Dk. Slaa: UCHAGUZI WIZI MTUPU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa: UCHAGUZI WIZI MTUPU

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzito Kabwela, Nov 10, 2010.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Matokeo ya Uchaguzi mkuu yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yalijaa utata, Mwanahalisi limegundua.

  Taarifa kutoka ndani ya NEC, vyama vya siasa na baadhi ya wagombea, zinasema matokeo yaliyotolewa yanatofautianma na kura halisi zilizopigwa.

  Kwa mujibu wa baadhi ya mawakala wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), matokeo mikononi mwao yanatofautiana sana na yale yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

  Matokeo mikononi mwa mawakala kutoka mikoa 18 ya Tanzania Bara na mitatu ya Zanzibar, hadi juzi jumatatu yanathibitisha kuwepo kwa tofauti kati ya idadi ya vituoni na ile iliyotangazwa na NEC.

  Katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro matokeo yaliyotangazwa na NEC yanaonyesha kuwa CCMimepata kura za Urais 35,910 huku Chadema ikionyeshwa kupata kura 18,513. Lakini matokeo ambayo yamekusanywa na mawakala wa Chadema yanaonyesha CCM imepata kura 20,120 huku Chadema ikipata kura 26,724.

  Katika jimbo la Karatu Mkoani Arusha, hesabu za NEC zinaonyesha CCM imepata kura za urais 24,382 huku Chadema ikipata kura 41 tu angalau kwa mujibu wa matangazo ya Televisheni. Bali kwa mujibu wa matokeo yaliyokusanywa na mawakala ambayo yamesainiwa na mawakala wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo CCM imepata kura 24,364 na Chadema ilipata kura 43,137

  Jimbo jingine ambalo matokeo yake yamejaa utata ni Geita, mkoani Mwanza. Matokeo yaliyotangazwa na NEC katika jimbo hilo yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 17,792 na Chadema imeambulia 3,989. Lakini Matokeo mikononi mwa mawakala yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 30,960 na Chadema kura 15,736. NEC ilikiri kuwapo kwa kasoro katika jimbo la Geita na ilikubali kufanyia Marekebisho.

  Katika jimbo la Ubungo Mkoani Dar es salaam matokeo ya NEC yameipa CCM kura 68,727 na Chadema kura 65,450. Hata hivyo kwa mujibu wa matokeo mikononi mwa mawakala yanaonyesha kuwa Chadema imepata kura 72,252 na CCM kura 70,472.


  Uchunguzi wa Mwanahalisi umebaini kuwa licha ya tofauti ya matokeo ya vituoni na yale ya NEC, matokeo katika baadhi ya maeneo hayakurekodiwa kwenye karatasi za tume, rasmi kwa shughuli hiyo. Gazeti limeona matokeo yaliyorekodiwa kwenye karatasi za kawaida na magamba magumu ya makasha, ingawa zimegongwa mhuri inayoonekana kuwa ni ya Tume. Matokeo ya aina hii yanashurutisha kuwepo ujenzi wa shaka juu ya usalama wa kura na uwezekano wa matokeo kughushiwa

  Mwanahalisi limeelezwa kuwa mbali na kasoro hiyo ya kutokuwapo kwa fomu za kurekodia matokeo, katika baadhi ya majimbo yaliyofanya uchaguzi, majumuisho ya kura za urais hayakufanyika.

  Gazeti hili lilitaka kujua maoni ya Dk. Slaa juu ya taarifa kuwa kuna maeneo ambako majumuisho ya kura za urais hayakufanyika naye alijibu " wewe unazungumza hilo; matatizo yaliyopo katika uchaguzi huu ni mkubwa sana. Kuna Uchafu mwingi. Ndio maana sisi tunasisitiza kuwa hatuwezi kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa" Anasema " Tunaendelea kukusanya nyaraka zote za uchaguzi na si muda mrefu ujao, tutaeleza dunia ni kitugani kilifanyika, wapi na akina nani walihusika. Tutaeleza pia hatua gani itafuata baada ya hapa"

  Gazeti hili lina taarifa kuwa baadhi ya majimbo ambako matokeo ya Urais hayakutangazwa ni Kiteto, Segerea, Muheza, Kibakwe, Kinondoni, Ilala na Moshi Vijijini.

  Kutoka Morogoro taarifa zinaeleza utata wa aina yake. Kati ya wapiga kura 422 waliotarajiwa kupiga kura katika kituo cha shule ya msingi Msufini, kata ya Msufini Manispaa ya Morogoro HAKUNA HATA MMOJA ALIYEKUWA NA SHAHADA YA KUPIGIA KURA

  NUNUA MWANAHALISI LA LEO TAREHE 10/11/2011 UONE JINZI CCM WALIVYO NA TAALUMA YA MWAKA 47 YA KUIBA
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  HALAFU ETI CCM WANATHUBUTU KUSEMA WAMESHINDA KWA KISHINDO!!!!!!!!!! NI AIBU KUBWA SANA HII....MIMI NASEMA IPO SIKU!!!!!!! ATAWAMALIZA HAWA MAFISADI WA CCM ......IPO SIKU NA INAKUJA UPESI......MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI....MAANA SIKU....ATAKAPOAMUA KUIDAI KWA NGUVU......WATU KAMA HAWA MAFISADI WATATAFUTA MVUNGU WA KUJIFICHA....ole wao ccm Siku inakuja! yaja upesi...Watu wanamuona Dr Slaa kwamba Mzushi lakini hawajui kuwa CCM imechakachua kwa kiwano cha kutisha....
   
 3. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  kaka nchi hii hata tembo anawezatambulishwa simba na ikasimamiwa hivyo. aibu tupu !!
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  CCM wamejirudisha madarakani wakishirikiana na NEC!!
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi CCM wataacha lini kuchakachua? Mimi nazani mwaka 2015 Wadau tufanye kama watu wa Nyamagana na Ilemela. Hakuna kura itakayoibwa
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mambo mbofu mbofu
   
 7. m

  mbombongafu Member

  #7
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NEC na CCM yao ni DOG kabisa hawa hawafai kutuongoza nchi hii
   
 8. monge

  monge Member

  #8
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 10, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi nilijua Kikwete hakushinda ,hata kama angeshinda siyo kama tulivyotangaziwa, yaani sisiemu wanataka kututania kiasi hiki wanadhani
  tutaendelea kukubali upuuzi wa namna hii!!!!;
  Watanzania tuamke tuache mzaha nchi inaagamia kwa sababu ya upole watu na kusema ndiyo katika kila japo pasipo kuuliza kwa nini!!!!!!!!!!!?
   
 9. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  nimeamini " kweli sikio la binadamu haliwezi kuzidi kichwa"
  labda yuchukue la tembo
   
 10. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Walikuwa wamezoea kumnyonga Maalim seif huko zanzibar.Safari hii wamekwaa kisiki cha mpingo, hadi kieleweke, wamezoea vya kunyonga.Sasa hivi wanagombania cheo cha Spika ni hulka yao wamezoea kula vilivyopakwa DAMU YA MWANADAMU .Nyerere aliwahi kusema" ukila nyama ya mtu utaendelea kula nyama ya mtu maisha yako yote" wametenda dhambi ya ubaguzi dhambi hiyo itaendelea kuwatafuna mpaka iwamalize, Wamembagua Dr.slaa na chama chake, leo wanaanza kumbagua Sitta wakitoka kwa Sitta hawabaki salama hao mapambafuuuu
   
 11. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Blue to them is Red
   
 12. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #12
  Nov 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Wizi wa kura kura umekuwa dhahiri, ila nasikitika tumekuwa mno very slow kukusanya ushahidi na kurespond....
   
 13. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  CCM mnajisikiaje jamani ndio maana akina Kibaki na Mugabe waliudhuria kushuhudia jinsi technologia ya wizi wa kura ilivyokomaa.
   
 14. Ally Msangi

  Ally Msangi Verified User

  #14
  Nov 10, 2010
  Joined: Jun 29, 2010
  Messages: 577
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kikwete alijua hali ni ngumu, si alisema watashinda kwa asilimia zaidi ya walizopata awamu ya kwanza... sasa kikowapi? wamezidiwa mpaka wakajitahidi kuiba ili wapate japo hizo 61% ambazo si sahihi kwakuwa zimefanyiwa ubadhilifu na NEC, ki msingi hapo hakuna uchaguzi huru
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Sasa nini kifanyike wadau?
  Tusiishie kulalamika tu kwani tunazidi kupata vidonda vya tumbo.
  Tufanye nini?
   
 16. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  tumechoka kusubiri maamuzi ya chadema.Dr. slaa please come out and say something!
   
 17. F

  Fishyfish JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM is Tanzania's greatest enemy.
   
 18. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Biharamulo JK hakufikisha hata kura 5000, na bukombe hardly JK alikuwa na kura 3000 tu, hizo wilaya hali ilikuwa tete kwa CCM na JK, nguvu ya ziada kubwa sana imetumika kumpa kura JK, yaani hakubaliki kabisa mpaka kesho
  nadhani Tanzania tunashida/tatizo la waandishi wa habari za kichunguzi, zaidi ni za udaku tu, lakini kama kungekuwa na waandishi wa aina hiyo kama Kubenea na MWanahalisi kwa ujumla wake, uchafu mwingi wa uchaguzi ungepatikana,
   
 19. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  sema dk usiogope sema! Sisi watanzania hatuogopi mafashisti.
   
 20. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa wizi huu wa kutisha CCM ijiandae kuondoka madarakani kwa aibu kabla ya 2015,haiwezekani kuongozwa na wezi na siku si nyingi nchi hii italipuka.Watanzania hawawezi kukubali kuendelea kuongozwa na mtandao wa wezi.JK nusuru nchi kwa kutafuta suluhu na Mshindi halali(Slaa) acha ubabe kwani wanaokulinda wamekuchoka.
   
Loading...