Dk. Willibroad Slaa amemtembelea nyumbani kwake Sheikh Abubakar Zuberi

Dk. Willibroad Slaa amemtembelea nyumbani kwake Sheikh Abubakar Zuberi

Chademakwanza

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
6,346
Reaction score
1,873
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTEUZI WA KAIMU MUFTI MKUU WA WAISLAM TANZANIA


Muda mfupi baada ya aliyekuwa mmoja wa Wajumbe wa Baraza Kuu la Ulamaa la BAKWATA Sheikh Abubakar Zuberi, kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), DK. Willibroad Slaa amemtembelea nyumbani kwake kumpongeza na kumtakia majukumu mema akimhakikishia ushirikiano kama jirani na kiongozi.

Sheikh Abubakar Zuber ambaye ametangazwa leo kukaimu nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa dini ya Kiislam kwa siku 90 hadi hapo atakapochaguliwa Mufti Mkuu kwa mujibu wa taratibu za dini hiyo, anaishi Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jirani na zilipo Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA.

Mbali ya kumtakia kila la heri, Katibu Mkuu Dk. Slaa amemuahidi Mufti Sheikh Zuberi kuwa CHADEMA iko tayari wakati wowote kutoa ushirikiano atakaouhitaji katika kutimiza wajibu wake huo.

"Shehe Zubeir, jirani yangu napenda kutumia fursa hii kukupongeza sana kwa namna ambavyo wenzako wamekupatia imani kubwa na kukuteua ili uwaongoze Waislam kiroho. Ni imani kubwa ambayo binafsi naamini utaweza kuitumikia wakati mkiendelea kusubiri taratibu zingine za uchaguzi.

"Nitumie fursa hii pia kusema tukiwa majirani zako hapa Mtaa wa Ufipa, tukiwa viongozi ambao tunao wanachama, wapenzi na wafuasi wetu wenye dini tofauti wakiwemo Waislam, naomba kukuhakikishia ushirikiano kutoka kwetu wakati wowote katika kutimiza majukumu yako haya makubwa na nyeti.

"Shehe wangu kwa muda wote tumeishi pamoja hapa tukiwa majirani… ukitimiza wajibu wako uliokuwa nao nasi tukiendelea kutimiza majukumu yetu katika jamii ya Watanzania, nakutakia kila la heri katika kuwatumikia na kuwaongoza kiroho Waislam wa Tanzania," alisema Dk. Slaa nyumbani kwa Sheikh Zuberi leo mara baada ya uteuzi wa Kaimu Mufti Mkuu wa Waislam kufanyika.

Imetolewa leo Jumatatu, Juni 22, 2015 na;
Idara ya habari na mawasiliano
CHADEMA

 
nimatumaini yetu utaibadilisha bakwata kuwa na taasisi ya kuwatumikia waislam
 

Katibu Mkuu Dk. Slaa alipokutana na Sheikh Zuberi. Hii ilikuwa ni mwaka jana wakati Katibu Mkuu akitoka kutoa kutoa pole Msikiti wa Mtambani ulioungua moto. Katikati yao ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanganyika, Prof. Abdalla Jumbe Safari.


attachment.php




 

Attachments

  • DK. SLAA MUFTI ZUBERI IMG-20140814-WA0029.jpg
    DK. SLAA MUFTI ZUBERI IMG-20140814-WA0029.jpg
    61.5 KB · Views: 11,004
In a jovial mood with Sheikh Zuberi



attachment.php





 

Attachments

  • DK. SLAA MUFTI ZUBERI IMG-20140814-WA0032.jpg
    DK. SLAA MUFTI ZUBERI IMG-20140814-WA0032.jpg
    58.4 KB · Views: 3,423

Katibu Mkuu Dk. Slaa alipokutana na Sheikh Zuberi. Hii ilikuwa ni mwaka jana wakati Katibu Mkuu akitoka kutoa kutoa pole Msikiti wa Mtambani ulioungua moto. Katikati yao ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanganyika, Prof. Abdalla Jumbe Safari.


attachment.php





Mungu abariki kazi ya mikono yako Dr Slaa mtetezi wa Wanyonge
 
Dk. Slaa in a jovial mood with Sheikh Abubakari Zuberi bin Ali listening to CHADEMA Vice Chairman (mainland) Prof. Abdalla Jumbe Safari...

attachment.php
 

Attachments

  • DK. SLAA MUFTI ZUBERI IMG-20140814-WA0033.jpg
    DK. SLAA MUFTI ZUBERI IMG-20140814-WA0033.jpg
    62.9 KB · Views: 3,707
Back
Top Bottom