Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,906
- 4,840
Waziri wa fedha Mhe.Dkt. Mwigulu Nchemaba leo mei 22,2024 Bungeni Jijini Dodoma amesimama kujibu hoja za wabunge waliochangia bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2024/2025 ya Wizara ya Viwanda na Biashara
Katika majibu yake Dkt. Mwigulu amesema kuwa mtu yoyote anayekusanya fedha ya Serikali ni lazima aifikishe sehemu husika
Dkt. Mwigulu amesema haiwezekani kumuachia mtu anayekusanya fedha za watanzania halafu akawa tajiri huku akina mama wajawazito na wanafunzi wanakosa huduma kwa sababu yake