Tuzo za muziki 2022 ni za umahiri sio umaarufu

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
732
475
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Tuzo za Muziki Tanzania zinatolewa kwa ajili ya wanamuziki mahiri na sio maarufu.

Mhe. Chana amesema hayo katika Usiku wa Tuzo hizo Aprili 29, 2023 zilizofanyika The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam ambapo amesema Tuzo hizo zinatolewa kwa kutambua mchango wa wanamuziki katika kukuza na kutangaza muziki wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

"Nina furaha sana kwamba mwaka huu upigaji kura umekua kwa kasi kubwa na mwaka huu kipengele cha Mwanamuziki Chipukizi kimepigiwa kura nyingi zaidi inayofanya Tuzo hizi kukua zaidi", amesema Mhe. Chana.

Awali Naibu Waziri, Mhe. Mwinjuma alisema kuwa muziki unaendelea kukua na ukuaji huo ulichagizwa zaidi na Rais wa Awamu ya Tano, Mhe. Jakaya Kikwete.

Naye Katibu Mtendaji wa BASATA alisema kuwa, tuzo hizo pia zimeshirikisha nchi za nje ikiwemo Afrika Kusini na Nigeria kwa kutambua ushirikiano wa kimuziki uliopo Afrika, huku akiongeza kuwa tuzo hizo pia zimetolewa kwa Taasisi ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika kukuza mziki.

Tuzo hizo zimetolewa katika vipengele mbalimbali ikiwemo Mwanamuziki Bora wa kike na kiume, wimbo bora wa kike na kiume, Singeli Bora ya mwaka n.kView attachment 2604756View attachment 2604757View attachment 2604759View attachment 2604761View attachment 2604758View attachment 2604760
IMG-20230430-WA0018.jpg
IMG-20230430-WA0024.jpg
IMG-20230430-WA0020.jpg
IMG-20230430-WA0021.jpg
IMG-20230430-WA0022.jpg
IMG-20230430-WA0023.jpg
 
Back
Top Bottom