Dk Slaa, Mnyika, Lema matatani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa, Mnyika, Lema matatani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jul 10, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 09 July 2012 20:53 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [​IMG]  Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Willibrod Slaa

  POLISI KUWAHOJI KWA MATAMSHI KWAMBA WANATISHIWA MAISHA, DK NCHIMBI ASEMA WANASABABISHA CHUKI
  Neville Meena na Florence Majani, Dodoma
  KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema huenda wakajikuta matatani kutokana na madai waliyoyatoa juzi kwamba wanatishiwa kuuawa na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa.Kutokana na matamshi hayo, jana Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ameliagiza Jeshi la Polisi kuwahoji viongozi hao ambao walidai kuwa mauaji hayo yamepangwa kufanywa kwa kuwekewa sumu kwenye chakula au kwa kutumiwa makundi ya ujambazi.

  Akizungumza na waandishi wa mjini hapa jana, Dk Nchimbi alisema licha ya kudai kwamba wanatishiwa, ameshangazwa na msimamo wa viongozi hao kukataa kupeleka suala hilo polisi kwa madai ya kuhofia suala hilo halitafanyiwa kazi.

  Alisema watawahoji viongozi hao kwa sababu suala la usalama wa Mtanzania yeyote si la hiari, bali ni la kikatiba na la kisheria hivyo, ni lazima polisi watimize wajibu wao.

  "Ni lazima tuwahoji ili tujue ni nani amewatisha na kwa sababu zipi. Hatutamuomba mtu ruhusa ya kumlinda kwa sababu huo ni wajibu na kazi yetu kuwalinda raia, hilo halina mjadala. Hatua zitachukuliwa endapo itabainika kuwa madai yao yana ukweli," alisema Dk Nchimbi.

  Aliwataka viongozi wote wa kisiasa wakiwamo wa Chadema wanapohisi kutishiwa usalama wao, watoe taarifa polisi ili vyombo vya dola viyafanyie uchunguzi malalamiko yao ili utaratibu ufanyike kuhusu usalama wao kama sheria inavyotaka.

  Alionya tabia ya viongozi kuzungumza nje ya utaratibu akisema haikubaliki kwani inaweza kuwa ni mbinu za kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

  Dk Nchimbi alisema jambo hilo si jema kwani linajenga hofu miongoni mwa Watanzania na kuwafanya wasiviamini vyombo vyao vinavyowalinda kwa mujibu wa sheria.
  "Ni kweli kuwa kila mwanasiasa anataka kukubalika na umma lakini, akubalike katika taratibu zinazokubalika," alisema Dk Nchimbi na kuongeza:

  "Ingekuwa Serikali inataka kukubali umaarufu kama huo, basi ingetumia mwanya wa haohao Chadema wakati mitandao ya kijamii iliposambaza taarifa kuwa Chadema ilihusika na kifo cha marehemu, Chacha Wangwe."

  Alisema Serikali haikukurupuka na kuwakamata, badala yake ilifanya uchunguzi kwanza na matokeo yake alikamatwa dereva wake ambaye ameshachukuliwa hatua.
  Alisema kama Serikali ingekuwa inatafuta umaarufu, ilikuwa ni fursa nzuri kwake kujipatia umaarufu na kukivuruga chama hicho kwa kuwakamata viongozi wa Chadema hasa baada ya kuwapo kwa uvumi kwamba wamemuua kiongozi huyo.

  "Viongozi wetu wa kisiasa ni lazima wafanye mambo ambayo kesho na keshokutwa watakiri mchango wao, ama katika ujenzi au uharibifu wa nchi yetu. Kila siku wakilalamika kuwa wanataka kuuawa basi ni lazima watu watawashangaa kwani badala ya kutatua matatizo ya wananchi wanabaki wakilalama wanataka kuuawa. Watu kama hawa wanafanya hivi kwa masilahi yao, wanaweza kuwagombanisha wananchi."

  Waziri Nchimbi aliwataka wananchi na viongozi wa kisiasa kuondoa hofu kwani Serikali ina wajibu wa kuwalinda na hakuna mtu atakayenufaika kwa mauaji ya wanasiasa hao.

  Kuhusu madai kwamba polisi wamekuwa wakipuuza malalamiko ya wapinzani, Dk Nchimbi alikiri kuwapo kwa baadhi ya polisi wenye kasoro katika utendaji wao lakini akasema wengi ni waadilifu.
  Alisema ikiwa kuna mtu haridhishwi na utendaji wa polisi kwa kutopata huduma kama inavyostahili, ana uhuru wa kutoa taarifa katika ngazi za juu hata ikiwa ni kwake.

  Ikulu nayo yatoa tamko

  Katika hatua nyingine, Ikulu imesema hakuna mpango wowote unaoratibiwa na Idara ya Usalama wa Taifa kwa lengo la kuwaua viongozi hao wa Chadema.
  Jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alihoji sababu za Serikali kutaka kuwaua viongozi hao wakati si tishio lolote kwa nchi.

  Balozi Sefue alisema Idara ya Usalama wa Taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi, bali kulinda masilahi ya taifa na kuhoji: "Sasa kwa nini wauawe? Wana nini hasa hadi Idara ya Usalama ifanye hivyo?"

  Alisema ni vyema wakati mwingine kukawa na umakini kwa kuangalia namna siasa zinavyoweza kufanya kazi... "Hii inaweza kuwa siasa tu. Sisi serikalini hatuna mambo ya vyama, tunafanya kazi kwa ajili ya watu wote."

  Alisema Idara ya Usalama wa Taifa na Serikali hazifanyi kazi kisiasa, bali kwa kuangalia masilahi ya Watanzania wote: "Huku serikalini sisi hatuna ugomvi na wanasiasa. Tunafanya kazi na watu wote."
  Alisema wanaoweza kufikiria kuwa kuna siasa katika Serikali na vyombo vyake wao ndiyo wanaweza wakawa wanafanya siasa.

  Tuhuma za Chadema
  Kauli hizo za Serikali zinatokana na tuhuma za Chadema kwamba kimebaini njama za kuwaua viongozi wake hao waandamizi ambazo zinaratibiwa na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa na kwamba nyendo zao zimekuwa zikifuatiliwa kwa saa 24.

  Tuhuma hizo za Chadema zilitolewa juzi na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni akisema: "Sisi Chadema hatuna mambo ya siri tunayotaka kufanya katika nchi hii. Matatizo ya Watanzania yapo wazi na yanajulikana na kila mmoja, Serikali ya CCM itekeleze sera na ahadi zao kwa wananchi na si vitisho."

  Chanzo: Mwananchi
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Taifa lipi linalolindwa maslahi yake la uswiss? au la mafisadi, je kuruhusu ndege za mataifa mengine kutua na kubeba twiga wetu ni maslahi ya nchi ipi...serikali iache usege wasifiki watanzania wote bado mapoyoyo..Kwanini mlitaka kumuua Dr. ulimboka, kwanini mlitaka kumuua Mwakyembe walikuwa na nini? au mnao wauwa kama mlivyo muua karume na Nyerere walikuwa na nini? au yalikuwa maslahi ya nchi ipi....
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naamini hakuakuwa na jipya katika hili zaidi ya kutululiza upepo!!!!
   
 4. m

  meemba Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali ya uswahili mwingi inaelekea kuzama,dunia ya leo ni kujenga hoja ndiyo jambo la msingi,Hawa mafisadi na genge la wahuni WANAMTISHA NANI?dunia hii?Mnaweza kuua watanzania wote?Ni nani mnamjengea nidhamu ya uoga?Kipindi kile cha kutisha watu kimepita kitambo sana MUWE MACHO MAGAMBA
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Vichwa vya habari vya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na thithiemu!!!!
   
 6. D

  DOMA JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Lusinde naye ahojiwe
   
 7. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Waache kutisha watu wazima bana .....kama mtu katishiwa kifo asiseme?????....Watanzania wa leo sio wale wa enzi za mwalimu jamani.....wa leo wameamka vilivyo!
   
 8. m

  maingu z Senior Member

  #8
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo makanusho ni kawaida kwa mwalifu yeyeto, tangu lini ulishawahi kusikia mtu ana kiri kuwa mimi ni mwizi,au mimi ni muuwaji au mimi ni fisadi, hata kama amekutwa anatekeleza uhalifu wake lakini bado atajitetea. Ndiyo ilivyo kwa watawala je wanaweza kukiri kuwa wao wanataka kutekeleza hayo wanayoshutumiwa?
   
 9. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  kwa nn mnahangaika na cdm?Embu nyamazeni muwaone
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Waandishi wa habari vilaza sana...
   
 11. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ngoja tumfundishe kazi huyu sefue kwa kumkumbusha yafuatayo ili ajue Serikali huwaua hata wasio na chochote
  1 Gari ya kikwete rais wa taifa hili liliwekwa maji badala ya mafuta likazima njiani
  2 Msafara wa rais ulipigwa mawe pale mbeya na tegeta je huoni kama watu wale wangekua na mabomu tungempoteza?
  3 Vyeti vya kidato cha sita viliibwa bale baraza la mitihani na hakuna aliyekamatwa usalama wa taifa wako wapi?
  4 Ndege ya jeshi ikiwa mbovu na chakavu ilinunuliwa kwa bei ya ajabu na akina chenge usalama walikua wapi kutujuza?
  5 Makampuni ya kijambazi yalipokwiba mabilioni pale Bot kwani hakuna usalama wa taifa na polisi pale?
  6 Mwenyekiti wa chadema kata ya usa river sio mtanzania?Mbona kachwa kama mbuzi polisi walikua wapi kuwalinda?
  7 Dr.ulimboka?au mmemsahau saa hizi?
  Endeleeni ila ipo siku ama zenu au zetu mpaka mtajuta kutudhulumu kiasi hiki!
   
 12. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #12
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mhe Nchimbi labda anatetea asichokijua,kwani Dr Mwakyembe alilalamika mara ngapi kuwa anatishiwa kuuwawa mwishowe si aliwekewa sumu??? Lazima watu waseme wasife kibudu watu wajue sababu ya kifo ikiwa itatokea!!!!
   
 13. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,684
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Very good! Wapasulie ukweli watie akili.
   
 14. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hii Bumba !
   
 15. kitali

  kitali JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 972
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 80
  hata mkanushe kupitia means gani,bt conclusion ni kwamba thithiemu ni killers mliokubuhu,eti mnajidai kukanusha!! hiyo ni tayar ishaingia kwenye damu zetu.
   
 16. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2013
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi hili sakata liliishia wapi?

  PM
   
 17. Isaac JK

  Isaac JK JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2013
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  eti nchimbi naye kajibu mapgo
   
 18. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi Mwandishi David Mwangosi aliuwawa na nani vile?
   
 19. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF, Hivi huyu Sefue anatofauti gani na Juliana wakufyonzwa? Eeee kwani nchi hii ina usalama wa taifa? Nijuavyo mimi usalama wa taifa alizikwa nao mwl.Nyerere, na waliopo kwa sasa ni usalama wa CCM. Sefue asitufanye wote ni mamburula kama magambaz.
   
 20. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2013
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,507
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hivi Dr. Mwakyembe alishahojiwa???
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...