Dk. Slaa: Tukishinda elimu itakuwa bure

Dk. Slaa: Tukishinda elimu itakuwa bure

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

slaa-pix1.jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Willibrod Slaa


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Willibrod Slaa (pichani), amesema chama hicho kimejiwekea ajenda nne na kuwa ifikapo 2015 kikishika dola, kazi yao ni kutoa elimu bure na bora kwa watanzania.

Hata hivyo, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeichakachua sera hiyo ya Chadema iliyowekwa katika Ilani yake ya uchaguzi wa mwaka 2010 na kusema elimu ya bure inawezekana, ingawa hadi leo chama tawala kimeshindwa kutekeleza ahadi hiyo.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Iringa.
Alisema ajenda ya pili ya Chadema katika uchaguzi mkuu uliopita ambayo pia wataitekeleza ni vifaa vya ujenzi kushushwa bei ili kila Mtanzania awe na uwezo wa kujenga nyumba ya saruji na bati.

Alisema kuwa wazee wote, wafugaji, wakulima, mama lishe na makundi mengine watapewa pensheni kwa sababu wote wamechangia uchumi wa nchi na kwamba haiwezekani kuona wazee wanakufa hivihivi wakati wamechangia.

Ajenda ya nne alisema ni huduma bora za maji na afya ambazo ni jukumu la serikali na siyo la mtu mmoja mmoja, lakini serikali ya CCM imewatupia wananchi badala ya kuhakikisha wanapata huduma hiyo.

Hata hivyo, alimkosoa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwamba anazunguka nchi nzima na kuwadanganya vijana kuwa atawapatia ajira, lakini hazungumzii kuimarisha na kujengwa viwanda.

"Kinana alisema kuwa atawapa vijana bodaboda, lakini Chadema kinasema msigawe bodaboda, tengenezeni viwanda hapa nchini ili vijana wapate ajira na ziuzwe kwa bei ya chini, lakini siyo wagawe bodaboda ambazo zitawafanya wawe vilema na kusababisha nguvu kazi ya nchi kushuka," alisema.

Kuhusu katiba inayopendekezwa, Dk. Slaa alisema vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitazunguka nchi nzima mtaa kwa mtaa na kijiji kwa kijiji katiba hiyo itakapopelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura na kuwataka wananchi waikatae.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari, alisema maendeleo ya Tanzania yamedumazwa na serikali kuingia katika mikataba mibovu ambayo haijali maslahi ya wananchi na kwamba umaskini wa wananchi umetokana na CCM huku akitolea mfano kwa sekta ya madini kuingiza mapato madogo.

SOURCE: NIPASHE
 
Heeee! Ni CHADEMA tena si UKAWA? Makubwa haya
 
Heeee! Ni CHADEMA tena si UKAWA? Makubwa haya
...hivi huyu Lizaboni vipi,nilikuwa nadhani huyu bwana anaweza kuwa msaada!.Kuwa na kondoo kama hawa ni hatari kwa ustawi wa ardhi hii.
 
unajua wewe kweli huna akili hata kidogo na hujui kupambanua mambo umeambiwa kuwa wakati wa kushirikiana pamoja utasainiwa na baada ya hapo ndio utaona hata wanazunguka pamoja kwa sasa kila chama bado kinaendelea kunadi sera zake na kuwaelimisha wananchi kuhusu katiba ya maharamia maccm, na uchaguzi wa srikali za mitaa kwani vipi huelewi
 
Ahsante Sana Dr Slaa, Mungu asimamie hii ahadi itimie vijana wetu wapate elimu bure
 
Sera ya Elimu ni kipaumbele namba moja katika kuinua uchumi wa Taifa.CCM watoke hadharani watuambie jinsi wanavyoweza kutekeleza sera ya Elimu bure.Hawawezi maana leo hadi waalimu wanakatwa mishahara kwa nguvu kujenga maabara huku mafisadi wakitafuna nchi
 
Elimu bure inawezekana kabisa!! Hongera DR. wa ukweli. Kazi inabakia kwetu watanzania 2015 kuchagua usanii ama ukweli.
 
Mkuu, hakika mnachekesha sana. Mnajifanya mpo pamoja ilhali kila mtu anawaza jambo lake. Kichekesho kweli!

Naona kichwa chako kimeshafomatiwa hujielewi! Ni lini umeskia kuwa CUF,NCCR NA CDM zimefutika umebaki UKAWA? Kwa sasa vyama vyote vipo field na vitashirikiana kisiasa ktk nyanja zote kwa kuweka mgombea anayekubalika katika eneo husika.jitambue!
 
Heeee! Ni CHADEMA tena si UKAWA? Makubwa haya
kiukweli hata mimi sina imani na kadima hata kidogo. tangia wawaite wapinzani wenzao ccm B na kukataa hata kuunda nao serikali wakati kabla yao CUF walikubali kuunda serikali nao hata akina slaa na Zitto wakapata popularity walizonazo kupitia kwao walinitoka kabisa moyoni.
bila kusahau fukuza fukuza kila anayehoji kama yalivyowakuta akina juliana, Zitto, Mwigamba, machange kafulila na wengineo wengi.
wajitathimini sana hawa jamaa? hawaaminiki. maana kwa kauli kama hizo wenye akili zinatutatiza sana.
 
Sera ya Elimu ni kipaumbele namba moja katika kuinua uchumi wa Taifa.CCM watoke hadharani watuambie jinsi wanavyoweza kutekeleza sera ya Elimu bure.Hawawezi maana leo hadi waalimu wanakatwa mishahara kwa nguvu kujenga maabara huku mafisadi wakitafuna nchi

Nimeshangazwa sana hii kauli yako, kumbe ndio wale wale wa mambo ya kibubusa. Katiba pendekezi imeisha sema elimu ni bure, soma katiba bora pendekezi.
 
Only fools argue by fighting na matusi.. Mtu badala ya kujibu na kutoa hoja anaanza "shoga" ushoga umetoka wapi jukwaani.. Hahaha! people are becoming more violent daily.. Turudi kwenye mada

Mi Slaa naona kaongea jambo la maana tu na la ukweli, swala ni implementation! Plans za kuimplement hiyo kitu nazo tunahitaji tuzisikie.. Na kuongelea elimu bure bila kugusia teachers duh! maana bongo tuna teachers wako ovyo kusema ukweli hilo kila aliyepita shuleni analijua, na system ya elimu mbovu pia..
 
Sera ya Elimu ni kipaumbele namba moja katika kuinua uchumi wa Taifa.CCM watoke hadharani watuambie jinsi wanavyoweza kutekeleza sera ya Elimu bure.Hawawezi maana leo hadi waalimu wanakatwa mishahara kwa nguvu kujenga maabara huku mafisadi wakitafuna nchi
Sijakupata vizuri mkuu, eti CCM watoka hadharani wafanye nn? Watu wako busy na biashara tena watoke nje waje waharibu mambo! Ama kweli kutaka kumwambia mtu wa CCM kusema asicho kiamini na kutenda asichokisema ni sawa na kumtongoza mama mkwe mchana kweupe bila chembe ya pombe kicwani.
 
Back
Top Bottom