Dkt. Mpango: Kodi si tatizo Bandarini

Naomba Wachanganuzi wa Uchumi wanijibu tu,

Je ni kwa muda gani na kwa namna gani zoezi hili litaongeza kipato cha taifa na kuboresha maisha ya Watanzania?
 
Wewe hujielewi na huelewi maana ya mizigo ya" Transit". Kwa hyo endelea kutokwa povu
 
....bado kuna vila.za watakuja hapa kusema hili ni tatizo la muda mfupi tu!, eti msijali watanzania, mnaandaliwa maisha mema mbele ya safari!

...hii kazi imeshawashinda wajomba, endeleeni kufukuzana na Lissu tu ndo mnachoweza!
 
Kama walikuwa hawalipi kodi wasije kabisa.. wakafie mbali... tunataka wafanya biashara walipa kodi.. period..!!
 
Wafanyakazi wa bandari kwa kiasi kikubwa inabidi wapewe Lidandaz kwa maana wengi wao hawana kazi za kufanya siku hizi.
 
Hilo ndiyo tatizo la nchi kuendeshwa kwa staili ya ONE MAN SHOW.....

Hashauliki wala haambiliki.......................

Kila kitu anataka kutoa maagizo yeye tu na hataki mtu yoyote atoe sababu zozote za kutotekelezwa kwa maagizo yake......

Tulimsikia JPM akitamba kuwa wacha hizo meli ziende kwenye hizo bandari za nchi ambazo wanazokubali bandari zao kupitisha mizigo bila kulipa kodi!

Lakini Mkuu wa nchi angetakiwa kuwa msikivu zaidi ili kujua sababu halisi za kupungua mizigo bandarini badala ya kufanya conclusion kuwa mizigo hiyo imepungua kutokana na wale waliokuwa hawalipi kodi kuhamishia mizigo yao kupeleka kwenye bandari za nchi nyingine zinazoruhusu bandari zao kupitisha mizigo bila kulipa kodi!

Kauli nyingine ya kibabe ya Mkulu ni ile ambayo alitoa kuwa watalii wasiotaka kulipa VAT waliyoianzisha ni bora wasije nchini, kwa kuwa yeye anataka watalii matajiri wenye uwezo wa kulipa kodi!

Kwa ubabe huo wa Presidaa wetu tayari sekta ya utalii nayo ishapata athari kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa watalii wanaoingia nchini.....

Naamini kwa mwendo huu nchi yetu inaelekea kuwa Zimbabwe nyingine, kwa kuwa hulka ya Rais wetu inashabiana sana na yule Mzee asiyetaka kung'atuka kule Zimbabwe.........
 
 
Sababu Ni udikteta uchwara
 
Hali hii imepelekea uongozi wa mamlaka ya bandari kufuta bandari kavu hii ni baada ya wafanya biashara kuikimbia.
Chanzo itv
Hawajazifuta. Hizo bandari kavu zipo tu ila hazipelekewi mzigo wowote maana bandarini kwenyewe mzigo umepungua kutoka magari 3500 kwa siku mpaka magari yasiyozidi 1500 kwa siku

At last wamekiri kwamba hali ni tete.
 
Safi sana. Kama kweli walikuwa wanalipa kodi na kodi hazijangezeka sana ni kwa nini wakimbie? Acha tupate kidogo tutumie wisely na maisha yatakwenda kwa shida na tutazoea.
 
Kama meli hazitakuja tutawezaje kuuza mbaazi...?na msimu ndio huu umekwisha anza wanunuzi ni wa huko India sisi hapa nchini hatutumii Mbaazi ila kidogo hivi , ukizingatia mbaazi hazivumilii wadudu ni rahisi sana kushambuliwa na wadudu kama meli haziingii nchini Zitasafirishwaje....?
 
....kwa mwendo huu sishangai kusikia Kafulila akisema jamaa keshakopa dola 900 milioni!, wacha wale kenge wa lumumba waje kuleta propaganda uchwara, na bado, mtaumbuka sana kwa unafiki wenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…