ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,114
- 49,840
Umri wa kuishi Mtanzania sasa ni wastani wa miaka 65.5 wakiongoza wanawake kwa kuishi miaka 69 na wanaume miaka 62. Na hii inafahamika wanawake sisi kibailojia tumezaliwa hivyo, Mungu katupendelea kidogo kwa sababu na sisi tunabeba watoto matumboni na kazi zetu sio ngumu kama za akina baba.” - Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa
===
Tumepiga hatua sana kutoka wastani wa miaka 55 hadi kufikia miaka 65 ni jambo la kupongezwa.
Ila wanaume wenzangu ukipata kazi nafuu fanya achana na kazi ngumu na za kuhatarisha maisha yako kama hakuna ulazima, hiyo ndio Siri ya kuishi miaka Mingi kama Wanawake.
Kingine karibu kuwa stress free kadiri inavyowezekana.
Ni hayo tuu.