Dkt. Hassan Abassi: Agizo la Rais Samia kufungulia vyombo vya habari linahusu televisheni za mitandaoni pekee

Sijaelewa huyu daktari ameyasema hayo kwa nafasi ipi inayompa jukwaa la kusema hayo.
Katibu mkuu wa wizara ya habari ndiye boss wa mkurugenzi wa habari. Greson Msigwa ni mkurugenzi kwenye wizara ya habari chini ya Dr Abbasi ambaye ndiye katibu mkuu wa wizara hiyo. Kuwa msemaji wa tasisi hakufanyi kuwa ndiyo mkuu wa tasisi hiyo na hakuwaondolei wakuu wa tasisi husika kuwa wasemaji wa tasisi zao. Unafanya kwa niaba yao.
 
Neno Uhuru wa Habari Dr Abbas limemchenga na hawezi kuwa MTU sahihi hapo alipo,anamharibia Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza maagizo yake apendavyo yeye!
Hivi tuapoongelea vyombo vya habari Dr anadhani ni TV pekee?Yaani Mh.Rais aanze kumfundisha Dr Abbas majukumu yake?Atoe ufafanuzi kuhusu magazeti,majarida,Radio's ama Online TV separately?
Post ya Dk. Abbas apewe Greson Msigwa - Msigwa fits the bill yuko well organised anajiamini na anajua kijieleza. Sio hawa wanao pewa kazi halafu wanasubiri maelekezo ya zaida kutoka kwa Rais nini cha kufanya - he goes "mimi sijapewa maelekezo" what a laughable comment! !
 
Dr Hassan Abbas bado haamini kama 'Ukuta wa Berlin' uliokuwa ukiwatenganisha Wajeruman umeanguka
 
Alichokisema rais ndicho hicho. Kila mtu alisikia hivyo. Kwa kuwa kwa kawaida serikali huendeshwa kwa maandishi au nyaraka na kwa sababu rais katika hotuba ile alitaja tu vi online tv vidogo vidogo vilivyokuwa vimefungiwa, Dr Abbas yuko sahihi. Kama rais aliimanisha na magazeti yaliyokuwa yamefungiwa Dr Abbas atapaswa kwanza kumuuliza Katibu Mkuu Kiongozi ili kupata uhakika. Halafu kwani ni magazeti yapi yalifungiwa? Si ni lile la Mbowe (Tanzania Daima), la Kubenea (Mwanahalisi) na lile la Tundu Lissu (jina nimelisahau) tu? Haya hata yakiruhusiwa wamiliki wake hawana uwezo tena wa kifedha kuyaendesha.
“Wizara ya Habari, nasikia kuna Vyombo vya Habari mmevifungia* sijui Viji- TV vya mikononi vile, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya Serikali, tusiwape mdomo wa kusema tunabinya Uhuru wa Vyombo vya Habari, tusifungie tu kibabe”-Rais Samia Suluhu Hassan
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abassi amesema agizo la kufungulia vyombo vya habari lililotolewa na Rais Samia Suluhu linahusu televisheni za mtandaoni pekee na siyo pamoja na magazeti.

Amesema endapo kukiwa na maagizo mengine yanayohusu magazeti, atatekeleza.

---
Huyu ni kichwa ngumu bado amelala, tunaomba mama yetu umuache huyu mtu aendelee kulala, hakufai.

Amelipuuza agizo lako...anajifanya mjuaji...anakujua sana kuliko unavyojielewa...
Kimsingi hana adabu, yeye binafsi anapata faida gani kufungia vyombo vya habari, kwa kuwa taifa linapata fedheha mbele ya jumhuia ya kimataifa, Rais ameagiza kuvifingulia vyombo vya habari, pia ameagiza makosa na adhabu ziwe wazi, sio kosa huyu analiona yule alioni adhabu haijulikani, akae afikiri vizuri!
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abassi amesema agizo la kufungulia vyombo vya habari lililotolewa na Rais Samia Suluhu linahusu televisheni za mtandaoni pekee na siyo pamoja na magazeti.

Amesema endapo kukiwa na maagizo mengine yanayohusu magazeti, atatekeleza.

---
Huyu ni kichwa ngumu bado amelala, tunaomba mama yetu umuache huyu mtu aendelee kulala, hakufai.

Amelipuuza agizo lako...anajifanya mjuaji...anakujua sana kuliko unavyojielewa...
Mama amesisitiza watumie akili. Ninachokiona hapa huyu Dkt Hassan ameshindwa kutumia akili, na badala yake anaendelea kutumia misuli.

Tumuachie mama mwenyewe ampe kadi ya njano.
 
Kajitoa ufahamu na kuja na tafsiri zake mwenyewe...

Mama ameshawaambia wasipopaelewa wamuulize...
 
Post ya Dk. Abbas apewe Greson Msigwa - Msigwa fits the bill yuko well organised anajiamini na anajua kijieleza. Sio hawa wanao pewa kazi halafu wanasubiri maelekezo ya zaida kutoka kwa Rais nini cha kufanya - he goes "mimi sijapewa maelekezo" what a laughable comment! !
Mkuu, Gerson Msigwa ndiye aliyepaswa kutoa taarifa hii kwa kuwa tayari amepewa post mojawapo aliyokuwa anaishika huyu bwana Abass (Ukurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Usemaji wa Serikali), lakini ni kama hajakubali kuiacha nafasi hiyo, ameamua kufanya majukumu ya msaidizi wake na ndio katoa boko kama hivyo. Bado hajakubali kilichotokea na kinachoendelea kutokea
 
Katibu mkuu wa wizara ya habari ndiye boss wa mkurugenzi wa habari. Greson Msigwa ni mkurugenzi kwenye wizara ya habari chini ya Dr Abbasi ambaye ndiye katibu mkuu wa wizara hiyo. Kuwa msemaji wa tasisi hakufanyi kuwa ndiyo mkuu wa tasisi hiyo na hakuwaondolei wakuu wa tasisi husika kuwa wasemaji wa tasisi zao. Unafanya kwa niaba yao.
Sawa kabisa mkuu, ila Mwenye Mamlaka ya kufungia magazeti ni Waziri wa Habari. Huyu bwana Abass kwa aliyoyasema na hata kwa jinsi ulivyoeleza kuwa ni Mkuu wa Taasisi huoni kama amepoka/amepora mamlaka ya Waziri wa Habari? Yaani yeye Katibu Mkuu ndie amejivika mamlaka ya kufungulia vyombo vilivyofungwa wakati barua zake za kufungia (wakati akiwa ni Msemaji wa Serikali) zilieleza kuwa aliyefanya hivyo ni Waziri wa habari.

Screen Shot 2021-04-07 at 6.01.53 PM.png

Screen Shot 2021-04-07 at 6.02.36 PM.png
 
Back
Top Bottom