Dkt. Mwakyembe: Sakata la Clouds kwa sasa ushahidi hautoshi kufanya maamuzi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
WanaJF,

Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo amejibu swali la waandishi kadhaa wa habari waliomhoji mapema leo baada ya kuapishwa katika viunga vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mwakyembe amenukuliwa akisema maneno yafuatayo juu ya sakata hilo lililotikisha vichwa vya habari nchini kwa juma moja sasa.

"Ninachokijua kuhusu tukio la Clouds Media kinatokana na vyombo vya habari, sidhani kama taarifa hizo zinatosha mimi kutoa uamuzi"-Waziri Mwakyembe

Kutosha au kutokutosha sio hoja ila inatakiwa atupe na yeye time frame ya ni lini atatupa upande wake wa report kama upande wa muhimu uligoma kushirikiana kwa maelezo ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa na nape.
Haki itendeke waziri ili wananchi wafanyakazi Bila manung'uniko ya upande flani wa waliochini ya sheria wanapendelewa
 
WanaJF,

Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo amejibu swali la waandishi kadhaa wa habari waliomhoji mapema leo baada ya kuapishwa katika viunga vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mwakyembe amenukuliwa akisema maneno yafuatayo juu ya sakata hilo lililotikisha vichwa vya habari nchini kwa juma moja sasa.

"Ninachokijua kuhusu tukio la Clouds Media kinatokana na vyombo vya habari, sidhani kama taarifa hizo zinatosha mimi kutoa uamuzi"-Waziri Mwakyembe

Mhu! Sidhani kama kuna jipya katika hili kama Nape aliishia hapo alipoishia.
 
Back
Top Bottom