SI KWELI Dkt. Gwajima amesema Kumusahau Polepole Ni Ngumu Maana Alikuwa Rafiki wa Kweli

SI KWELI Dkt. Gwajima amesema Kumusahau Polepole Ni Ngumu Maana Alikuwa Rafiki wa Kweli

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
1774328490391.png
 
Tunachokijua
Kumekuwepo Na Chapisho Ambalo Limechapishwa Na Ukurasa wa Facebook Wa Mjumbe Plus Likiwa Na Nukuu Ambayo Inakadiriwa Kutolewa Na Dr Dorothy Gwajima Kuhusu Yeye Kushirikiana Na Alyekuwa Balozi Wa Tanzania Nchini Cuba Polepole Ambaye Hadi Sasa Hajulikani Alipo.

Katika Chapisho La Facebook linamnukuu Dkt. Gwajima kuwa amesema "Ni mambo mengi tumefanya pamoja na Polepole na pia tulikuwa tunashirikiana kwenye mambo ya kiserikali,na kupeana ushauri wa hapa na pale , Kwahiyo itakuwa ngumu sana kuto kumkumbuka sana Polepole maana alikuwa ni rafiki wa kweli . Naomba walipompeleka wamuachie maana bado tunamuhitaji kama familia ya Taifa la Tanzania."

Je, ni upi uhalisia wa Taarifa hiyo?


Kupitia utafutaji wa Maneno muhimu unabainisha kuwa Dkt. Gwajima hajatoa kauli hiyo kwani hakuna chanzo rasmi cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo au yeye mwenyewe kuchapisha nukuu hiyo.

Aidha kupitia kusara zake za mitandao ya kijamii amekanusha taarifa hiyo na kwamba si ya kweli.

"Nataka kusema hivi, naomba tusitengenezeane habari za uongo uongo kwa malengo binafsi. Kama ni habari inayonihusu mimi, naweza kuisema mwenyewe kwenye kurasa zangu zote. Hivyo, habari hii kwenye picha hapo juu na maneno yaliyokuwa yameandikwa chini yake na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ni ya kutengeneza yaani ni ya uongo, IPUUZWE, na nitashtaki Polisi ili, walioniwekea maneno haya mdomoni watafutwe kwa mujibu wa Sheria wakajibu uongo wao.

Na katika habari ya kutungiana maneno ya uongo, SITAKUBALI....... maana uongo ni ufitini na adui wa haki na UONGO HAUJAWAHI KUWA MTAJI WA MAENDELEO."

Attachments

  • 1774299733056.jpg
    1774299733056.jpg
    65.1 KB · Views: 2
Back
Top Bottom