Elections 2010 Dk Slaa, NEC wamshukia Tendwa!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,037
22,728
Dk Slaa, NEC wamshukia Tendwa
Boniface Meena, Rombo na Salim Said Dar - Mwananchi

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imemshukia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, ikibainisha kuwa msajili huyo amevuka mipaka kutokana na kitendo chake cha kutetea baadhi ya wagombea kufanya kampeni hadi nje ya muda uliopangwa kisheria wa saa 12 jioni.

Juzi Tendwa alitetea hatua ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, kufanya kampeni hadi hadi saa 1:00 usiku badala ya saa 12:00 jioni ulioidhinishwa na Nec.

Nec imeeleza hayo jana ikiwa ni siku moja tu baada ya Tendwa kueleza kuwa kuanzia sasa wamekubaliana kuwa mwisho wa mikutano ya kampeni ni saa moja usiku badala ya saa 12 jioni.

Akitoa tathimini ya mzunguko wa kwanza wa kampeni mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Slaam jana, Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame alisema Tendwa amevuka mipaka kwa sababu ameingilia majukumu yasiyokuwa ya kwake.

"Msajili wa Vyama amevuka mipaka kwa kutetea baadhi ya wagombea kupiga kampeni hadi saa 1:00 usiku jambo ambalo ni kinyume cha sheria," alisema Jaji Makame.

Jaji Makame aliongeza kuwa: "Kazi ya kupanga ratiba ya mikutano ya kampeni na uchaguzi ni ya Nec na sio ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa."


Jaji Makame alikemea vikali ukiukwaji wa kanuni na taratibu zilizowekwa na Nec kuhusu mikutano ya kampeni na kwamba, Tume haitosita kuchukua hatua kali zaidi kama ambavyo zimeainishwa katika maadili ya uchaguzi.

"Hatua hizo ni pamoja na kusimamisha kampeni za chama au mgombea atakayeendelea kukiuka sheria na maadili ya uchaguzi," alisema Jaji Makame.

Wakati Tendwa akisema muda wa kampeni umeongezwa hadi saa 1:00 kuanzia sasa kutokana na sababu za kijiographia, Jaji Makame huku akinukuu kanuni za sheria na maadili ya vyama vya siasa alisema muda wa kampeni uliokubaliwa kisheria, ni kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

"Tume inapenda kusisitiza kwamba ni muhimu kwa vyama na wagombea wao, kuendesha kampeni kwa njia ya busara na kuheshimiana," alisema Jaji Makame na kuongeza:

"Kampeni za uchaguzi zifanyike katika muda unaoruhusiwa kisheria ambao ni kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni."

Tofauti na Tendwa ambaye kisheria hana mamlaka ya kuratibu mikutano ya kampeni, Jaji Makame alisema hakuna mabadiliko yoyote ya muda wa mikutano ya kampeni yaliyofanywa na kwamba vyama na wagombea waheshimu muda na ratiba iliyopangwa na Nec na sio msajili.

Akitoa tathmini ya awamu ya mzunguko wa kwanza wa kampeni hizo, Jaji Makame alisema kiujumla kampeni zimekuwa zikienda vizuri katika maeneo mengi nchini.

Hata hivyo, alisema ofisi yake imebaini mapungufu nane ambayo yameonekana waziwazi katika mzunguko huo wa awali katika kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.

Aliyataja mapungufu hayo kuwa ni pamoja na baadhi ya wafuasi wa vyama kuingilia mikutano ya kampeni ya vyama vingine na kusababisha fujo, baadhi ya vyama na wagombea kufanya mikutano ya kampeni nje ya muda unaoruhusiwa na baadhi ya wagombea kutumia lugha za kejeli na matusi kushambulia wagombea wengine.

"Jazba kwa wafuasi wa baadhi ya vyama na kuchana bendera na mabango ya wagombea wengine, baadhi ya wagombea kutumia lugha za kienyeji (kikabila) badala ya Kiswahili na wafuasi wa baadhi ya vyama kuwabuguzi waandishi wa habari na kulazimisha kuvaa sare za vyama vyao," alisema Jaji Makame.

Alisema mapungufu mingine ni pamoja na baadhi ya vyama kutumia mabango yasiyoidhinishwa na Tume na baadhi ya vyombo vya habari kushindwa kutoa taarifa sahihi na zisizoegemea upande wowote na hivyo kukiuka maadili ya habari kuhusu usawa wa kuripoti.

Alisema kufuatia mapungufu hayo, Tume kupitia wasimamizi wake wa uchaguzi na makao makuu imeweza kushugulikia malalamiko na rufaa kadhaa zilizofikishwa ofisini kwao.

Alisema vitendo hivyo vikiachiwa kuendelea vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu wa nchi, huku akivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanaimarisha ulinzi sehemu za mikutano.

Alisema kampeni sheria imeruhusu kampeni za nyumba kwa nyumba, lakini mambo ya kitanda kwa kitanda, kichwa kwa kichwa ni tafsiri za wanasiasa tu.

Wakati hayo yakiendelea Chadema, kimemshukia Tendwa kwa kusema kuwa hakina imani naye tena kwa kuwa ameonyesha kuisaidia CCM baada ya kuongeza muda wa kampeni kinyume cha sheria.

Akihutubia wananchi wa Tarakea katika Jimbo la Rombo mgombea urais wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alisema kuwa Tendwa ameamua kufanya hivyo baada ya mgombea wa CCM, Kikwete kufanya kampeni zaidi ya muda uliopangwa kinyume na maadili waliyokubaliana.

"Kikwete amekuwa akihutubia zaidi ya muda uliopangwa wa saa 12 kamili, kwa mfano alipokuwa Arusha, Babati na Mbulu amehutubia zaidi ya muda huo na hakuna hatua alizochukuliwa na ndiyo maana Tendwa ameamua kufanya hivyo,"alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alitaka Tendwa ajiuzulu baada ya kauli ya NEC kusema kuwa haitambui alichokifanya na kama hatajiuzulu Rais Kikwete amfukuze kazi kwa kuwa anaweza kuleta vurugu katika Uchaguzi Mkuu.

Dk Slaa alisema kuwa wanasheria wa Chadema wanalishughulikia suala hilo kwa kuwa Tendwa haaminiki.

"Mimi siogopi kufa, niko tayari kupigwa risasi kwa kutetea Watanzania masikini na Tendwa ajue wananchi wamechoka na mizengwe wanayofanya kumlinda Kikwete ambaye amevunja sheria tangu alipoanza kampeni kwa kutoa ahadi lukuki kitu ambacho sheria inakataza,"alisema.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa aliwataka wakazi wa Jimbo la Rombo kutokumchagua Basil Mramba kuwa mbunge kwa kuwa ni mtuhumiwa na jimbo hilo halina sababu ya kuongozwa na mtuhumiwa ambaye ana kesi mahakamani.

"Mramba apumzike kwa kuwa anahitaji kupunguza aibu aliyoipata, kwani asipofanya hivyo aibu hiyo itaongezeka. Ninaishangaa CCM kumpitisha mtuhumiwa kitu ambacho ni cha kuwazalilisha wananchi wa Rombo,"alisema Dk Slaa.

Hata hivyo, Tendwa alipotafutwa na gazeti hili kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo hakuwa tayari kusema chochote kutokana na kile alichosema ana uchovu mkubwa.
"Nemechoka sana, ndio kwanza nimemaliza safari ndefu ya kutoka Arusha kuja Mwanza, kwa hiyo unaonaje kama tukizungumza kesho," alisema Tendwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema kuwa chama chake kilisoma alama za nyakati kilipoamua kumteua Dk Slaa kugombea urais na ndiyo maana CCM imechanganyikiwa.

Alisema Chadema iliamua kufanya hivyo baada ya kusoma alama hizo kwa kuwa Dk Slaa anauzika kutokana na kazi nzuri aliyoifanya bungeni kwa muda wa miaka 15 iliyopita.

Mbowe alisema chama kilifanya siri uteuzi wa Dk Slaa kwa kuwa CCM walijua yeye ndiye atakayegombea hivyo walijua njia ya kuwamaliza ni kuwapa Dk Slaa wapambane naye.

Mbowe alisema kuwa Slaa anawachanganya CCM na ndiyo maana mgombdea wa CCM, Kikwete hivi sasa anahaha kuhutubia hadi usiku na kuvunja sheria ya uchaguzi ambayo aliisaini mwenyewe.

"Kikwete roho yake itamtoka kutokana na sheria ya uchaguzi aliyoisaini mwenyewe, nadhani hakuisoma sheria hiyo vizuri na sasa hivi anayaona maumivu yake,"alisema Mbowe.

Alisema kuwa hivi sasa maji yako shingoni kwa Kikwete na ndiyo maana huwa anafanya mikutano mijini na kuacha wananchi wa vijijini kutokana na kutokujua afanye nini Dk Slaa asimdondoshe.

Akizungumzia kuhusu nafasi yake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Hai dhidi ya mgombea wa CCM, Fuya Kimbita, Mbowe alisema kuwa Kimbita akimshinda katika kinyang'anyiro hicho ataachana na siasa moja kwa moja.

"Fuya akinishinda naachana na siasa, amekuwa akifanya mikutano usiku na mchana wakati mimi sijafanya hata mmoja mpaka alipofika Dk Slaa ndiyo nikazunguka naye," alisema Mbowe.


Hivi Tendwa anajua hata mipaka ya utendaji wa Ofisi yake ?
 
Tunataka tuone NEC inamwadhibuje Kikwete. Maana ukivunja sheria inabidi upewe adhabu iliyoainishwa na sheria hiyo. Sheria ni msumeno.
 
NILISEMA jana
Tendwa ukimuangalia usoni kwake na namna anavyoongea napata taswira ya mgonjwa mwenye taahira aliyepewa jukumu la kuwatibu madaktari.

NAdhani kunahitaji public outcry AJIUZULU. hata kama mwanaye ni msaidizi wa rais hiyo hatujali kama analipa fadhila ama la. lakini he raped democracy.
 
Huyu ndiye mlitegemea angetoa maamuzi sahihi kuhusu pingamizi la chadema dhidi ya JK????
 
Huyu ndiye mlitegemea angetoa maamuzi sahihi kuhusu pingamizi la chadema dhidi ya JK????


  • Kikwete alipowatukana wafanyakazi, Tendwa alimtetea akidai huo ulikuwa ni utani tu.
  • Kiwete alipotembeza rushwa kwa wapiga kura, Tendwa alimtetea akidai anatekeleza ilani ya CCM.
  • Sasa Kiwete kavunja sheria ya uchaguzi, Tendwa anaingilia madaraka yasiyo yake katika kujaribu kumlinda.
  • Tendwa, Tendwa, Tendwa - huu ujeuri wako wa kutetea mambo haya ya kijinga na ya hovyo hovyo unautoa wapi ?
 
mgonjwa mwenye taahira aliyepewa jukumu la kuwatibu madaktari.

Msanii, hii imetulia!
 
  • Kikwete alipowatukana wafanyakazi, Tendwa alimtetea akidai huo ulikuwa ni utani tu.
  • Kiwete alipotembeza rushwa kwa wapiga kura, Tendwa alimtetea akidai anatekeleza ilani ya CCM.
  • Sasa Kiwete kavunja sheria ya uchaguzi, Tendwa anaingilia madaraka yasiyo yake katika kujaribu kumlinda.
  • Tendwa, Tendwa, Tendwa - huu ujeuri wako wa kutetea mambo haya ya kijinga na ya hovyo hovyo unautoa wapi ?

Hivi job description ya Msajili imebadilika? Mbona ayule wa zamani alikuwa hasikiki kabisa zaidi ya kusajili vyama!
 
Tendwa alikwisha 'tendwa' na CCM. Hapo adhabu ni lazima, otherwise sina imani na NEC! Utawala wa serikali ya CCM si wa sheria hata kidogo na hii imedhihirishwa na kutokujali sheria hata wakati wa kampeni. CHADEMA wametupa jukumu la kutoa adhabu kama wamiliki wa nchi hii hapo 31 Oktoba 2010. Na hii yote inatokana na Urais kuwa suala la kifamilia!!!!!!! Je, Tanzania ni ya familia ya JK? Kama ndiyo, je tumerudi kwenye utawala wa ki-monarchy?
 
Tendwa sasa ni kama Kivuitu wa Kenya....bravo Makame..
 
  • Kikwete alipowatukana wafanyakazi, Tendwa alimtetea akidai huo ulikuwa ni utani tu.
  • Kiwete alipotembeza rushwa kwa wapiga kura, Tendwa alimtetea akidai anatekeleza ilani ya CCM.
  • Sasa Kiwete kavunja sheria ya uchaguzi, Tendwa anaingilia madaraka yasiyo yake katika kujaribu kumlinda.
  • Tendwa, Tendwa, Tendwa - huu ujeuri wako wa kutetea mambo haya ya kijinga na ya hovyo hovyo unautoa wapi ?



  • Kikwete alipowatukana wafanyakazi, Tendwa alimtetea akidai huo ulikuwa ni utani tu.


Tendwa must GOOOOOOOO


  • Kiwete alipotembeza rushwa kwa wapiga kura, Tendwa alimtetea akidai anatekeleza ilani ya CCM.


Tendwa must GOOOOOOOO


  • Sasa Kiwete kavunja sheria ya uchaguzi, Tendwa anaingilia madaraka yasiyo yake katika kujaribu kumlinda.


Tendwa must GOOOOOOOO


  • Tendwa, Tendwa, Tendwa - huu ujeuri wako wa kutetea mambo haya ya kijinga na ya hovyo hovyo unautoa wapi ?


Tendwa must GOOOOOOOO

Tendwa yeye anataka kujifanya anaijua sheria na yuko juu ya sheria naona sasa yeye hapishani na Makamba kuropoka ropoka nadhani kuna jinamizi linawakumba hawa watu.

Tendwa sasa kama huwezi kumudu hicho kiti step down mapema iwezekanavyoooo hujui majukumu yako. umeudanganya umma sana huko arusha ulienda waambia watu na kuutangazia wananchii nawe TAKUKURU ikuchunguze, kwani huwezi kupungukiwa akili mpaka ukaropoke na kuvunja kanunu na taratibu za uchaguzi unaonyesha nini kwa jamii yako na viongozi wajo katika nafasi yako??

Viongozi wa kama wewe ndio mwatuvurugia uchaguzi kwa sababu hasimamii sheria na taratibu zote za uchaguzi
 
endelezeni porojo kwenye hii web lakini hakuna loooooooooooooote TENDWA na NEC ni baba mmoja mama mmoja wapo hapa kwa CCM tu kama kuna mtu anajipa tamaa kama atashinda basi anajifurahisha tu CCM chini ya uongozi wa Lewis Makame itashinda tena kwa tsunami
 





Tendwa must GOOOOOOOO




Tendwa must GOOOOOOOO




Tendwa must GOOOOOOOO




Tendwa must GOOOOOOOO

Tendwa yeye anataka kujifanya anaijua sheria na yuko juu ya sheria naona sasa yeye hapishani na Makamba kuropoka ropoka nadhani kuna jinamizi linawakumba hawa watu.
Sheikh alishasema atampa jk ulinzi wa majini,na majini yenyewe si ndo yanajidhihirisha kitendwatendwa!!!!
 
Huyu Tendwa ana lake jambo anajifanya hajui kuwa afya ya JK haitabiriki? Anasababisha CCM wam-over work JK and you people know kwamba Muungwana nguvu yake kiafya ni ndogo. Tendwa, Tendwa sheria na kanuni za mchezo hazibadilishwi wakati mchezo unaendelea.
 
Nyie mwacheni ahutubie usiku yaje kumpata yaliyompata mbeya. Si alishazuiwa kutembea usiku!!!!! AU "walinzi" aliopewa na daktari wake mkuu (Sheikh Yahaya) ndo yanamtia kiburi????
 
1. Naomba kujua ni adhabu gani inastahili kwa mgombea yeyote kupitiliza muda (time) wa kumaliza kampeni.

2. Jaji Makame fuata sheria inasemaje kwa matendo sio useme tu mdomoni bila kutekeleza
 
Nyie mwacheni ahutubie usiku yaje kumpata yaliyompata mbeya. Si alishazuiwa kutembea usiku!!!!! AU "walinzi" aliopewa na daktari wake mkuu (Sheikh Yahaya) ndo yanamtia kiburi????

Haya mwana nijuze hayo ya mbeya kulikuwa na nini. Asee kukaa kijiji mbaya! sina nijualo ati. Nimegee hiyo mkuu.
 
Mambo ya double standards kama kawaida yatachukua mkondo wake hapa..'kunya anye kuku, akinya bata kaharisha'-msemo wa kiswahili.
 
NILISEMA jana
Tendwa ukimuangalia usoni kwake na namna anavyoongea napata taswira ya mgonjwa mwenye taahira aliyepewa jukumu la kuwatibu madaktari.

NAdhani kunahitaji public outcry AJIUZULU. hata kama mwanaye ni msaidizi wa rais hiyo hatujali kama analipa fadhila ama la. lakini he raped democracy.

Mzee Msanii wewe ni mkali, hiyo statement imenitoa jasho!
 
KUNa kutofautiana kauli baina ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu muda wa kampeni kwa siku.

Wakati Msajili, John Tendwa, akitangaza juzi kwamba kuna makubaliano baina yake na ofisi ya NEC juu ya kuongeza muda wa kumaliza kampeni kwa siku, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajab Kiravu, jana alisema kuwa hakuna makubaliano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Tendwa alisema kuna malalamiko kuhusu baadhi ya wagombea kupitiliza muda wa kampeni ambao ni saa 12 jioni na hivyo kuomba uongezwe hadi saa moja usiku.

Kutokana na maombi hayo, Tendwa alisema, aliwasiliana na NEC na kukubaliana kuongeza muda huo hadi saa moja usiku, kwa kuwa baadhi ya maeneo yapo mbali.

Hata hivyo, Kiravu jana alikanusha makubaliano hayo na kusema Msajili amevuka mipaka kulitolea kauli suala hilo.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kutoa tathmini ya Tume katika kipindi cha mwezi mmoja tangu kuanza kampeni, Kiravu alisema Msajili hakutakiwa kutoa maelezo hayo bali jukumu hilo ni la Tume.

Alisema kwa mujibu wa kanuni na sheria, mgombea anatakiwa kufanya kampeni kati ya saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni.

Alipotembelea ofisi za vyama vya siasa na kuzungumza na viongozi wa vyama hivyo, Arusha juzi, Tendwa alikaririwa akisema wamekubaliana na NEC kuwa kuanzia sasa mwisho wa kampeni ni saa moja usiku na nyongeza hiyo ya muda imetokana na sababu za kijiografia.

Katika kutetea hoja yake, alitolea mfano wa Mkoa wa Kigoma na Wilaya ya Ngara, Kagera, ambapo jua huchelewa kuzama hivyo saa 12 jioni inakuwa bado ni mapema sana.

Sambamba na hilo, NEC ilitangaza mikakati ya kulinda kura wakati wa uchaguzi ikiwamo kuweka namba kwenye masanduku ya kura kulingana na majimbo.

Mkakati mwingine ni kuchapisha karatasi za kura Uingereza, ambapo Kampuni ya Kalamazoo ndiyo iliyoshinda zabuni hiyo baada ya Tume kutangaza zabuni ya kimataifa.

Kiravu alisema kama kuna watu wametengeneza masanduku ya kura watakuwa wamejisumbua, kwani hayatatumiwa; na ya Tume yatakuwa na namba maalumu kulingana na jimbo husika.

Kiravu alikuwa akijibu tetesi kuwa kuna masanduku ya kura yametengenezwa na kuhifadhiwa katika maeneo ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambapo alisema: “Sisi hatuna taarifa na hayo hayatuhusu, isipokuwa yatakayotumika ni ya kwetu tu”.

Kuhusu karatasi zenye picha na majina ya wagombea, alisema majina yataandikwa kwa kufuata alfabeti na yataanza na chama chenye herufi ya A na kuendelea, mpango ambao umewekwa kuwarahisishia wasioona.

Wagombea urais ni Peter Mziray (APPT-Maendeleo); Jakaya Kikwete (CCM); Dk. Willibrod Slaa (Chadema); Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi); Mutamwega Mugahywa (TLP) na Fahmi Dovutwa (UPDP).

Katika udhibiti huo wa kura, alisema matokeo yatajumlishwa kisayansi majimboni na ya urais yatabandikwa kila yatakapohesabiwa na pia kutakuwa na kituo cha matokeo, ambapo yatajumlishwa kwa uwazi na waandishi wa habari kuruhusiwa kushuhudia.

Akijibu malalamiko ya vyama vya siasa ya kutoona majina yaliyo kwenye Daftari la Wapiga Kura, Kiravu alisema sheria inaitaka Tume kuwasilisha Daftari kwenye vituo siku nane kabla ya uchaguzi, lakini mwisho wa mwezi huu watavipelekea vyama vya siasa Daftari hilo.

Kwa upande wa malalamiko yaliyowasilishwa NEC, alisema yapo matatu na Kamati ya Maadili imeshashughulikia la CCM dhidi ya CUF na Chadema na jana ilipanga kushughulikia rufaa ya NCCR, iliyowasilishwa kutoka Iringa na ya chama hicho dhidi ya kituo cha televisheni cha TBC1.

Hata hivyo, alikataa kuzungumzia kwa undani rufaa hizo zinahusu nini na kuahidi kutoa maelezo wakati wa kutangaza uamuzi.

Awali Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lewis Makame, alitoa kauli ya Tume kuhusu mwenendo wa uchaguzi ambapo alisema ni muhimu vyama vya siasa viendeshe kampeni kwa njia ya busara na kuheshimiana na vijikite kutangaza sera na ilani zao, na pia kunadi wagombea na zisiwe za lugha za kejeli, matusi au vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjaji amani.

Aliwataka wagombea kutosita kupeleka malalamiko Tume au kwa wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo wanayoona kuna ukiukwaji wa sheria na maadili ya uchaguzi, ili hatua zichukuliwe ipasavyo.

Jaji Makame alisema katika tathmini ya Tume hiyo ya mwezi mmoja licha ya kampeni kuendelea vizuri katika maeneo yote ya nchi kwa wagombea kufuata ratiba na kueleza sera na ilani zao, bado katika baadhi ya maeneo kumeonekana wafuasi wa vyama kuingilia mikutano ya uchaguzi ya vyama vingine na kusababisha fujo.

Alitaja dosari nyingine kuwa ni baadhi ya vyama na wagombea kufanya mikutano nje ya muda ulioruhusiwa; wagombea kuhutubia kwa lugha za kejeli, matusi na kushambulia wengine na wafuasi wa vyama kuwa na jazba na kuchana bendera na mabango ya vyama vingine.

Pia baadhi ya wagombea kutumia lugha za kienyeji badala ya Kiswahili ambapo alifafanua: “Kuna baadhi ya maeneo watu hawafahamu vizuri Kiswahili, mgombea atumie Kiswahili na awepo mkalimani atakayetafsiri”.

Alitaja ukiukwaji mwingine wa maadili na kanuni kuwa ni wafuasi wa baadhi ya vyama kubughudhi waandishi wa habari na kuwalazimisha kuvaa sare za vyama vyao; vyama kutumia mabango yasiyoidhinishwa na Tume na baadhi ya vyombo kutotoa taarifa sahihi zisizoegemea upande wowote.

Source: Habari Leo

Mtazamo: Haya wanaanza kuumbua wenyewe kwa wenyewe kweli ukombozi wa Tanzania waja. Ndio matatizo ya idara kuendeshwa na siasa badala ya sheria.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom