Dk Stephen Ulimboka Jembe na Nguzo ya MADAKTARI Nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Stephen Ulimboka Jembe na Nguzo ya MADAKTARI Nchini

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Chief Lugina, Jan 28, 2012.

 1. C

  Chief Lugina JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 290
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]Madaktari wakiwa wameshika mikono huku waiimba nyimbo za kuashiria umoja katika mgomo wao unaoendelea jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix

  Geofrey Nyang’oro
  SAKATA la madaktari nchini linazidi kuchukua sura mpya baada ya wataalamu hao kukataa hoja za ujumbe wa Serikali ulioongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi, Hawa Ghasia huku wakigoma kusikiliza kauli yoyote kutoka kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hadji Mponda

  Wakati mawaziri hao wakikumbwa ana tafrani hiyo tayari wauguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na ile ya Mkoa wa Dodoma wametishia kusitisha utoaji huduma ifikapo Jumatatu kama masuala yao hayajapatiwa ufumbuzi.

  Vigogo wa Serikali waliofika kukutana na madaktari hao jana ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na naibu wake, Dk Lucy Nkya, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Blandina Nyoni, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa.
  Tukio hilo lilitokea jana kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Star Light, Jijini Dar es Salaam ambako madaktari hao walikusanyika na baadaye kupewa taarifa kuwa kuna ujumbe wa Serikali utafika kwa majadiliano. Madaktari hao waliwatimua ujumbe huo baada ya kuusikiliza juu ya wito wao wa kuwataka wasitishe mgomo ili wafungue ukurasa wa majadiliano, wakajibiwa kuwa kwa sasa ni wakati wa kutekeleza kwa vitendo na siyo ahadi.

  Ujumbe huo wa Serikali uliwasili ukumbini hapo majira ya mchana na kukaribishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Stephen Ulimboka ambaye baada ya kuwawekea viti pembeni mwa jukwaa kuu, aliwatambulisha kwa washiriki. “Ugeni tuliokuwa tunasubiri umefika, si rahisi sisi wote kuwafahamu ni vema wangejitambulisha wao kwa majina kisha tuendelee na utaratibu tuliojiwekea,” alisema Dk Ulimboka.

  Mara baada ya kauli hiyo, wageni hao walianza kujitambulisha. Wa kwanza alikuwa Waziri Ghasia aliyewasalimia madaktari hao na kujitambulisha kisha kueleza kuwa aliongoza ujumbe huo kuwasilisha taarifa ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Dalili mbaya kwa ujumbe huo, zilianza kujitokeza walipoitika kwa nguvu salamu ya Waziri Ghasia huku wakiwanyamazia Waziri wa Afya na maofisa waandamizi wa wizara hiyo.

  Baada ya tukio hilo kumalizika, Dk Ulimboka alitoa taratibu za mkutano kuwa ni kusoma taarifa maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kupelekwa kwa Waziri Mkuu. “Sisi hapa tutawakabidhi taarifa iliyoandaliwa na madaktari ambayo ni maalumu kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baada ya kuwasomea, tutawakabidhi kisha tusubiri majibu ya taarifa yetu tukiwa hapahapa,” alisema Dk Ulimboka.

  Dk Ulimboka alisoma taarifa hiyo mbele ya wageni hao ambayo ilitaja madai yao kadhaa ikiwemo kumtaka Waziri Ghasia kumshauri Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa katika wizara hiyo, Waziri Mponda na naibu wake Dk Nkya, Katibu Nyoni na Mganga Mkuu, Dk Mtasiwa.

  Mara baada ya kusoma taarifa hiyo alikabidhi barua hiyo kwa Waziri Ghasia huku akisisitiza kuwa wataendelea na mgomo hadi watakapopatiwa majibu ya hoja zao.

  “Tunaomba taarifa hiyo imfikie haraka Waziri Mkuu, ijadiliwe kwa haraka na kutoa majibu yatakayotupatia ufumbuzi ili nasi turudi kazini tukaokoe maisha ya Watanzania,” alisema Dk Ulimboka ambaye kwa kauli yake iliashiria kufunga mjadala.

  Baada ya kauli hiyo, Waziri Ghasia alisimama na kueleza kuwa wao walifika wakiwa na ujumbe toka kwa Waziri Mkuu hivyo ni vema wangekubaliwa wauwasilishe ambapo alimtaja Waziri wa Afya Dk Mponda kuwa angeusoma.
  Dk Ulimboka alijibu hoja hiyo akisema “Madaktari hatuna tatizo na ujumbe toka kwa waziri Mkuu Mizengo Pinda ila ujumbe kutolewa na Waziri wa Afya Dk Hadji Mponda hatukubali kwasababu hatuna imani naye labda kama kweli ni taarifa, ungesoma wewe,” alisema Dk Ulimboka na kukaa chini.

  Waziri Ghasia alikubaliana na hoja hiyo na katika kuwasilisha taarifa hiyo, alisema alisononeshwa kusoma majibu yanayohusu madai ya madaktari hao kwa niaba ya waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Afya wakati yeye (Dk Mponda) akiwepo.

  Ghasia alisema wizara imetafakari kwa kina suala la madaktari waliokuwa kwenye mafunzo katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili na kuwarudisha kwenye kituo hicho cha kazi huku ikiahadi kuwalipa stahili zao.
  “Wazira imetafakari kwa kina na imeamua kuwarejesha madaktari wote waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili na wanatakiwa kuripoti katika vituo hivyo vya kazi kuanzia Jumatatu,” alisema Ghasia.

  Kuhusu madai mengine, alisema Serikali itaendelea na majadiliano ya pamoja huku akiwaomba warejee kazini.
  “Sisi tuwaombe tu kwamba madai yenu yote Serikali inayafanyia kazi. Suala la nyumba tayari tumeshapata fedha kutoka Global Fund kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za madaktari ili waweze kukaa karibu na vituo vyao vya kazi,” alisema Ghasia. Akijibu ombi la kuwataka warejee kazini, Dk Ulimboka alisema hilo litategemea majibu ya taarifa walioiwasilisha kwa Waziri Mkuu, ambapo alisisitiza kuwa wao wataendelea na mikutano katika ukumbi huo.

  “Sisi tutaendelea na mikutano kujadili taarifa yenu na pia tungeshauri taarifa hii mtuletee kwa maandishi, lakini pia tunasubiri majibu ya taarifa yetu tuliyoiwasilisha kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambayo tumeitoa kwa maandishi,” alisema Dk Ulimboka. Dk Uliomboa aliwataka wawakilishi hao wa Serikali kutambua kuwa ujumbe haukuwa wa kushawishiana kurudi kazini bali ni wa kupeana taarifa.

  Kauli hiyo iliashiria kwamba hoja ya ujumbe huo haina uzito wa kuwashawishi kuacha mgomo huku wakikataa hoja zao sasa kujadiliwa na wizara badala yake walisisitiza Waziri Mkuu kushughulikia suala hilo. Walimtaka Waziri Mkuu, kutoa majibu ya madai yao kwa wakati ili asiwafanye kufikia hatua ya kusitisha huduma katika vitengo vya dhararu.

  “Mgomo huu unaendelea nchi nzima hadi majibu ya madai yetu tuliyowasilisha kwa Waziri Mkuu yamepatiwa majibu.
  Tunashauri kazi hiyo ifanywe haraka vinginevyo tusije tukashawishika kusitisha huduma kwenye vitengo vya dharura,” alisema Ulimboka.

  Tishio la mgomo zaidi
  Wakati huo huo, Chama cha Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kimesema kuwa wauguzi wataendelea kutoa huduma kwa kusuasua hadi Jumatatu na kama suala hilo litakuwa halijapatiwa ufumbuzi, watasitisha huduma na kufunga hospitali.

  “Sisi tutaendelea kutoa huduma katika mazingira ya shida hivi mpaka Jumatatu tu,” alisema Mwenyekiti wa chama hicho, Paul Magesa.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  He was instrumental kwenye mgomo wa mwaka 2000 sina uhakika na mwaka vizuri, lakini Alijenga hoja vizuri, this is a noble profession....endeleeni na mgomo ila emergency cases zone muwepo kuziattend,
   
 3. k

  kiche JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wajiandae kutimuliwa kutoka kwenye hiyo mikutano yao!!it better for them to initiate the second plan before the action,huu ukimya wa serikali unatia shaka,yasije yakatokea kama yale ya mkesha wa arusha
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  serikali kila siku kuwadanganya watu kuwa madaktari na waalimu wanapangiwa kwenda mahala fulani mikoani wakafanye kazi wanakataa kwenda but in actual fact serikali inachokifanya ni siasa tu. wanakupagia kituo huku wakijua wazi ukifika pale una sehemu ya kuishi na wanategemea wewe na familia yako mukaishi chini ya mwembe.
   
 5. P

  Pamoja-Daima New Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukimya siyo tatizo, ishu ni madaktari kuwa wamoja, that's what is important
   
 6. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,599
  Likes Received: 2,455
  Trophy Points: 280
  @ Dr haji mponda; najaribu kuvaa viatu vyako na kwa kweli nahisi vinapwaya. Hawa doctors ulikuwa na nafasi ya kushughulikia madai yao katika hatua za mwanzo kabisa, sijui nn kimekuingia ukawbip na sasa wamepiga. Kazi mnayo na niwaombe doctors msiache kuokoa maisha ya ndugu zetu ktk emergenge unit vinginevyo goma na ikibidi tuandamane mpaka kieleweke. Mungu wabariki wazalendo wa tz.
   
 7. P

  Pax JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wasiwasi wangu ni kama madaktari wanaweza kuhold on the pressure a little bit longer, I can sniff divisions among them. Sina uhakika kama serikali inaweza kujicommit katika kutimiza madai yao japo ni ya msingi, the timing could not be any worse. This being the case, I can predict the situation to be out of control after the meeting with PM, of which the government will have left with only one option, kuwafukuza. Hapa ndio nawashauri wawe makini in their next move maana baada ya PM there is no one else left who can talk to them, wasipolitambua hili wajue wanafanya kosa. Baada ya kesho kutakuwa na mgawanyiko mkubwa kati yao, wengine watataka kuendeleza mgomo wengine wameshachoka sasa kukaa kijuweni.

  Doctors need to play their next card very cautiously, serikali imerun out of option, to throw the PM in the game is an obvious sign. I would say he is the last player they can afford to play. Sasa madaktari hapa lazima wawe makini kidogo, PM atakuja na ahadi na sidhani kama ataweza kufanya kosa la kufanya maamuzi ya papokwa papo. Nawashauri madaktari waipe serikali muda, kama miezi 4-6 hivi kufanyia kazi hoja zao. Less than that mgomo utakosa mvuto.
   
 8. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  katika kichwa chako cha habari ni ujinga kumuita mtu jembe wakati hatiwi mpini
   
 9. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,915
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Tujiulize hawa madaktari ni nani anawalipia fedha za kukodi kumbi za mikutano kila siku??
   
 10. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kuwafukuza sio rahisi kiasi hicho sheria ya kazi hairuhusu watu walio kwenye mgomo wafukuzwe kazi, kuna taratibu zake. Halafu serikali ktk kucheza karata zake inabidi iwe imepima km kuwafukuza ndio kutatua tatizo waliwaondoa interns matokeo yake yamekuwa mabaya.
   
 11. A

  August JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  aliye kupa ujumbe huu ni PM, Ghasia, Mponda, NKya, "Asha Ngedere" au wote kwa pamoja?
   
 12. P

  Pax JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Naongea kwa experience, sheria za kazi pia hairuhusu migomo kama suala lako limeshafika kwa wahusika na umeshaambiwa suala lako serikali inalishughulikia, kumbuka PM ndio serikali nyenyewe. Ukiwa na madai lazima utoe muda wa mdaiwa kuyafanyia kazi. Miaka ya 90 kama sijakosea Zakhia Meghji akiwa waziri wa afya walifukuzwa, kwa hiyo sio jambo geni hilo. Serikali pia ikishakosa namna the only option ni nguvu, sheria zinasahaulika kwanza kwa kipindi hicho. Yetu macho!
   
 13. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakuona dk stephen ukiwa na sifa ya kuvaa gwanda za chadema...ningependa kukuona ukijiunga na wapiganaji,,,bila shaka mwaka 2015 unakuwa waziri wa afya
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  nimepokea taarifa toka ofis ya waziri mkuu kuwa kesho atakutana na madaktairi hao...........
   
 15. m

  mwanakazi Member

  #15
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Madaktari watakutana j3..yote haya yalishajadiliwa kwenye meeting ya leo. Unless itoke taarifa kutoka kwenye kamati waliounda. Yetu macho..................
   
 16. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  acha kutisha madokta..wewe kama kunguru baki na uwoga wako uendelee kudhulumiwa haki zako za msingi mpaka yesu arudi
  madaktari mpaka kieleweke,msiwasikilize watu kama hawa
   
 17. P

  Pax JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mpaka sasa madaktari wameshapata attention ya serikali, kinachofuata wakae wazungumze na kustrike a deal. Zaidi ya hapo ni kulewa sifa na kiburi mkiamini kuwa serikali itavumilia pasipo na mwisho. Nakuambia hivi baada ya PM kama hamtarudi kazini mtafukuzwa, dont ever undermine the strength of the so called government even at its weakest state.
   
 18. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  wakati mwingine kurudi nyuma kwenye mapigano ni mbiinu ianayotumiwa na wanajeshi . hii haimaanishi kwamba umeshindwa hapana ni kwenda kujipanga vizuri. Nashauri pia Madakitari wasisite kutumia mbinu hii kama wataona inafaa ili kutoharibu umoja wao.... kumbuka sio wote wenye nguvu sawa za uvumilivu... hiyo kuridi nyuma na kuwatia moyo ni jambo la muhimu katika mapambano... kumbukeni umoja ni nguvu utengano ni dhaifu.
   
 19. P

  Pax JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wengi hawaelewi hizi strategy mkuu, hawajui kuwa miongoni mwao kuna ambao wameshachoka. Mimi nakuambia wasipoelewana na PM ndio mwisho wao, kila mtu atajiokoa kwa namna yake, watasambaratika kila upande.
   
 20. only83

  only83 JF-Expert Member

  #20
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  ...Akiongea na Channel Ten,Mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari..Dr Ulimboka,ameongea kutoka mafichoni na kusema kuwa mgomo uko pale pale na utakuwa unashika kasi kwa mfumo tofauti tofauti..alipoulizwa kwanini hataki kujitokeza hadharani amesema amepata taarifa kuwa anatafutwa na usalama.Na amewaimiza madaktari kuendelea kugoma mpaka serikali itakapokuja kusikiliza madai yao.

  source:Channel Ten.
   
Loading...