao anayotaka kuyasikia
 
Mwigulu nilimuona mjinga sana kipindi kama kile allibidi aonyeshe ushirikiano yule ni ndugu yake mtu wa Singinda umri bado Lissu unamruhusu kua mtu yoyo Tanzania hii Mwigulu akabaki kuwalamba viatu Waliomteua
 
Walinzi walikuwa wapi na nani aling'oa CCTV baada ya shambulio?! Nashangaa maswali haya hayajibiwi na wanaowahoji hawaulizi maswali haya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Kungoa CCTV camera baada ya shambulio sio kwamba huwezi pata matukio yaliotokea kabla ya kungoa camera.
Mfumo wa Closed Circuit Television System (CCTV )una Camera,Recorder,Monitor kwa uchache.
Ni wazi KAMA Mfumo ulikuwa active wakati wa shambulio Recorder ili record,na sio hiyo kama kuna viunganisho kama TV,au Monitor au hata smart phone iliona.
Watu wanagangania camera camera,lakini kuna zaidi ya camera.
Bado kuna smart cheap CCTV System za watu wakawaida,kwa shs.laki mmoja tu au chini yake
Ukisikia vyombo vya kipolisi vimekaa kimya ujue wana mambo mazito,wanasubiri mtu ajisahau katika maelezo.
 
Attachments

  • main-qimg-010ec171b8bb898854605e4bf349eb29.jpeg
    main-qimg-010ec171b8bb898854605e4bf349eb29.jpeg
    38.6 KB · Views: 17
"Tulimumu, hii habari ya walinzi walikuwa wapi mbona ni ya kijinga- hivi nani aliwafungulia geti Mh. Lissu na DREVA wake? Na mlinzi wa Mh. LISSU naye alikuwa wapi?

..kwa hiyo walinzi walikuwepo?!

..Na unasema ndio waliofungua geti.

..Je waliwahoji washambuliaji ni kina nani na wamemfuata nani Area D?

..Je, walinzi walishuhudia shambulio?

..Washambuliaji walitoka vipi ktk eneo la area D?

..Je, walifunguliwa geti na walinzi?
 
Hongera Dr Mwigulu kwa kuweka wazi msimamo wa Mhe Rais/serikali punde tu baada ya Lissu kushambuliwa.Watu wanadhani kila hatua ya uchunguzi sharti iwekwe wazi kwa umma wakati kuna taratibu za kiintelijinsia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe Mwigulu ndo aliyesababisha uchunguzi wa tukio hili usitishwe au umesitishwa na mrithi wake? Unapotaka kutetea udhalimu jipange Mwigulu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..kwa hiyo walinzi walikuwepo?!

..Na unasema ndio waliofungua geti.

..Je waliwahoji washambuliaji ni kina nani na wamemfuata nani Area D?

..Je, walinzi walishuhudia shambulio?

..Washambuliaji walitoka vipi ktk eneo la area D?

..Je, walifunguliwa geti na walinzi?
Haya maswali ya kinoko hayawezi kupata jibu piga UA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya maswali ya kinoko hayawezi kupata jibu piga UA.

Sent using Jamii Forums mobile app

..kuna watu wanadhani wanaitetea serekali kumbe ndiyo wanaidhalilisha.

..bora hata wangesema walinzi wote walikuwa msalani kwa haja kubwa, ndipo tukio likatokea.

..lakini hii ya kusema walinzi walikuwepo na walifunguliwa geti ni mbaya kwa upande wa serekali.
 
..kwa hiyo walinzi walikuwepo?!

..Na unasema ndio waliofungua geti.

..Je waliwahoji washambuliaji ni kina nani na wamemfuata nani Area D?

..Je, walinzi walishuhudia shambulio?

..Washambuliaji walitoka vipi ktk eneo la area D?

..Je, walifunguliwa geti na walinzi?
JokaKuu, unautando kwenye ubongo- ebu tuanze upya
makazi ya Mh. Lissu kama alivyojaribu kutuaminisha yanalindwa na hii pengine inamaana ya kusema kuwa pana geti linalokuwa limefungwa mda wote na hufunguliwa pale mtu au gari linapoingia na kutoka. Sasa yametolewa maelezo au hoja ya kwanini walinzi waliondolewa. kama waliondolewa inaamana hata mfunga na mfungua geti hakuwepo. SWALI. NANI ALIWAFUNGULIA GETI AKINA MH. LISSU?
 
..kuna watu wanadhani wanaitetea serekali kumbe ndiyo wanaidhalilisha.

..bora hata wangesema walinzi wote walikuwa msalani kwa haja kubwa, ndipo tukio likatokea.

..lakini hii ya kusema walinzi walikuwepo na walifunguliwa geti ni mbaya kwa upande wa serekali.
JokaKuu, HII NDIYO SHIDA YAKO - UNAHISIA KUWA KUNA WATU WANATETEA SERIKALI WAKATI SIYO KWELI ILA WANAJADILI HOJA
 
Mwigulu Mwigulu unatafuta uteuzi au ni kuomba huruma kwa WaTz kwa maovu yako

Sasa alikuagiza uwakamate Ulishawakamata wako wapi??

Siku ya kufa nyani miti yote huteleza

Ndipo mlipofikia
Mungu atawaadhibu tu
 
JokaKuu, unautando kwenye ubongo- ebu tuanze upya
makazi ya Mh. Lissu kama alivyojaribu kutuaminisha yanalindwa na hii pengine inamaana ya kusema kuwa pana geti linalokuwa limefungwa mda wote na hufunguliwa pale mtu au gari linapoingia na kutoka. Sasa yametolewa maelezo au hoja ya kwanini walinzi waliondolewa. kama waliondolewa inaamana hata mfunga na mfungua geti hakuwepo. SWALI. NANI ALIWAFUNGULIA GETI AKINA MH. LISSU?

..na ni nani aliwafungulia geti washambuliaji wakati hawahusiki kuingia area D.

..na nani aliwafungulia geti washambuliaji wakati wanaondoka?

..je, walinzi walichukua hatua gani baada ya kuona Mh.Lissu anashambuliwa?

..Je, walinzi hawana dhamana na usalama wa TL? JE, wameelekezwa kulinda viongozi wa serekali tu, na siyo vyama vya upinzani?
 
JokaKuu, nakubaliana na wewe kabisa; na kwa vile nakubaliana na wewe USIKATAE KUKUBALINA NA MIMI KUWA HOJA YENU KUWA WALINZI WALIONDOLEWA HAINA MASHIKO
 
Back
Top Bottom