Dkt. Hoseah: Hakuna ubaya kudai Katiba

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015

‘Hakuna ubaya kudai Katiba’​

Sunday September 05 2021​

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk Edward Hoseah amesema si kosa kwa wananchi kudai Katiba Mpya na kwamba wakati umefika kwa mamlaka za nchi kutoa mwongozo mpya wa kufikia hatima ya dai hilo.

‘Hakuna ubaya kudai Katiba’

By Bernard James

Dar es Salaam. Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk Edward Hoseah amesema si kosa kwa wananchi kudai Katiba Mpya na kwamba wakati umefika kwa mamlaka za nchi kutoa mwongozo mpya wa kufikia hatima ya dai hilo.

Akitoa maoni yake binafsi (si ya TLS), Dk Hoseah alisema wanaodai na wasiodai Katiba Mpya nchini, wanapaswa pia kujua kuwa haiwezi na haitakuwa mwarobaini wa kila tatizo linaloikabili nchi au mtu binafsi.

“Hakuna ubaya watu kuomba Katiba mpya. Si kosa, ni mawazo yao, tena nchi hii inaruhusu watu kutoa maoni yao,” alisema Dk Hoseah katika mahojiano na Mwananchi huku akisisitiza mambo mengi yanahitaji kutazamwa kuhusu Katiba Mpya.

“Katiba Mpya haiwezi kuwa mwarobaini wa kila tatizo. Haiwezekani! Angalia Kenya, walipata katiba mpya, nzuri lakini matatizo yako palepale na bado wanataka kubadili katiba vifungu fulani.

“Kwa hiyo unapopata Katiba Mpya haimaanishi kwamba umetatua kila tatizo, bali utafika mahali utasema haya mawazo kwa kipindi hiki si sahihi,” alisema.

Dk Hoseah alisema wakati umefika kwa mamlaka za juu nchini kutoa mwongozo utakaosaidia kulifikisha suala hili mwisho.

“Huu mjadala hauwezi kupata ufumbuzi bila kufika mahali mamlaka ya juu kabisa ikasema ‘Ok, nimewasikia, sasa twende kwa utaratibu huu’. Hiyo ndiyo hoja yangu, kwamba mamlaka ya juu imesikia, sasa itoe maamuzi kwamba tunakwendaje kuanzia hapa.

“Kuna sauti nyingi zinataka Katiba Mpya, kuna sauti nyingi zinasema hapana, kuna sauti nyingine zinasema hazijafanya uamuzi, sasa nadhani mwenye mamlaka, kwa ushauri wangu, aseme hebu sasa twende kwa utaratibu huu. Na huu ndio wakati wenyewe,” alisema Dk Hoseah.

Maoni ya mwanasheria huyo mkongwe aliyewahi kuongoza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) yanakuja kukiwa na vuguvugu la vyama vya siasa na mashirika ya haki za binadamu kuishinikiza Serikali kumalizia mchakato wa kupata Katiba Mpya.

Wengi hawajui maana ya katiba
Dk Hoseah alisema anaamini kuwa watu wengi hawajui maana ya Katiba, hivyo wakati vuguvugu la kudai Katiba Mpya likiendelea, kuna umuhimu mkubwa wa wananchi kuelimishwa maana halisi ya Katika.

“Nadhani hapa ndipo pa kuanzia. Katiba ni nini? Ukiweza kulijibu hilo, mambo mengine ni rahisi kuyaelezea,” aliongeza.

Maeneo ya kufanyiwa kazi

Dk Hoseah alisema kuna maeneo ya Katiba yanayohitaji kufanyiwa kazi kwa weledi na utulivu mkubwa.

“Si maeneo yote, lakini yapo yanayohitaji kufanyiwa kazi. Kweli tumeona athari ya hizo ibara au sura ndani ya katiba. Kwa hiyo naunga mkono kuwa Katiba si perfect (timilifu). Yako maeneo ya kufanyiwa marekebisho au kuondolewa kabisa,” alisema.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa nchi kujua inataka nini, hasa katika dai la Katiba mpya ili katiba itakayoandikwa ikidhi maslahi mapana ya nchi.

“Siku zote huwa nasema hebu tujiulize sisi Watanzania tunataka nini. Tukijibu hilo swali ni rahisi kuielezea Katiba tunayotaka. Ukimuuliza kila mtu anayetaka Katiba Mpya, ukipata majibu hayatafanana.”

Alisema hivi sasa mamlaka ya juu inaweza kuunda kamati ndogo ya wataalamu wakaishauri na baadaye suala hilo likajadiliwa na wananchi wote ‘ili tufikie mwafaka.’

Katiba Mpya haimalizi matatizo

Dk Hoseah alitoa angalizo la wananchi kutobeba imani kuwa Katiba Mpya ni suluhisho la kila tatizo katika nchi.
“Si kila Katiba Mpya inatatua matatizo, lakini sisemi kwamba katiba iliyopo haina matatizo. Hili ni suala la kitaalamu na linahitaji sasa wataalamu waliobobea katika eneo hilo washauri.

“Najua kuna siasa ndani yake, najua pia kuna mambo ya kisheria lakini tujifunze kwa wenzetu walifanyaje katika mazingira kama haya. Hatuishi kisiwani, hatuishi kwenye bahari isiyokuwa na mifano ya kuigwa,” alisema Hoseah.

“Katiba nzuri ni ile ambayo itatatua matatizo ya Tanzania. Tunaweza kutaka Katiba ya Marekani au Katiba ya Japan, hizo hazitatusaidia sana. Lazima tuwe na katiba inayoangalia matatizo yetu na historia yetu.

“Watu wasisahau historia ya Taifa hili. Nchi hii ina historia nzuri tu. Tunapozungumzia Katiba tusije tukafikiria kwamba nchi hii haina historia. Tuone athari za kila tunalopendekeza,” alisema.
 
Asante Rais wa TLS, Hakika dai la Katiba Bora ni la Msingi.Hatuna sababu kusubiri machafuko.
 
Huko magaidi wamefura. 😅😅😅
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Magaidi nasikia huko nyumnani mmefura kama Dubu.

Mungu hamfichi mnafiki. Mlikuwa mnafurahi kuita wengine magaidi

tatizo lenu hua mnajionaga kama mna akili kushinda watu wote hii nchi ndo maaana mpaka leo hamjawahi kukubalika na wananchi, ccm bado ina miaka mingine 100 ya utawala mpaka ichoke yenyewe
 
Baada ya Jenerali Ulimwengu kuanza kufatiliwa sasa anaefata kwenye list ni Dr. Hosea.
Ccm haijawai kuwaacha watu wenye hoja concrete kama hawa.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom