Dkt Mvungi: Muungano Ulishavunjika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dkt Mvungi: Muungano Ulishavunjika!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Buchanan, Aug 25, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nimeangalia kipindi cha Pambanua cha Channel Ten ambapo David Ramadhan alikiongoza akiwa amewakaribisha Dkt Sengodo Mvungi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Alex Mgongolwa wa Kituo cha Haki za Binadamu ambapo Dkt Sengodo Mvungi amedai kwamba mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 ya kuanzisha "Nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" ni kuvunja Jamhuri ya Muungano kwa sababu nchi ni Jamhuri ya Muungano na si vinginevyo. Kwa hiyo Jamhuri hiyo ilishavunjika tangu mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ambayo alidai kwamba "yalichomekewa!" Ni kwa sababu kulikuwa na swali kwenye kura za maoni: "Je, unataka mabadiliko ya Muundo wa Serikali baada ya uchaguzi wa Oktoba, 2010" ambalo alidai ni swali pana sana! Katika Orodha ya Mambo ya Muungano Dkt Mvungi alidai kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano nayo ni jambo la Muungano, kwa hiyo kuivunja Katiba hiyo ni kuvunja moja kati ya mambo ya Muungano. Pia amedai Wagombea wenza ni "batili" kwa sababu wanatoka "katika nchi nyingine!" Amedai kwamba saratani imeula Muungano wetu mpaka uko mahututi, tutafute suluhisho la kuachana na wazanzibari kwa amani tusije tukapigana. Tutapendana zaidi kuliko Wakenya na Waganda!

  Kwa upande wa Alex Mgongolwa amedai kwamba tukae chini tutafute suluhisho kwa mazungumzo.

  JK wetu ndio huyo hana habari kwamba hata urais wake wa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" haupo! Tujadili!
   
 2. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Lol... Kazi ipo... Hana habari JK yupo zake Kagera ana-campaign URAHISI wa Tanganyika bila ya kujua...
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Anagombea urais wa nchi ambayo haipo kisheria! Kaaazi kweli kweli!
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Huyu Profesa wenu mushkila!
   
 5. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Sasa basi itabidi tuiweke kisheria, ukiangalia baadhi ya mambo utagundua Tanganyika ipo, kunamawaziri ambao si wa mungano hawa ni watanganyika, ukiangalia nembo ya Tanganyika ndio nembo ya Tanzania. Kwahiyo Tanganyika ipo lakini sio kisheria, na wazenj wamepiga kelele sana muungano unamatatizo,
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hivi huko kwenye kampeni hawatoi muda wa wapiga kua kuuliza maswali. Au ndo danganya watoto wanapangwa watu kuuliza maswali ya ya kitoto.

  Huu muungano kwa maoni yangu unaweza kusurvive zaidi CUF wakishindaat least kwa muda fulani.Lakini sio CCM. CUF watahitaji muungano sana kuongoza zenj. CCM zenj wanataka kuchomoka kivyao as soon as possible.
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hivyi ninyi mnamlalamikia nani?
  hakuna kiongozi wa nchi hii ambaye anajali masuala ya muungano.
  Dawa ni kwenda mahakamani kuishtaki jamhuri na serikali ya zanzibar kwa kutishia uhai wa UWEPO WA TANZANIA
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  Buchanan, namkubali Prof. Mvingi kama msomi wa sheria aliyebobea kama ambavyo nitamkubali Prof. Mwakiembe, ila sizikubali comments zake kwenye baadhi ya issues kwa sababu yeye Mvungi, ameshajipambanua kushiriki siasa, na ndivyo ambavyo Prof. Mwakiembe atakavyo jipambanua kulinda mauza uza yote ya CCM.

  Honest opinion kwenye hili, inatakiwa kutoka kwa wanasheria independent kama Prof. Shivji.

  Kusu Zanzibar kuwa nchi ndani ya nchi, nilisema yafuatayo,
  Zanzibar na Tanzania ni kama Baba na mwana. Wewe ndiye baba, unaitwa baba kwa sababu ndiye mkuu wa kaya, bread winner mwenye mamlaka yote.

  Inapotokea mtoto wako umpendaye akaanza kulia kutwa kucha kwamba kwa nini ni wewe tuu unaitwa baba, na yeye anataka lazima aitwe baba, na kuendelea kulia kwa makelele mpaka unakosa amani, lakini wife alipomwambia 'nyamaza baba', ghafla alinyamaza na kuanza kufurahi sana, na yeye ameitwa Baba!, akamwambia mama na mimi ni baba. Jee wewe baba wa ukweli, utakasirika au kununa kuwa mwanao amechukua nafasi yako ya kuitwa baba, ama na yeye anataka kuitwa baba jina tuu lakini sio baba chochote, kwa vile powers za ubaba hana!.

  Ndivyo ilivyo kwa JMT, Zanzibar kwanza walianza kwa kuomba bendera yao, wakapewa, kisha wakaomba wimbo wao wa taifa, wakapewa, kisha wale wagambo wao, (KMKM na JKU) kumpigia saluti rais wao, wakapewa, ndipo juzi wakajitwalia jina la 'nchi' na kuliingiza kwenye katiba ya Zanzibar ili hali kwenye katiba ya JMT, Zanzibar sio nchi ni sehemu tuu ya JMT. Jee JMT inasababu wa kuwakatalia kujiita majina yoyote inayoyataka hata wakiuita Falme za Zanzibar na kiongozi wao akawa Sultani Seif/Shein etc.

  Zanzibar ni nchi kweli kama Zanzibar ndani ya Tanzania, kama mwanao atakavyoitwa baba ndani ya nyumba yenu, lakini nje ya nyumba, mwanao ni mtoto tuu, hana ubaba wowote mbale ya macho ya umma, ndivyo ilivyo nchi hii mpya ya Zanzibar, ni nchi jina tuu, haina uinchi yoyote mbele ya mataifa, ni nchi jina isiyo na nguvu zozote za dola. Sasa unamashaka na jina tuu?.

  Zanzibar nchi jina!.
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo wazanzibar watapiga kura kuchagua rais wa muungano kwa ajili gani..............wakati mambo yote ya muhimu yaliyokuwa chini ya muungano sasa yapo chini ya zanzibar km nchi....
   
 10. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  alikuwa Harold Sungusia -
   
 11. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu Pasco umesema vizuri lkn si baadaye watataka vya ziada...
   
 12. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Samahani walikuwa Sengondo Mvungi na Harold Sungusia
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, tayari wameshayaomba mafuta na gesi asilia yatolewe kwenye orodha ya Muungano, na pia wamepitisha rasmi sheria ya kura za maoni ili baadaye waje wapige kura ya maoni kuhusu Muungano, hawakujua kuwa Nyerere ni Mkatoliki, ndoa ya Katoliki haina talaka, hata mke alete vitimbi gani vya kudai talaka, ndio maana CCM imemuweka pale Dr. Shein, maana Seif hata akishinda kura, hapewi nchi asijehatarisha muungano wetu huu adhimu ulioasisiwa na waasisi wa taifa letu tukufu.
   
 14. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Walichosema wataalam hao ni kweli na sahihi. Huwezi kuwa na Muungano wa Tanzania na Wakati huo na Nchi ya Zanzibar. Katika moja ya threads nililizungumza hili. Hata huu uchaguzi ni batili kwa sababu nchi inayoitwa Tanzania tayari imeishamegwa kipande na Kisheria haipo. Sijui hata hao wanaowania Ubunge kutoka Zanzibar wanajua wanalolifanya. Kuna mgogoro wa Kikatiba na jambo hili linaweza kutupeleka pabaya. Kwenye Gazeti la Mwanahalisi toleo la Jumatano tarehe 25/8/2010 kuna mada inazungumzia suala hili.
   
 15. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mfano huu si mwafaka. Mfano stahiki ni ule mtoto anataka kurithi mali na madaraka wakati ungali hai. Akizidi kukuzonga bila shaka atakuua. Ndivyo walivyofanya akina Karume na Seif na BLWZ na SMZ.
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Aug 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sorry, kama nimekosea jina la pili!
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Ibara ya 46B ya katiba inasema bayana:
  Wajibu wa viongozi Wakuu wa vyombo vya Mamlaka ya Utendaji kudumisha Muungano
  (1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia uliotajwa katika ibara ya 28 ya Katiba hii, viongozi wakuu wa vyombo vyenye mamlaka ya utendaji
  katika Jamhuri ya Muungano vilivyotajwa katika ibara ya 4 ya Katiba hii, watawajibika, kila mmoja wao katika kutekeleza madaraka
  aliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii au Katiba ya Zanzibar, 1984, kuhakikisha kuwa analinda, kuimarisha na kudumisha umoja wa
  Jamhuri ya Muungano.

  (2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (1), kila mmojawapo wa viongozi wakuu wa vyombo vyenye mamlaka ya utendaji
  katika Jamhuri ya Muungano kabla ya kushika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii ataapa kuitetea na kudumisha
  umoja wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii.

  (3) Viongozi wakuu wanaohusika na masharti ya ibara hiiĀ–
  (a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
  (b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
  (c) Rais wa Zanzibar; na
  (d) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

  Je ni uhaini?????????
   
 18. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #18
  Aug 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  It is treason in strict terms!
   
 19. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  and complicated sort of, to harmonise the Union constitution with the Zanzibar constitution the union constitution must be changed substantially.It means the whole structure of the Union Constituion will change.

  Are the people responsible aware of that ?
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Aug 27, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Is that the way of dealing with the highest criminal act in the land (ie treason), by condoning it?
   
Loading...