Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Huyo mzee atawapata hawa wadogo zetu ambao hawakuwa wamezaliwa enzi za awamu ya kwanza.Napingana sana na watu kama hawa, wanaotaka kutuaminisha kuwa siasa za Mwl Nyerere zilikuwa bora sana kuliko za leo.
Nyerere aliye binya uhuru wa kupata habari kiasi cha kutulazimisha kusikia mapambio ya siasa za ujamaa kupitia RTD pekee. Kulazimisha wote tutumie radio zisizo na masafa ya kupata taarifa toka nje ya Tanzania (177) maarufu Mkulima na ukibahatika kuipata yenye masafa hayo unasikilizia kwenye uvunguni.
Watu binafsi walinyimwa uhuru wa kuzalisha mali kwa kutengenezewa taswira ya ubepari na kutiwa kizuizini, kiasi wenye hasira waliua wakuu wa mikoa na kunyongwa. Ukiingia bar unahesabiwa vizibo vikizidi unadakwa ukaeleze umepata wapi pesa ya kununua chupa 24 na huwezi kumnunulia rafiki yako isije kuwa kesi.
Tulilazimishwa kutumia baiskeli hata kama una uwezo wa kuwa Peargot lazima ujadiliwe na Kamati kuu ya TANU kama unastahili sifa za kuwa na gari hiyo vinginevyo tumia baiskeli ya Swala.
Hatukuwa na uhuru wa kujumuika na kuongea juu ya serikali na mkiipata mnaongea kwa kunong'onezana tukiaminishwa Ikulu inasikia lolote linaloongelewa juu ya serikali.
Lwaitama usitukumbushe ya Nyerere
Meza za magazeti pale posta mpya Jumatatu mpaka ijumaa zilikuwa na magazeti mawili tu Daily News na Uhuru, Jumamosi linaongezeka mfanyakazi.
Enzi zetu meza za magazeti zimejaa ya kila sina, kwenye mitandao kila mtu anaandika anachotaka.
Anachosahau huyo mzee ni kwamba kuna maisha ya wanaharakati yapo mtandaoni na kuna maisha halisi huko mikoani, awamu hii inapambana ili maisha halisi yaboreshwe.