Dkt. Modestus Francis Kipilimba: Wasifu wake

Dkt. Modestus Francis Kipilimba: Wasifu wake

Huyu bwana hajawahi kufanya biashara ya aina yoyote katika maisha yake. Kimsingi, naweza kukuthibitishia kwamba hajawahi kumiliki hata duka katika maisha yake,” mmoja wa marafiki wa Dk. Kipilimba aliniambia katika mazungumzo naye wiki hii.
Eyooooo! Nimeipenda hii đź’ť
Biashara ni stress
 
Dunia hii hutakimbia mauaji hata baada ya miaka 10 akistaafu atalipa tu aliyofanya kisheria au kimtaani
 
Correct me if I'm wrong. Mtu aliyetoka TISS na kuja Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo Ramadhani Kahilima? Nakumbuka ndo alikuja kuwa mkurugenzi wa uchaguzi.
Kailima hakuteuliwa na Magufuli

Watu%20wanatokea%20mbali%20sana!.jpg
 
Mkuu huyu jamaa aliondolewa na Magufuli kwa vile alikataa kwenda extremes za ukichaa wa Magufuli.
Aliondolewa unceremoniously.
Mungu amlaani yeye mpaka kizazi chake cha 10

Naamini Dunia inamsubiri kwani wahenga walisema kwa kinyume chake

"... WALIMWENGU HADAA DUNIA SHUJAA ..."

Kwamwe mlimwengu hawezi kuishinda DUNIA
 
Tumekwisha isikia sana hii hadithi, ni wakati wa kuipumzisha, hakuna haja ya kuirudia rudia kila mahali kila dakika. Kila mtu anafahamu maji hulowanisha nguo.
Ukachero ni zaidi ya kufanya kazi za kawaida na vile vile makachero huwa kila sehemu wapo, hata rafiki yako wa karibu waweza kumuamini na kumpa siri zako za ndani kumbe mwenzako ni kachero tena mbobezi, huwa na uwezo wa kufanyakazi popote na katika mazingira yoyote tena yaliyojaa usiri.
 
WASIFU MFUPI (CV) WA MKURUGENZI MKUU MPYA WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA, TANZANIA (TISS), DKT MODESTUS KIPILIMBA

Jina kamili ni Modestus Francis Kipilimba

Dini ni Mkristo

Ni mzaliwa wa Morogoro, Tanzania

Alifunga ndoa mwaka 1988, na ana watoto watatu.

Kuanzia Januari mwaka 1973 hadi Novemba mwana 1976 amesoma Shule ya Sekondari Kingonsera iliyopo Mbinga mkoani Ruvuma. Kidato cha 5 na 6 amesoma Mkwawa High School iliyopo mkoani Iringa. Shahada ya kwanza amesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika masuala ya Kompyuta.

Shahada ya Uzamili (Masters Degree) alisoma nchini Uingereza katika chuo Salford, Manchester ambapo alisomea masuala la Kompyuta tangu Septemba 1992 hadi Novemba 1994.

Shahada ya Uzamivu (PhD) alisoma katika chuo hicho hicho cha Salford kilichopo Manchester Uingereza, kutoka Februari 2002 hadi Septemba 2005.

Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Tarehe 15 Februari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Dkt. Kipilimba alijaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dickson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Tarehe 24 Agosti, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Mafunzo alipata lini
 
Back
Top Bottom