Elections 2010 Dk Slaa, NEC wamshukia Tendwa!

mgonjwa mwenye taahira aliyepewa jukumu la kuwatibu madaktari.

Msanii, hii imetulia!
hahaha mkuu nilipost kwa hasira ndo ninaisoma sasa. duh hata mie nakubali kuwa jamaa ni ovyo kuliko hovyoooo
 
Haya mwana nijuze hayo ya mbeya kulikuwa na nini. Asee kukaa kijiji mbaya! sina nijualo ati. Nimegee hiyo mkuu.

Aaaaaah, mjomba...hata kama unakaa bush ilitakiwa uwe umeyasikia yaliyompata mkuu wa kaya huko mbeya. ALitembea usiku wananchi wakaurushia mawe msafara wake. Kuanzia hapo akazuiwa asiwe anatembea usiku. Naona sijui "jamaa" zake wamesahau kumkumbusha
 
Bwana John Tendwa, ni mtu anayejiona kuwa yuko juu ya kila kitu when it comes to vyama vya upinzani. Jamaa ananyodo huyo, na hastahili hasa kuwa katika nafasi kama hiyo alonayo. Nafikiri nafasi hiyo inafaa akateuliwa mtu mwingine na ambaye ataidhinishwa na bunge. Lakini, kwa ufupi huyu jamaa hafai, hafai,hafai, japo kwa kulumangiwa kwa ugali.
 
Ukali na msimamao huu wa jaji Makame tunaomba uwe wa dhati na thabiti mpaka kwenye kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais. Asiishie kumkanya Tendwa tu halafu ikija kwenye kutangaza matokeo apate kigugumizi (maana Kikwete kishashindwa tayari) kuwaruhusu CCM kuchakachua matokeo.
 
Angalau taaluma ya Lewis Makame imeonekana katika hili, kwani ametoa tafsiri ya sheria ya uchaguzi bila kutafuta maneno tofauti kabisa na msanii Tendwa. Tunapozungumzia Tume huru ya uchaguzi inatakiwa ichaguliwe kwa mfumo tofauti na ilivyo hii ya sasa kwa kuwa ina taathira ya kumjali aliyemteua.
Ingekuwa vyema tume huru ya uchaguzi ikachaguliwa na jopo huru kama tunavyoweza kuona angalau anachofanya Lewis, binafsi amenitia moyo mno ingawa ana kazi ya kufanya kwani kusema tu pekee haitoshi. Tunahitaji mbwa abwekae awe na meno ya kuwajeruhi wahalifu na sio kuishia kubweka tu.
 
Back
Top Bottom