Dk. Slaa: UCHAGUZI WIZI MTUPU

Dk. Slaa: UCHAGUZI WIZI MTUPU

Nyerere ndio aliwafundisha CCM uhuni huu mwaka 1995, kuanzia uchaguzi wa zanzibar hadi ule wa Dsm kufutwa. Hakika utakatifu wake utakuwa na kasoro - Vatican nawaamini; chunguzeni kwa makini.
 
Sasa nini kifanyike wadau?
Tusiishie kulalamika tu kwani tunazidi kupata vidonda vya tumbo.
Tufanye nini?

YES, TUFANYE NINI? Maana kama kawaida yetu, tunalalamika tu, mwisho tunasema "waache tu, mwisho utafika".. alah, sasa huo mwisho unataka nani akuletee? Nani ambaye ni Mtanzania zaidi yako ambae anahaki ya kuanzisha? Au ni nani unataka kumtanguliza, ili likiharbika umrushie shutuma wewe ile hali yeye akiunyea? Mfano hata ile migomo ya vyuo vikuu, wanaofukuzwaga ni walioanzisha, lakini kwa aibu wengine hurejea kwa business as usual! Nani hurudi nyuma aghalabu kuulzia mwenzetu anapata mstakabali gani kwa kujitoa kwa ajili yetu? Au NDO TUNACHOCHEA KARAMA ZA WATU, WAKISHAVUNA TUNAJIFANYA TULIKUA NA KARAMA IZO SOTE? ONENI SASA MNAMSUBIRI SLAA ASEME.... KWANI NI YEYE NDO KAIBIWA KURA AU SISI SOTE? Mpaka utakapofika wakati kila mtu aone kadhulumiwa yeye na si mwenzake.. then we will be talking, then we will be acting... THEN THAT IS WHAT WE CALL A REVOLUTION!
 
tumechoka kusubiri maamuzi ya chadema.Dr. slaa please come out and say something!

tuvute subira kaka.nadhani ni busara apate vielelezo vyote vya msingi kabla ya kusema lolote.asipokua na vielelezo vyote watamuita mzushi.ninaimani ataibuka na concrete evidence.cha msingi tumuombee kwa Mola ili amuongeze na ampe evidence za kutosha plus utashi wa kuifafanulia dunia yaliojiri katika uchaguzi
 
Kiwete anataka tu madaraka kwa wizi , kwa uchawi ,kwa kuuwa ,kwa kutangaza sera za kidini na yooote machafu mbele ya macho yetu tukiona hivi hivi. Ajiulize basi baada ya hiyo miaka mitano atakuwa wapi .Tanzania ? au atajiua kishenzi kama BALALI huko kwa washakji zake Boys Two Men?

Kama yeye alivyo wa kulipza kisasi watanzania tutalipiza kisasi kwake yeye na familia yake iliyofanya ushenzi huu. The day will come when he will live the poorest life at Bagamoyo. Tusibiri.
 
Mambo yaliyofanywa ni aibu kwa taifa, kwa sababu ya chama kimoja 2.Sauli alikataliwa na Mungu ndipo Daudi akachaguliwa, na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, napenda kuwatia moyo wana Jf tusimame katika maombi na kuhakikisha haki inatendeka kwa vitendo.Sisiemu mtandao wao ni mkubwa hivyo bila nguvu ya Mungu iliyoambatana na nguvu ya umma hatutaweza kufika.
 
tumechoka kusubiri maamuzi ya chadema.Dr. slaa please come out and say something!

Ngoja afanye tathmini ya kutosha, yeye sio mruka ruka kama JK. Anatuliza boli anatazama, anachungulia halafu anapiga goliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Haraka hamna haja sasa maana baada ya NEC kumtangaza JK, hakuna cha mahakama wala nin kinachoweza kufanya mabadiliko. Ila ni sisi raia kuweka rekodi safi na maazimio ya mbele kwa mbele
 
Did you find this post helpful? |
icon1.gif
Re: Dk. Slaa: UCHAGUZI WIZI MTUPU

CCM wamejirudisha madarakani wakishirikiana na NEC!!

mi naunga hoja hapa
 
south africa walipata uhuru kwa kutumia harakati nyingi sana - lakini wananchi wa kawaida/wanafunzi - kwa kuimba
WADAU MNAONAJE - tuanze kwa KUWAZOMEA - kila wakipitia????? nawasilisha hoja.
 
Matokeo ya Uchaguzi mkuu yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yalijaa utata, Mwanahalisi limegundua.

Taarifa kutoka ndani ya NEC, vyama vya siasa na baadhi ya wagombea, zinasema matokeo yaliyotolewa yanatofautianma na kura halisi zilizopigwa.

Kwa mujibu wa baadhi ya mawakala wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), matokeo mikononi mwao yanatofautiana sana na yale yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

Matokeo mikononi mwa mawakala kutoka mikoa 18 ya Tanzania Bara na mitatu ya Zanzibar, hadi juzi jumatatu yanathibitisha kuwepo kwa tofauti kati ya idadi ya vituoni na ile iliyotangazwa na NEC.

Katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro matokeo yaliyotangazwa na NEC yanaonyesha kuwa CCMimepata kura za Urais 35,910 huku Chadema ikionyeshwa kupata kura 18,513. Lakini matokeo ambayo yamekusanywa na mawakala wa Chadema yanaonyesha CCM imepata kura 20,120 huku Chadema ikipata kura 26,724.

Katika jimbo la Karatu Mkoani Arusha, hesabu za NEC zinaonyesha CCM imepata kura za urais 24,382 huku Chadema ikipata kura 41 tu angalau kwa mujibu wa matangazo ya Televisheni. Bali kwa mujibu wa matokeo yaliyokusanywa na mawakala ambayo yamesainiwa na mawakala wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo CCM imepata kura 24,364 na Chadema ilipata kura 43,137

Jimbo jingine ambalo matokeo yake yamejaa utata ni Geita, mkoani Mwanza. Matokeo yaliyotangazwa na NEC katika jimbo hilo yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 17,792 na Chadema imeambulia 3,989. Lakini Matokeo mikononi mwa mawakala yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 30,960 na Chadema kura 15,736. NEC ilikiri kuwapo kwa kasoro katika jimbo la Geita na ilikubali kufanyia Marekebisho.

Katika jimbo la Ubungo Mkoani Dar es salaam matokeo ya NEC yameipa CCM kura 68,727 na Chadema kura 65,450. Hata hivyo kwa mujibu wa matokeo mikononi mwa mawakala yanaonyesha kuwa Chadema imepata kura 72,252 na CCM kura 70,472.

Uchunguzi wa Mwanahalisi umebaini kuwa licha ya tofauti ya matokeo ya vituoni na yale ya NEC, matokeo katika baadhi ya maeneo hayakurekodiwa kwenye karatasi za tume, rasmi kwa shughuli hiyo. Gazeti limeona matokeo yaliyorekodiwa kwenye karatasi za kawaida na magamba magumu ya makasha, ingawa zimegongwa mhuri inayoonekana kuwa ni ya Tume. Matokeo ya aina hii yanashurutisha kuwepo ujenzi wa shaka juu ya usalama wa kura na uwezekano wa matokeo kughushiwa

Mwanahalisi limeelezwa kuwa mbali na kasoro hiyo ya kutokuwapo kwa fomu za kurekodia matokeo, katika baadhi ya majimbo yaliyofanya uchaguzi, majumuisho ya kura za urais hayakufanyika.

Gazeti hili lilitaka kujua maoni ya Dk. Slaa juu ya taarifa kuwa kuna maeneo ambako majumuisho ya kura za urais hayakufanyika naye alijibu " wewe unazungumza hilo; matatizo yaliyopo katika uchaguzi huu ni mkubwa sana. Kuna Uchafu mwingi. Ndio maana sisi tunasisitiza kuwa hatuwezi kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa" Anasema " Tunaendelea kukusanya nyaraka zote za uchaguzi na si muda mrefu ujao, tutaeleza dunia ni kitugani kilifanyika, wapi na akina nani walihusika. Tutaeleza pia hatua gani itafuata baada ya hapa"

Gazeti hili lina taarifa kuwa baadhi ya majimbo ambako matokeo ya Urais hayakutangazwa ni Kiteto, Segerea, Muheza, Kibakwe, Kinondoni, Ilala na Moshi Vijijini.

Kutoka Morogoro taarifa zinaeleza utata wa aina yake. Kati ya wapiga kura 422 waliotarajiwa kupiga kura katika kituo cha shule ya msingi Msufini, kata ya Msufini Manispaa ya Morogoro HAKUNA HATA MMOJA ALIYEKUWA NA SHAHADA YA KUPIGIA KURA

NUNUA MWANAHALISI LA LEO TAREHE 10/11/2011 UONE JINZI CCM WALIVYO NA TAALUMA YA MWAKA 47 YA KUIBA

jamani tuendelee kumuombea DK.Slaa na Chama chetu maana tulio jeruiwa ni sisi wenyewe,
 
Hivi tuna tume ya uchaguzi au tume ya UCHAFUZI?
 
NEC wameondoa huduma ya kujua 'registration status' kupitia website yao ili watu wasiendelee kuona madudu. NEC pia hawakuvitoboa vitambulisho vilivyorudishwa na wale waliobadilisha maeneo yao kama inavyofanyika sehemu kama benki, ni kwa nini?
 
Pamoja na kwamba hatutachoka kuelimisha umma lakini naunga mkono hoja ya KUWAZOME. maana kama ni wababe na wanajua hatuwezi kuwafanya kitu. dawa ni kuwazomea mpaka waote kutu
 
muonamambo,
Asante sana kwa comment yako. Najua wengi wangelipenda tutoe Tamko haraka haraka. Mambo magumu hayahitaji ushabiki, wala haraka haraka. Tukumbuke haraka haraka haina baraka. Niseme tu uwizi wa kura mwaka huu ni wa kutisha sana. Hivyo tunajiandaa kikamilifu, ili tutakapotoka kusiwe na shaka lolote. Kuna mambo mawili, tunaweza kutoa Tamko la kisiasa na hatimaye Tamko lenye Data. Lakini pia ujue kuwa Tamko la namna hiyo inatolewa siyo na Dr. Slaa, bali na vyombo vya maamuzi ya Chama,kwani katika siasa hakuna jambo muhimu kama kushirikishana. Naomba subiri, si muda mrefu Tamko litatoka. Ninalotaka kuwahakikishia watanzania ni kuwa hatuwezi kuwaangusha kamwe, na wala hatuwezi kuwauza.
Tunawaahidi Watanzania kuwa Wabunge takriban 45 wa Chadema wataendeleza jitihada za kumkomboa Mtanzania. Ajenda ya Wabunge wetu licha ya kushughulikia majimbo yao, lakini Wabunge wa Chadema watakuwa katika ujumla wao Wabunge wa Taifa, na watakuwa wakishughulikia kupitia Bunge maswala ya kitaifa ili hatimaye tufikie lengo letu la kumkomboa Mtanzania, wote wanaohitaji ukombozi yaani wakukulima, wafugaji, wafanyibiashara(wasio mafisadi) kwa lugha ya kawaida Walalahoi. Ninachoomba kwa wote wenye nia njema, tuendelee kushikamana, kushirikiana kwani vita vya ukombozi si vya mtu mmoja wala siyo vya kundi la watu au chama fulani tu, bali wote wenye nia na malengo yanayofanana. Najua tuko wengi wenye nia ya aina hii. Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana Wana JF kwa ushirikiano, ushauri, mawazo japo wakati mwingine yamekuwa very critical yametusaidia sana kujielekeza(focused) na kulenga "real issues". Nawashukuru sana wale wote walioniombea muda wote mkono wangu ulipokuwa umevunjika. Nashukuru mkono unaendelea vizuri, na hata sasa kwa mara ya kwanza leo ninafanya "blind typing" kwa mikono yote miwili. Namshukuru sana Mungu. Mungu awabariki nyote na Mungu ibariki Tanzania.

tumechoka kusubiri maamuzi ya chadema.Dr. slaa please come out and say something!
 
matokeo ya uchaguzi mkuu yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi (nec) yalijaa utata, mwanahalisi limegundua.
taarifa kutoka ndani ya nec, vyama vya siasa na baadhi ya wagombea, zinasema matokeo yaliyotolewa yanatofautianma na kura halisi zilizopigwa.

kwa mujibu wa baadhi ya mawakala wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), matokeo mikononi mwao yanatofautiana sana na yale yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi (nec)

matokeo mikononi mwa mawakala kutoka mikoa 18 ya tanzania bara na mitatu ya zanzibar, hadi juzi jumatatu yanathibitisha kuwepo kwa tofauti kati ya idadi ya vituoni na ile iliyotangazwa na nec.

katika jimbo la hai, mkoani kilimanjaro matokeo yaliyotangazwa na nec yanaonyesha kuwa ccmimepata kura za urais 35,910 huku chadema ikionyeshwa kupata kura 18,513. Lakini matokeo ambayo yamekusanywa na mawakala wa chadema yanaonyesha ccm imepata kura 20,120 huku chadema ikipata kura 26,724.

nunua mwanahalisi la leo tarehe 10/11/2011 uone jinzi ccm walivyo na taaluma ya mwaka 47 ya kuiba

nani asiemjua mhariri wa gazeti hili ni mchochezi na kibaraka mkubwa! Ndio maana alimwagiwa tindikali na vibaka wa jiji!!!!
 
muonamambo,
Asante sana kwa comment yako. Najua wengi wangelipenda tutoe Tamko haraka haraka. Mambo magumu hayahitaji ushabiki, wala haraka haraka. Tukumbuke haraka haraka haina baraka. Niseme tu uwizi wa kura mwaka huu ni wa kutisha sana. Hivyo tunajiandaa kikamilifu, ili tutakapotoka kusiwe na shaka lolote. Kuna mambo mawili, tunaweza kutoa Tamko la kisiasa na hatimaye Tamko lenye Data. Lakini pia ujue kuwa Tamko la namna hiyo inatolewa siyo na Dr. Slaa, bali na vyombo vya maamuzi ya Chama,kwani katika siasa hakuna jambo muhimu kama kushirikishana. Naomba subiri, si muda mrefu Tamko litatoka. Ninalotaka kuwahakikishia watanzania ni kuwa hatuwezi kuwaangusha kamwe, na wala hatuwezi kuwauza.
Tunawaahidi Watanzania kuwa Wabunge takriban 45 wa Chadema wataendeleza jitihada za kumkomboa Mtanzania. Ajenda ya Wabunge wetu licha ya kushughulikia majimbo yao, lakini Wabunge wa Chadema watakuwa katika ujumla wao Wabunge wa Taifa, na watakuwa wakishughulikia kupitia Bunge maswala ya kitaifa ili hatimaye tufikie lengo letu la kumkomboa Mtanzania, wote wanaohitaji ukombozi yaani wakukulima, wafugaji, wafanyibiashara(wasio mafisadi) kwa lugha ya kawaida Walalahoi. Ninachoomba kwa wote wenye nia njema, tuendelee kushikamana, kushirikiana kwani vita vya ukombozi si vya mtu mmoja wala siyo vya kundi la watu au chama fulani tu, bali wote wenye nia na malengo yanayofanana. Najua tuko wengi wenye nia ya aina hii. Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana Wana JF kwa ushirikiano, ushauri, mawazo japo wakati mwingine yamekuwa very critical yametusaidia sana kujielekeza(focused) na kulenga "real issues". Nawashukuru sana wale wote walioniombea muda wote mkono wangu ulipokuwa umevunjika. Nashukuru mkono unaendelea vizuri, na hata sasa kwa mara ya kwanza leo ninafanya "blind typing" kwa mikono yote miwili. Namshukuru sana Mungu. Mungu awabariki nyote na Mungu ibariki Tanzania.
Doctor asante sana maana hata hilo ulilolisema ni neno pia. Tumekuelewa na tunasubiri tamko rasmi,CHADEMA inafahamika kuwa haikurupuki kwenye masuala ya msingi.
 
Back
Top Bottom