Dkt. Hussein Mwinyi ndie kiongozi mstaarabu kuliko yeyote Tanzania

Kama anasifa apewe tu Maji hufuata mkondo mbona Karume amekuwa Raisi na Baba yake alikuwa Raisi.
Zanzibar hiyo. We should avoid mambo hayo. Yataanza kujenga dhana ya kupasiana madaraka.
 
Kwani Mzee wa skafu umesikia akimpigia kelele nani?

Kunakupiguwa kelele nakupiga kelele

Je umeshasikia JWTZ wakilushiwa lawama zozote kama ilivyo kwa jeshi la polisi kulaumiwa kwa utendandaji mbovu, kuegemea chama tawala, kamatakata, watu kuokotwa wamekufa hovyo nk

Yoote hiyo inamhusu mzee wa skaf hatakama yeye kauchuna raia watamsema

Je huyo wamajeshi???????....
 
Uko sahihi kabisa alipewa malezi bora na Mzee mwinyi, pia amesimamia wizara nyeti muda mrefu.
Kwanini mpate shida tizameni mzee wake,mzee(rais alli hassan mwinyi) ni mtu mwenye haiba ya ucha mungu,mnyenyekevu asie na makuu,mwenye busara na hekima nyingi,mtulivu sana asiye na papara huwezi kumsikia akisema hadi atakiwe kusema,mzee huyu mola amemjaalia mambo mengi mazuri.

M/Mungu anasema kwenye qur an tukufu kuwa "aliyepewa hekima basi amepewa heri nyingi"basi pasi na shaka mzee huyu kapewa heri nyingi sana ikiwemo na umri na siha njema (92 yrs) tena akiwa imara kweli kweli sio jambo jepesi.

Sasa baadhi ya haiba,tabia na malezi bora aliyoyapata toka kwa mzee wake huyu(rais mwinyi) ndio yaliyomtengeneza dr hussein kuonekana kama tunavyomuona na kumsifu leo bila kujua kilicho nyuma yake naam...... nami ntakwambieni...,(nyuma ya haiba ya dr hussein wapo wazee wake waliyemlea vyema),malezi yana nafasi kubwa sana katika kumjenga haiba ya mtu mbele ya jamii tujihimize kuwalea vizazi vyetu katika maadili mema na hasa ya dini bila shaka utakuwa umetengeneza mtu mwenye haiba nzuri sana mbele ya jamii.

Waswahili (wahenga) wanamsemo wao kuwa "huwezi okota embe chini ya mti wa mwarobaini" ...huwezi pata mtu mwenye haiba ya dr hussein kwa mzazi asiyefanana naye kimaadili na kihaiba.
Haiba ya dr hussein ina akisi malezi bora kutoka kwa wazee wake.
 
Namsifu sana huyu waziri asiyependa majivuno, hana vijembe hakika huyu ndiye anastahili kupewa wadhifa mkubwa na kutupeleka inchi ya maziwa na Asali.
Tatizo ni chama kilichomlea na wastaafu wanao mzunguka.
Ila naamini 2025 watampa kupeperusha bendera anafaa

.. Ustaarabu hatutaki, tunataka maendeleo kama ya Rais wetu JPM..
 
Hamna hata anaye mjua! wadau wa sheria hasa watetezi wa mambo ya "Cameron" watakua anamjua na skandali ileeee....mwananyamala deshi deshi! ..Mafia hatari huyo!
 
Anaongoza JWTZ

Ata mpigia kelele nani kule?

Apewe mambo yandani kama hajageuka kituko in few weeks
True, Kule JWTZ anafanyakazi na wasaidizi ambao karibu wote wanamiliki nishani za utumishi uliotukuka. Na vilevile scandals za hiyo wizara hasa zile zinazohusisha JWTZ huwa hazivuji hovyo na hata zikivuja hakuna mwanasiasa wala media inayothubutu kuzivalia njuga hadharani tofauti na wizara za maliasiri au nishati nk.
 
huyu bwana sio kiongozi mzuri hapendi kujichangany na watu W/ulinzi inambeba sana akitupwa kwingine ataumbuka, n muda mwafaka pia mkawamkumbuk vijana wa hayati Jk Nyerere japo mmoja miongon mwao akiwa future president sio mbaya ili kumuenzi mwasisi wa taifa hili,
akina nani hao?
 
Kiukweli Hussein Mwinyi anajielewa na hana purukushani ni mtu wa kimyakimya hafanyi kazi kwa kujionesha ktk vyombo vya habari
 
Hajawahi kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani

1) Alianza naibu Waziri wa Afya enzi za Mzee Mkapa waziri akiwa Anna Abdalla
2) Akateuliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano) wakati wa JK
3) Akateuliwa Waziri wa Ulinzi
4) Akatuliwa Waziri wa Afya
5) Akarudi tena Ulinzi
6) Awamu ya JPM akabakishwa Ulinzi

Kwa maoni yangu ni kweli ni Kiongozi Mkimya na mstaarabu lakin kwa siasa zetu za wakati huu hafai kuwa Rais kwa kuwa sio Mtu wa kujichanganya na sio Creative kiasi cha kuweza kufanya Maamuzi na kuyasimamia!

Mwigulu Nchemba au Hamis Adrea Kigwangala wanafaa sana kuwa Ma Rais wa awamu ya sita

kwa Maoni yangu Paul Christian Makonda anafaa sana kuwa Waziri Mkuu kwa kuwa hayumbishwi na shutuma, kwenye hilo namfananisha na Hayati Mzee Kawawa alivyokuwa ndio taulo la kufutia Uchafu wa Mwl Nyerere.
Kigwangala baba yake mrundi,nchemba sio kiongozi ana ujuaji na siasa za show..rais ni kiongozi wa nchi..unaposema hachanganyiki unataka achanganyike na nani kwa lengo lipi?
 
Namsifu sana huyu waziri asiyependa majivuno, hana vijembe hakika huyu ndiye anastahili kupewa wadhifa mkubwa na kutupeleka inchi ya maziwa na Asali.
Tatizo ni chama kilichomlea na wastaafu wanao mzunguka.
Ila naamini 2025 watampa kupeperusha bendera anafaa
Huyu MH hata mimi ntampa kura yangu ya Urais
 
Back
Top Bottom