OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,185
- 103,685
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi wakati wa uzinduzi wa Royal Tour Dodoma leo amempongeza Rais Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya wakati wa utengenezwaji wa Filamu hiyo "Tumpongeze Rais wetu, nitawapa mikasa miwili"
"Kuna sehemu Rais anavua samaki ilikuwa Pemba, za ndani tu ni kwamba ilimchukua Rais kutwa nzima kurekodi tukio la kuvua samaki, tulipofika Pemba tukakuta Bahari ina mawimbi makubwa, mwingine angesema tuondoke ila Rais akasema tusubiri akatutania 'wengine sio Watu wa Pwani hamjui kuwa Bahari ikifika saa nane tisa inatulia', Rais akasubiri tangu saa 4 asubuhi hadi saa 9 kwenda saa 10 alasiri, makofi kwa Rais"
"Kingine ni siku alipokuwa anaingiza voice over kuna masimulizi yalifanyika field mengine alirekodi Ofisi kwake, Mimi ni miongoni mwa Waumini wa shughuli za Ikulu maana ukinywa juisi au kula samaki Ikulu ni juisi au samaki muhimu kuliko wote Duniani , tulijiandaa na wenzangu tukasema tume-miss Juisi na samaki wa Ikulu, kufika Ikulu Rais alirekodi voice over kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 2 usiku bila kupata chakula cha mchana zaidi ya korosho na juisi tu"
"Wengine tunarajia pilau litakuja lakini wapi Rais anapiga kazi, saa 2 usiku amemaliza kazi tukaagana hakuna lunch wala dinner, huyu Mimi ningedhani ni Kiongozi ambaye badala ya kumparura tungempetipeti kwasababu wako miongoni mwetu wangepata hiyo nafasi Rais wa Nchi unarekodi Royal Tour angeweza kuitisha pilau, ugali na nyama, chips kuku lakini Rais Samia yupo kazini ameweka pembeni masuala mengine yote"
My Take
Sioni tofauti ya KM na hawa Chawa wa mitandaoni