InvisibleTarget
JF-Expert Member
- Dec 20, 2014
- 1,126
- 2,122
Napingana sana na watu kama hawa, wanaotaka kutuaminisha kuwa siasa za Mwl Nyerere zilikuwa bora sana kuliko za leo.
Nyerere aliye binya uhuru wa kupata habari kiasi cha kutulazimisha kusikia mapambio ya siasa za ujamaa kupitia RTD pekee. Kulazimisha wote tutumie radio zisizo na masafa ya kupata taarifa toka nje ya Tanzania (177) maarufu Mkulima na ukibahatika kuipata yenye masafa hayo unasikilizia uvunguni.
Watu binafsi walinyimwa uhuru wa kuzalisha mali kwa kutengenezewa taswira ya ubepari na kutiwa kizuizini, kiasi wenye hasira waliua wakuu wa mikoa na kunyongwa. Ukiingia bar unahesabiwa vizibo vikizidi unadakwa ukaeleze umepata wapi pesa ya kununua chupa 24 na huwezi kumnunulia rafiki yako isije kuwa kesi.
Tulilazimishwa kutumia baiskeli hata kama una uwezo wa kuwa Peargot lazima ujadiliwe na Kamati kuu ya TANU kama unastahili sifa za kuwa na gari hiyo vinginevyo tumia baiskeli ya Swala.
Hatukuwa na uhuru wa kujumuika na kuongea juu ya serikali na mkiipata mnaongea kwa kunong'onezana tukiaminishwa Ikulu inasikia lolote linaloongelewa juu ya serikali.
Lwaitama usitukumbushe ya Nyerere
Acha upuuzi kumsema vibaya Baba wa Taifa, Huna Adabu. Unashindwa kuheshimu hata Umoja wa Kitaifa aliouhasisi yeye kwa kuunganisha kabila zaidi ya 100 tukawa kitu kimoja na kuishi kwa Amani ambayo inakufanya hadi saizi upo una-type upuuzi huu au ujui kuna nchi zina makabila hata 20 hayafiki lakini hadi leo hii wameshindwa kuwa kitu kimoja na kujiona wao Taifa moja.
Unashindwa kuheshimu hata namna alivyoweza kulinda Rasilimali za Nchi ambazo hadi leo hii kwa namna moja au nyingine zinatunufaisha au unadhan alishindwa kuwapa mataifa wakamjaza pesa akaishi starehe na anasa kama baadhi ya maraisi wa Africa walivyofanya.
Tuwe watu wa Shukrani ulitaka awe Perfect kwa kila kitu kwani umeambiwa yeye alikuwa ni Malaika ?Unajua ni ugumu gani aliupata kuwaongoza watu waliotoka kutawaliwa kikoloni huku wengi wao wakiwa hawana uelewa wa mambo ya maendeleo..et unazungumzia Redio..kwa hiyo ulitaka aachilie uhuru wa Media watu wajazwe propaganda na uelewa wao kwa wakati huo utokee mtifuano ili mkoloni ajipenyeze aendelee kuvuna rasirimali au unadhan baada ya mkoloni kutoa uhuru alipenda kuona tupo wamoja.
Kila jambo na wakati wake, Ndio maana wenye akili zaidi yako walichuja mema na mabaya yake wakaona anastahili apewe heshima ya BABA WA TAIFA na Wengine wakaenda mbali zaidi wakakubaliana awe MWENYE HERI wewe endelea tu kushiba na kuandika propaganda zako za kipuuzi hazitakusaidia lolote.