Dk. Slaa: Tukishinda elimu itakuwa bure

Dk. Slaa: Tukishinda elimu itakuwa bure

slaa-pix1.jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Willibrod Slaa

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Willibrod Slaa (pichani), amesema chama hicho kimejiwekea ajenda nne na kuwa ifikapo 2015 kikishika dola, kazi yao ni kutoa elimu bure na bora kwa watanzania.

Hata hivyo, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeichakachua sera hiyo ya Chadema iliyowekwa katika Ilani yake ya uchaguzi wa mwaka 2010 na kusema elimu ya bure inawezekana, ingawa hadi leo chama tawala kimeshindwa kutekeleza ahadi hiyo.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Iringa.
Alisema ajenda ya pili ya Chadema katika uchaguzi mkuu uliopita ambayo pia wataitekeleza ni vifaa vya ujenzi kushushwa bei ili kila Mtanzania awe na uwezo wa kujenga nyumba ya saruji na bati.

Alisema kuwa wazee wote, wafugaji, wakulima, mama lishe na makundi mengine watapewa pensheni kwa sababu wote wamechangia uchumi wa nchi na kwamba haiwezekani kuona wazee wanakufa hivihivi wakati wamechangia.

Ajenda ya nne alisema ni huduma bora za maji na afya ambazo ni jukumu la serikali na siyo la mtu mmoja mmoja, lakini serikali ya CCM imewatupia wananchi badala ya kuhakikisha wanapata huduma hiyo.

Hata hivyo, alimkosoa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwamba anazunguka nchi nzima na kuwadanganya vijana kuwa atawapatia ajira, lakini hazungumzii kuimarisha na kujengwa viwanda.

“Kinana alisema kuwa atawapa vijana bodaboda, lakini Chadema kinasema msigawe bodaboda, tengenezeni viwanda hapa nchini ili vijana wapate ajira na ziuzwe kwa bei ya chini, lakini siyo wagawe bodaboda ambazo zitawafanya wawe vilema na kusababisha nguvu kazi ya nchi kushuka,” alisema.

Kuhusu katiba inayopendekezwa, Dk. Slaa alisema vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitazunguka nchi nzima mtaa kwa mtaa na kijiji kwa kijiji katiba hiyo itakapopelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura na kuwataka wananchi waikatae.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari, alisema maendeleo ya Tanzania yamedumazwa na serikali kuingia katika mikataba mibovu ambayo haijali maslahi ya wananchi na kwamba umaskini wa wananchi umetokana na CCM huku akitolea mfano kwa sekta ya madini kuingiza mapato madogo.

SOURCE: NIPASHE

Aanze kwanza (Slaa) kumwambia yule ndugu ya Stivini Wasira Mwenye Shule ya kulipia hapa Dar ambaye ni Mtu mwenye Cheo CHADEMA na mwaka uliopita alialikwa (Slaa) kwenda kwenye mahafali na badala yake alienda
Kitila Mfwatamkumbo, hiyo Shule hakuna mtoto wa uswazi hata mmoja kwa kuwa bei yake haishikiki, na mmiliki ni mwana CHADEMA, hivyo Slaa anaweza kuanzia hapo sio lazima asubiri akiingia Madarakani!

Vinginevyo tunadanganyana tu!
 
Ujinga ni mzigo na wewe ni mzigo! Dr Slaa anaonglea public schools if you want to send you child to private school is up to you! Public school ziiwa bora hamna mtu ataenda private! Nchi za wanjanja public school ndo bora na siyo private!
 
Wewe ndio unaonyesha ujinga kama unataka Usawa ktk nchi Masikini kama yetu ni kuhakikisha Elimu inatolewa kwa wote kama ilivyokuwa hapo kale na sio kuruhusu wenye uwezo wa kulipa wasome vizuri na wasio na uwezo wabaki nyuma hakuna kitu kama hicho, kama kweli anataka kupigania masikini basi aidha afute shule Binafsi ama aseme kwamba hata mtoto wa Masikini pia anaweza kusoma huko kwenye Binafsi kwa serikali kulipia hiyo gharama vinginevyo ni kiini macho tu!
 
Hongera sana raisi wetu mtarajiwa sera ya kuwapa wanachi elimu ya bure ni sera ya CHADEMA pekee ccm tunawapuuzia kama walivyo wapuuzi
 
Mkuu, hakika mnachekesha sana. Mnajifanya mpo pamoja ilhali kila mtu anawaza jambo lake. Kichekesho kweli!

Unadhani ni robots wa lumumba hao wanakaririshwa cha kusema hata kama hakina manufaa kwa taifa.
 
Hawa ukawa hawana nia ya kuunganisha nguvu. Ndio maana hata sera zao ni za kuunga unga.
Siwaelewi hawa CHADEMA kuwa ni wajamaa au mabepari.
Kama ni wajamaa watatekeleza vipi sera za ujamaa na kujitegemea;Na kama ni mabepari watatekeleza vipi sera za kibepari katika nchi yenye rasilimali za pamoja tulizopewa na Mungu?

Nawashauri CHADEMA wakutane na UKAWA ili watengeneze sera za pamoja ili wanapokuja kwetu tusione kama wanatuchanganya.
CHADEMA au CUF peke yake hawawezi kamwe kuingia madarakani leo na hata kiama.
 
Kuota ruksa... Kalale uendelee kuota sasa
 
Watanzania tumeuziwa maneno weee, yametuchoshaaaaaa. Tunataka vitendo. Sio kubwabwaja tuuuu.
 
kiukweli hata mimi sina imani na kadima hata kidogo. tangia wawaite wapinzani wenzao ccm B na kukataa hata kuunda nao serikali wakati kabla yao CUF walikubali kuunda serikali nao hata akina slaa na Zitto wakapata popularity walizonazo kupitia kwao walinitoka kabisa moyoni.
bila kusahau fukuza fukuza kila anayehoji kama yalivyowakuta akina juliana, Zitto, Mwigamba, machange kafulila na wengineo wengi.
wajitathimini sana hawa jamaa? hawaaminiki. maana kwa kauli kama hizo wenye akili zinatutatiza sana.

Toka lini nuru na giza vikawa na shirika? Endelea kutumika hapo Lumumba
 
Si alisema atahalalisha upikaji wa gongo, mbona anaanza kuweweseka tena
 
Nimeshangazwa sana hii kauli yako, kumbe ndio wale wale wa mambo ya kibubusa. Katiba pendekezi imeisha sema elimu ni bure, soma katiba bora pendekezi.

Katiba inayosema elimu ya msingi ni haki lakini haki hiyo huwezi kuidai mahakamani.Soma ibara 20(1) (2) (3)

Katiba inayosema elimu ya sekondari na elimu ya juu ni fursa?
 
Ujinga ni mzigo na wewe ni mzigo! Dr Slaa anaonglea public schools if you want to send you child to private school is up to you! Public school zikiwa bora hamna mtu ataenda private! Nchi za wanjanja public school ndo bora na siyo private!

Aanze kwanza (Slaa) kumwambia yule ndugu ya Stivini Wasira Mwenye Shule ya kulipia hapa Dar ambaye ni Mtu mwenye Cheo CHADEMA na mwaka uliopita alialikwa (Slaa) kwenda kwenye mahafali na badala yake alienda
Kitila Mfwatamkumbo, hiyo Shule hakuna mtoto wa uswazi hata mmoja kwa kuwa bei yake haishikiki, na mmiliki ni mwana CHADEMA, hivyo Slaa anaweza kuanzia hapo sio lazima asubiri akiingia Madarakani!

CCM baada ya kuona maji yamefika shingoni, inawakumbatia matajiri kama akina John Cheyo na wenye private schools kama akina mama Lwakatare ili kukabiliana na CHADEMA.

Katika watu ambao hawatataka CHADEMA ishike dola ni watu sampuli ya Mch. Lwakatare. Ni vyema tukaanza kuwaorodhesha maadui zetu. Adui yetu sio CCM pekee - anyone siding with CCM ni adui yetu!
 
Back
Top Bottom