Dkt. Lwaitama: Hawa jamaa (CCM) wakiendelea hivi, hata mwakani chama pinzani chenye kujiheshimu kitajitoa

Napingana sana na watu kama hawa, wanaotaka kutuaminisha kuwa siasa za Mwl Nyerere zilikuwa bora sana kuliko za leo.
Nyerere aliye binya uhuru wa kupata habari kiasi cha kutulazimisha kusikia mapambio ya siasa za ujamaa kupitia RTD pekee. Kulazimisha wote tutumie radio zisizo na masafa ya kupata taarifa toka nje ya Tanzania (177) maarufu Mkulima na ukibahatika kuipata yenye masafa hayo unasikilizia uvunguni.

Watu binafsi walinyimwa uhuru wa kuzalisha mali kwa kutengenezewa taswira ya ubepari na kutiwa kizuizini, kiasi wenye hasira waliua wakuu wa mikoa na kunyongwa. Ukiingia bar unahesabiwa vizibo vikizidi unadakwa ukaeleze umepata wapi pesa ya kununua chupa 24 na huwezi kumnunulia rafiki yako isije kuwa kesi.

Tulilazimishwa kutumia baiskeli hata kama una uwezo wa kuwa Peargot lazima ujadiliwe na Kamati kuu ya TANU kama unastahili sifa za kuwa na gari hiyo vinginevyo tumia baiskeli ya Swala.

Hatukuwa na uhuru wa kujumuika na kuongea juu ya serikali na mkiipata mnaongea kwa kunong'onezana tukiaminishwa Ikulu inasikia lolote linaloongelewa juu ya serikali.

Lwaitama usitukumbushe ya Nyerere

Acha upuuzi kumsema vibaya Baba wa Taifa, Huna Adabu. Unashindwa kuheshimu hata Umoja wa Kitaifa aliouhasisi yeye kwa kuunganisha kabila zaidi ya 100 tukawa kitu kimoja na kuishi kwa Amani ambayo inakufanya hadi saizi upo una-type upuuzi huu au ujui kuna nchi zina makabila hata 20 hayafiki lakini hadi leo hii wameshindwa kuwa kitu kimoja na kujiona wao Taifa moja.

Unashindwa kuheshimu hata namna alivyoweza kulinda Rasilimali za Nchi ambazo hadi leo hii kwa namna moja au nyingine zinatunufaisha au unadhan alishindwa kuwapa mataifa wakamjaza pesa akaishi starehe na anasa kama baadhi ya maraisi wa Africa walivyofanya.

Tuwe watu wa Shukrani ulitaka awe Perfect kwa kila kitu kwani umeambiwa yeye alikuwa ni Malaika ?Unajua ni ugumu gani aliupata kuwaongoza watu waliotoka kutawaliwa kikoloni huku wengi wao wakiwa hawana uelewa wa mambo ya maendeleo..et unazungumzia Redio..kwa hiyo ulitaka aachilie uhuru wa Media watu wajazwe propaganda na uelewa wao kwa wakati huo utokee mtifuano ili mkoloni ajipenyeze aendelee kuvuna rasirimali au unadhan baada ya mkoloni kutoa uhuru alipenda kuona tupo wamoja.

Kila jambo na wakati wake, Ndio maana wenye akili zaidi yako walichuja mema na mabaya yake wakaona anastahili apewe heshima ya BABA WA TAIFA na Wengine wakaenda mbali zaidi wakakubaliana awe MWENYE HERI wewe endelea tu kushiba na kuandika propaganda zako za kipuuzi hazitakusaidia lolote.
 
aisee mbona uko bize kujibu maswali ambayo hayapo mezani.Unaenda OP.unachokisema sicho alichokisema Lawitama mkuu rudi kwenye mada
Kingine anachopotosha jamii ni ukweli kuwa kuanzia awamu ya kwanza nchi imekuwa ikisomesha wataalam, ni lazima ufike muda wale waliosomeshwa wakatumia maarifa yao kwa faida ya wote.

Hatuwezi kuwa na mindset ya siasa tu wakati taifa linavidai vizazi maendeleo yenye kuonekana.
 
aisee mbona uko bize kujibu maswali ambayo hayapo mezani.Unaenda OP.unachokisema sicho alichokisema Lawitama mkuu rudi kwenye mada
Ninaifahamu vyema mindset ya huyo msomi, nilichokiandika ni sehemu tu ya mawazo yake yalivyo. Huyo ni mwana CDM na anayo haki ya kuchagua ni aina ipi ya maoni awe nayo.
 
Kumbe unaongea ya kwako siyo Mada basi lete mada yako hiyo tuidiscuss. Watu wenye akili hujadili kwanza hoja ya msingi na hayo mengine huja baadae.Tuongee kwanza alichoksema maana hapo ameongelea effect ya kinachotokea kwa hapo baadae.Watanzania sijui tumelogwa na nani kwa nini huwa hutusikilizi kwanza ndio tujadili.
Ninaifahamu vyema mindset ya huyo msomi, nilichokiandika ni sehemu tu ya mawazo yake yalivyo. Huyo ni mwana CDM na anayo haki ya kuchagua ni aina ipi ya maoni awe nayo.
[/QUOTE
 
November 26, 2019

Humphrey Polepole katibu Uenezi wa CCM abishana vikali na mwandishi wa BBC kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo CCM imeibuka na 'ushindi wa kishindo' wa asilimia 99.9 na huku wachunguzi wa kisiasa wakiwemo viongozi wa vyama kama Augustino Lyatonga Mrema wa TLP walia uchaguzi kuchafuliwa :
  1. Fursa ya kujipima mtaipata vipi ikiwa vyama vikubwa vimejitoa
  2. Mtajipima mnakubalika vipi ikiwa mmeshiriki wenyewe tu
  3. Mtafanya tathmini gani ya kisiasa
  4. Ushindi wa kisheria ni tofauti na ushindi wa kisiasa, CCM mnasemaje kuhusu hilo ?
  5. BBC Inatisha suala hili likijirudia 2020, Humphrey Polepole asema halitishi
  6. Katika mitaa zaidi ya 500 Dar es Salaam ni mitaa miwili tu uchaguzi wa ushindani umefanyika

Source: ABC Habari
 
Augustino Lyatonga Mrema atoa maneno mazito kijijini Kiraracha Moshi vijijini nchini Tanzania kuhusiana na uchaguzi ulivyovurugwa aapa kwenda kwa Mh. Rais kumwambia hali hiyo mbaya ya kisiasa na kwa uzoefu wake kama naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani miaka ya nyuma hali hii ni hatari kwa nchi kifupi nanukuu 'anasema hakuna nchi'
 
'Hakuna demokrasia inji hii' - Augustino Mrema awaambia viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro waliokuwa wanapita kukagua zoezi la upigaji kura linavyoenda

 
Lwaitama=la shavu
Lui lwaitama=kofi la shavu
Lwaitama=kofi la shavu

Naona anazidi kutoa vibao vya mashavu kwa watawala
 
Wewe hopeless! Lazima ujue credibility ya huyo anayetoa hiyo hoja kabla ya kuanza kuijadili. Sasa hoja ya commedian inaweza ikawa siyo hoja bali kioja! Ndiyo hichi kioja cha Lwaitama ukikiingia kichwa kichwa anakuacha peupee unaogelea mwenyewe!
Watu wangapi walioko serikalini wenye PhD na huongea utumbo na ku-discredit credibility zao na kujitoa ufahamu waziwazi plus unafiki wa hali ya juu?wewe ushaongezwa kwenye list ya mwenzio kawe alumni na mnashea nae kapu moja la ujinga kuanzia sasa.
 
Walichokifanya hawa wanaojiita CCM mpya si wizi hapana bali ni Uporaji.

Mwizi anakuvizia kisha anakuibia unashtuka huna simu....Mporaji anakuja live live anachukua ulichonacho na huna mamlaka ya kujitetea, anaweza kukumaliza.
 
Yaani Lwaitama "Commedian" naye wakumwamini kiasi hicho? Kwali mmechanganyikiwa na hammjui Lwatama! Hana lolote huyo mnapoteza muda wenu tena huwa anataka kuwaaminisha yeye kuwa ni Prof. wakati ni uongo hajafikia level hiyo!
Hv Prof wa fisiem anamfikia Dr Lwaitama kwa nondo? yule Prof wa jalalani anabanwa kidogo na maswali ya mwandishi anaanza kutoa macho tu
 
Na yeye na wenzake ndio waliokuwa waalimu wa Siasa, wakituaririsha zidumu fikra za Mwalimu. Wakimaanisha wao na usomi wao walikuwa hawana uwezi wa kufikiri kama JKN.
aliyewakaririsha leo hii yeye ni chadema! na ninyi, je? hamjiulizi kitu? mnajikaririsha ujinga mwenyewe!
 
Back
Top Bottom