Wake up.Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Sir Harold Wilson aliwahi kusema, ''A week is a long time in politics''.
Katika historia ya Tanzania, Dkt. Bashiru Ally kama inavyododoswa kwa sasa kurudi tena kuwa Katibu Mkuu wa CCM atakuwa ni mmoja wa watanzania ambao utumishi wao wa umma unaweza kidogo kulinganishwa na Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa!
Historia inaonyesha Rashid Kawawa aliwahi kushika nafasi ya juu kabisa katika serikali lakini baadaye akaja kushushwa mpaka kwenye nafasi ya waziri asiye na wizara maalum katika utawala wa Mwalimu Nyerere. Fikiria Makamu wa Rais ambaye pia ni Waziri Mkuu anajikuta amekuwa waziri tu!
Najua kuna baadhi ya watu wasiokuwa na uelewa mpana wa kile kilichokuwa kikiendelea walikuwa wakimcheka Rashid Kawawa alipokuwa anashushwa kwenye vyeo.
Watu waliokuwa wakimcheka Rashid Kawawa hawana tofauti na wale wa sasa waliomcheka na wanaendelea kumcheka Dkt. Bashiru Ally bila kujua kinachoendelea ndani ya CCM!
Kikao cha Mkutano Mkuu wa CCM kinachoenda kukutana Mwezi mwishoni mwa mwezi huu au ujao kinaenda kutoa majibu ya uhakika kuhusu sababu ya Dr. Bashiru Ally kurudishwa tena CCM kama Katibu Mkuu wa CCM Taifa!
Ninajua kuna kundi la baadhi ya wanaCCM ambao fagio la uhakiki wa mali za CCM na safisha CCM liliwakumba kwa sasa wanafanya kazi kuhakikisha Dkt. Bashiru asirudi tena CCM kama Katibu Mkuu lakini Wazee wa CCM ambao ni Makamu Mwenyekiti wa CCM wa Bara na yule wa visiwani wamekubaliana na uamuzi wa Mwenyekiti ajaye wa CCM Taifa wa kulipeleka jina la Dkt. Bashiru katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ili likathibitishwe kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa.
Kuna watu watakuja na hoja wakisema, atakuwaje Katibu Mkuu wa CCM wakati ni Mbunge na kwa nini alipewa Ubunge? Jibu la swali hili lilishatolewa kwenye uteuzi wa Dkt. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye alikuwa mbunge wa kuteuliwa kabla hajateuliwa kuwa Balozi. Dkt. Bashiru akiwa Katibu Mkuu wa CCM itabidi ajiuzulu Ubunge wake kama alivyofanya Dkt. Possi.
Kwa wasiojua, Dkt. Bashiru asingeondolewa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi na kubaki mitaani bila sehemu ya ''kumuingizia kipato'' wakati akisubiri wenye CCM kumthibitisha! Njia iliyotumika ni kumpa ''ajira'' ya muda mfupi ambayo inajulikana kisheria ili kusubiri Mkutano Mkuu wa CCM na Kikao cha NEC ya CCM.
Kuna msemo usemao, Anayelia mwanzoni, mwisho hucheka kwa furaha na anayecheka mwanzoni, mwisho hulia!
Baahiru keshamwagwa.
Yeye na Polepolr sasa hivi wanaionea power kwenye kioo