Dkt. Chana atangaza wanaowania tuzo za muziki 2022

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
742
479
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana ametangaza Vipengele vya Wanamuziki wanaowania Tuzo za Muziki mwaka 2022.

Dkt. Chana ametangaza Vipengele hivyo jijini Dodoma ambapo amevitaja baadhi kuwa ni Mwanamuziki Bora wa Kiume, Mwanamuziki Bora wa Kike na Wimbo Bora wa Mwaka ambapo amesema Vipengele vingine vitaendelea kutangaza.

Katika Kipengele cha Mwanamuziki Bora wa kiume wanaowania ni Alli Kiba, Harmonize, Marioo, Rayvann na Dullar Makabila.

Kipengele cha Msanii Bora wa Kike wanaowania ni Nandy, Zuchu, Chemical Trixy Tonic na Waddy B.

Aidha ametaja kipengele cha Wimbo Bora wa mwaka ambapo zinazoshindanishwa ni Pita huku wa Dullah Makabila, Nakupenda wa Jay Melody, Nitaubeba wa Harmonize, Kwikwi wa Zuchu pamoja na Mwamba wa Rayvann.

Hata hivyo Mhe. Dkt. Chana ameeleza kuwa, Vipengele vya kuwania Tuzo hizo vimeongezeka kutoka 47 hadi 57,huku akibaibisha kuwa zoezi la kuwapigia kura litaanza Aprili 8, hadi 28, 2023 saa sita usiku na Tuzo zitafanyika Aprili 29, 2023 jijini Dar es Salaam.
IMG-20230406-WA0049.jpg
 
Mwanamziki bora wa kiume jay melody wangemuongeza hapo kafanya vizuri toka 2021-2023
 
at least serikali yetu imeanza kuzinduka na kuzingatia sanaa yetu. Japo wasanii bado wana safari ndefu kufikia level za wenzetu huko West na South Africa
 
Ni Bongo tu ndio waziri anaweza kutangaza kuhusu tuzo za muziki.
 
Kwa miaka ya hv karbn tuzo yeyote ya hip hop asipokuepo young lunya kindly ipuuzwe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom