Dkt. Mpango: Askari wa Barabarani wakianza kuvaa Kamera itapunguza Rushwa

Tatizo hapa pia wanatengeneza mazingira ya rushwa

Unakuta mtu kashaongea na kampuni ya kuwapa hii tenda mnaanza kutulegeza ila mpige mabilioni

Kipindi Cha lugumi si mlisema serikali imetoa hela vituo vyote vifungwe machine za finger prints nchini, mliishia wapi?
 
Mbinu pekee ni sisi madereva kutegesha kamera ndani ya gari then baadae kuzirusha mitandaoni.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Izingatiwe kuwa kunapotokea makosa dereva ndo anashawishi kutoa elfu tano kuliko kulipa elf thelathini. Askari waboreshewe maslahi yao, faini iwe ya kawaida. Hata 10,000/=
 
Duh,hiyo haitasaidia kitu,watabuni mbinu tu ya kuziminya,kupoteza ela tu uku
Haya ndiyo matatizo makubwa ya nchi yetu. Wanasiasa wanajaribu kubuni suluhisho la matatizo bila kufanya utafiti wa kutosha na kushirikisha wataalam huku wakivutiwa na upigaji. Hizo camera watakosa namna ya kuzichezea? nfact hizo kamera ni nani (ambaye hataki ulaji) ambaye atakuwa anazisimamia? Ujinga mtupu.
 
Mbinu pekee ni sisi madereva kutegesha kamera ndani ya gari then baadae kuzirusha mitandaoni.
Ndiyo maana nimesema hawa wanasiasa wanajaribu kuleta suluhisho la matatizo kwa kutengeneza matatizo mengine makubwa zaidi tena kwa gharama. Wangeshirikisha wataalam na jamii mtu kama wewe una mawazo mazuri sana.
 
Izingatiwe kuwa kunapotokea makosa dereva ndo anashawishi kutoa elfu tano kuliko kulipa elf thelathini. Askari waboreshewe maslahi yao, faini iwe ya kawaida. Hata 10,000/=
Mkuu hawa hawaangalii chanzo cha matatizo bali wake zao ndiyo huwapa ushauri. wazo la kijinga kabisa ametoa na litaongeza gharama bila ufumbuzi.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Wazo zuri na ambalo kwa sasa linatekelezwa nchi zilizoendelea, ila kwa Afrika nchi kama Tanzania sijui ufanisi wake utakuaje...

Serikali ikitaka kuzuia rushwa za barabarani, inapaswa ipunguze au uondoe kabisa human intervention ya askari polisi na kuacha teknolojia ya utambuzi wa makosa ifanye kazi, makosa na faini yawe yanamfikia mkosaji kiteknolojia
 
Nimesoma kichwa cha habari tu sijasoma hayo maelezo mengine, swali langu niii


Atakaekuwa anazomonitor hizo camera na vitendo vyao ni polisi mwenzao?
 
Nimesoma maoni vilivyo,katika yote nakubaliana na mdau aliyependekeza teknolojia iachiwe na cha kuongezea kuwe na barrier patakapofaa, askali kazi yake iwe ni kufunga na kufungua kizuizi pale mwenye chombo cha moto atakapo ingiza leseni yake ya udreva katika mashine maalum ikiwa expired imtengenezee faini ya kulipa mbele ya safari bila kusahau waendesha bodaboda mashine iwascan kama wamevaa element,safety jacket na boot ngumu na pia katika barrier chombo kisimamapo kitafsiri mfumo mzima wa hicho chombo kina kosa gani kati ya indicator,brake,etc kwa hapo rushwa itakoma na asiyelipa faini huko aendako baada ya siku tatu akibainika na mfumo basi isiwe majadiliano bali mahakamani ili ikiwezekana alipe faini zote pamoja na kifungo cha mwezi mmoja,mijeredi kila asubuhi na kazi ngumu hapo tutakomesha rushwa za barabarani.
 
Kabla ya hizo camera waongezeeni kwanza mishahara, mnataka kuua watu njaa - sh 540,000 kwa mwezi mtu ana watoto 5 na wajukuu 6 kweli? Hapo hajalipa kodi ya nyumba na ada za watoto.
 
Back
Top Bottom