Dkt. Msukuma amkosoa Godwin Kunambi kwa kujenga hoteli na Soko la Ndugai, miradi ya hasara tupu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,134
Akichambua Ripoti ya CAG, Dr Msukuma Mbunge wa Geita vijijini amemlaumu Godwin Kunambi aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kutekeleza miradi inayoleta hasara.

Dkt. Msukuma amesema Ujenzi wa Hotel ya nyota 5 ni ubabaishaji mtupu.

Ujenzi wa Soko la Ndugai hauna tija na Fedha iliyowekezwa pale haitarudi.

Ujenzi wa Stendi za Mabasi ya mikoani ni ufisadi mtupu ukiondoa chache za miji mikubwa amesema Msukuma

Kuna haja gani ya Law School kuwepo wakati katika Wanafunzi 700 wanayofanya mtihani kila Mwaka wanafaulu 26 tu amehoji Dokta.

Inawezekana CAG naye huwa anapokea mlungula kwa sababu ziko Halmashauri bobezi kwa ufisadi lakini zimepewa Hati Safi, amesisitiza Daktari wa Heshima

Mwisho Dkt. Msukuma ameshauri utaratibu wa kuwapata Wakurugenzi wa Halmashauri ubadilishwe badala ya kuteuliwa wawe wanaomba kazi kwa kushindanishwa.

Chanzo: TBC
 
Miradi mingi ya Dodoma haitakuja zalisha kutokana na aina ya wananchi wa Dodoma

Treni ya SGR ikimamilika ndo mtaamini Dodoma itapoteza watu kila weekend maana watakuwa na uhakika wa kurudi mapema.

Haya masaa 10 njiani hukera watu, treni ikitumia masaa 4 hadi Dodoma watu watakaa Dsm
 
Stendi ya mabasi haiko mbali kivile, na ukubwa wake ni sahihi kwa sababu unapojenga mradi kama huo lazima uangalie miaka kadhaa mbele. Stendi imetulia na haina vurugu. Kutokuwa na magari mengi kwa sasa ni kufikiria mwisho wa pua.

Hii ni pia kwa soko la Ndugai, pale lilipo inaweza kuonekana mbali lakini lipo kilometa kama 8 kutoka city centre tena pembeni ya barabara kuu Baada ya miaka 10 litaonekana lipo ndani katikati ya Jiji. Kwa mfano kuna Watu wanatoka Tegeta (kilomita zaidi ya 20) kufuata bidhaa Kariakoo kwa hiyo hakuna ajabu, au alitaka lijengwe katikati ya Mji?!!

Kuhusu hoteli, ile siyo nyota tano labda nyota mbili au tatu ikikamilika. Ikipata usimamizi zuri itaingiza faida kwa sababu ipo katikati ya Mji karibu ya maeneo mengi muhimu.

Napinga miradi isiyokuwa na tija, lakini kwa hiyo miradi ya Dodoma ipo sahihi
 
Hivi ukilaumu ujenzi wa stand kubwa kama ile ya Dodoma ina maana utapinga pia ujenzi wa barabra ya njia 6 kule Dar, maana hesabu ya ujenzi wake inapigia miaka takribani 10 au 20 mbele, AU hata ile aiport terminal 3 kule Dar mbona bado sehemu kubwa tu haijaweza kutumika,ni kwa sababu ya hesabu za mbali,ni kweli tunalaumu sasa hivi lakini manufaa yake tutayaona baadaye sana.
 
Stendi ya mabasi haiko mbali kivile, na ukubwa wake ni sahihi kwa sababu unapojenga mradi kama huo lazima uangalie miaka kadhaa mbele. Stendi imetulia na haina vurugu. Kutokuwa na magari mengi kwa sasa ni kufikiria mwisho wa pua.

Hii ni pia kwa soko la Ndugai, pale lilipo inaweza kuonekana mbali lakini lipo kilometa kama 8 kutoka city centre tena pembeni ya barabara kuu Baada ya miaka 10 litaonekana lipo ndani katikati ya Jiji. Kwa mfano kuna Watu wanatoka Tegeta (kilomita zaidi ya 20) kufuata bidhaa Kariakoo kwa hiyo hakuna ajabu, au alitaka lijengwe katikati ya Mji?!!

Kuhusu hoteli, ile siyo nyota tano labda nyota mbili au tatu ikikamilika. Ikipata usimamizi zuri itaingiza faida kwa sababu ipo katikati ya Mji karibu ya maeneo mengi muhimu.

Napinga miradi isiyokuwa na tija, lakini kwa hiyo miradi ya Dodoma ipo sahihi
Unalinganisha upanukani wa Dsm na Dodoma?

Ni miaka 5 toka Serikali ihamie huko ila upanukaji wa mji ni mdogo mno
 
Back
Top Bottom