JOYOPAPASI
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 250
- 408
Dk. Hussein Mwinyi chaguo
sahihi kwa Wazanzibar
Na Hamis Shimye
ZANZIBAR na Wazanzibari kwa ujumla wake kwa awamu hii inaenda tena kupata kiongozi aliye bora zaidi na mwenye maono ya pekee katika ukombozi wa Mzanzibari mwenyewe na hata kwenda kuenzi mapinduzi ya Zanzibar ambayo ndio alama ya ukombozi wa Zanzibar na huyo si mwingine bali ni Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Dhana hii inajengwa kutokana na washindani wa mgombea wa Urais wa Zanzibar, Dk. Mwinyi waliojitokeza si watu wenye uwezo wa kusimama naye katika kuendeleza maendeleo makubwa yaliyopatikana na kuletwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM), visiwani humo toka mwaka 1964 pale alipondolewa madarakani Sultani na serikali yake.
Lengo lilikuwa ni kumkomboa Mzanzibar na madhira aliyokuwa nayo enzi za Msultan, ambapo katika kitabu cha masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha, kilichoandikwa na mwandishi Minael-Hosanna Mdundo, Sheikh Kombo anasimulia kuwa “Tumesononeka kwa sababu matumaini yetu yote ya kuupata uhuru wa nchi yetu kwa njia ya vote (kura) yalikuwa yamefutika".
Kitabu hicho kimeelezea mambo mengi, ambayo kwa ujumla Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimeyaenzi toka kwa aliyekuwa Rais wa kwanza, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume na sasa wakati huu ambao Rais Dk. Ali Mohamed Shein, anamaliza muda wake wamefanya mambo makubwa mno na hata kutoa taswira kuwa CCM imekidhi haja na tamanio la Wazanzibar katika kuwaletea maendeleo yao.
Dk. Mwinyi ni tumaini linalokwenda kuendeleza maendeleo yaliyofanywa na viongozi waliotangulia kutokana na kuwa ni kiongozi mwanamageuzi anayekwenda kuleta chachu ya maendeleo kwa Mzanzibar na Zanzibar kwa ujumla, kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kiongozi na wa kuleta maendeleo kwa Wazanzibar, ambao wako mstari wa mbele katika kuendeleza maendeleo waliyoyapata.
Zanzibar inahitaji kiongozi bora mwenye maono ya kusukuma gurudumu la maendeleo lililopo sasa, ambapo sifa za kiongozi huyo anazo Dk. Mwinyi, ambaye amekuwa kiongozi mwenye kujua tafsiri na maana ya uongozi. Dk. Mwinyi ni mfuatiliaji wa mambo, mtendaji kazi, mchukia rushwa kwa vitendo, mpenda maendeleo ya Zanzibar na Wazanzibar kwa ujumla, ambaye ni mtu sahihi wa kushirikiana na Rais Dk. John Magufuli.
Siasa za Zanzibar inahitaji mtu anayepata Urais kwa kusukumwa na tamanio la kuondoa umaskini na kuleta maendeleo na sio mtu anayegombea kwa kupewa fedha na watu au mataifa ya nje ili aweze kupenyeza agenda yao wanayoitaka kwa Wazanzibar. Dk. Mwinyi amekuwa askari mwaminifu katika kuutukuza Uzanzibar na kuleta maendeleo kwa wananchi wa visiwani humo.
Hii inatokana na toka alipochukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM na baadae kupitishwa na Chama kuwa mgombea wake, anayesubiri kuchukua fomu siku Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) itakapotangaza amekuwa mtu mwaminifu, mwadilifu, asiyekuwa na makuu na mtu aliyeridhika na kipato ambacho MwenyeziMungu amemruzuku na hata kutokuwa na tamaa. Huyu ni kiongozi anayefaa kwa siasa za Zanzibar atakayekwenda kushirikiana na Dk. Magufuli
Dk. Mwinyi ni mtu mwenye uthubutu na kama taifa hasa Zanzibar wapo kwenye kipindi na hatua muhimu ya kidemokrasia wakati wanapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, hivyo wanapaswa kumtazama Dk. Mwinyi kama mboni na wasikubali kumpoteza kwani ni mtu anayekwenda kulinda Muungano na kuleta maendeleo ya dhati ya Mzanzibar na si kwenda kuendeleza siasa za 'usultani' kama wengine.
Ubora na uimara wa Dk. Mwinyi kiueledi na kiutumishi ndio mambo yanayomtofautisha na wagombea wengine, ambapo yeye ana sifa za upekee na utofauti wake wa uongozi na anastahili kupewa nafasi ya kuwa Rais wa Zanzibar na sio vinginevyo, huu si upendeleo bali ni ukweli wa kimantiki unaotumia mifumo ya kisiasa kumtambua mtu kulingana na sifa zake za kiuongozi, ambazo zote anazo Dk. Mwinyi.
Japokuwa Zanzibar ilishakombolewa kutoka kwenye makucha ya wakoloni, Dk. Mwinyi ni atazidi kuikomboa Zanzibar kifalsafa, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni, upekee wa kiuongozi aliokuwa nao unasimama katika falsafa ya uweledi, utashi, misimamo na maamuzi ikiwa ni pamoja na kuiva kiitikadi na kitaaluma katika nafasi zote alizoshika ikiwemo ya Uwaziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mantiki hiyo, Dk. Hussein Ali Mwinyi ni chaguo tosha kwa CCM katika kuhakikisha anapeperusha vyema bendera ya chama hicho tawala katika kinyanganyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, kwa kuwa wamempata mgombea sahihi mwenye uwezo na utayari wa kusimamia mapinduzi ya Zanzibar na kuishi kwenye kutekeleza zaidi matamanio waliyokuwa Wazanzibar katika kujikwamua na kujiletea maendeleo.
End