Dk Slaa, Mnyika, Lema matatani

Dk Slaa, Mnyika, Lema matatani

Status
Not open for further replies.
Mh Sefue tafadhali subiri hao viongozi wahojiwe ili tujue UWT unahusika vipi kwenye hili. Si hekima kukanusha haraka tuhuma hizi bila kusikia kauli za viongozi wa chadema waliozileta.
 
Hivi wale waliomteka Dr.Ulimboka baada ya kutajwa wamefanyiwa nn au ndio yaleyale
 
Mh mwakyembe pamoja na kutoa taarifa kwa maandishi na kuripoti polisi bado mpango wa kumdhuru uliendelea mpaka alipoponea chupuchupu,je Nchimbi anatuambia vipi watanzania kwa hilo.

Dk ulimboka aliteswa na akaelezea yote ilivyotokea hadi akaponea tundu la sindano, je? Nchimbi na sefue wako wapi kwa hili mpaka sasa.

Mauaji ya mwangosi yametekelezwa hadharani tena mbele ya kamanda kamhanda ,je sefue anatuambia vipi kwa hilo.

Mauaji ya padre kule zanzibar yametokea na hawa uhasama wa taifa wapo lakini rais kaamua kuomba msaada wa FBI, je sefue haoni kwamba hakuna usalama wa taifa hapo bali uhasama wa taifa na ndio maana hata rais inaelekea hana imani na vyombo vyetu vya usalama na ndio maana kaomba msaada toka ughaibuni

Nchimbi kwa hili ulitakiwa uanze kujitafakari na kuchukua uamuzi mgumu,unajiuzulu afu Mwema nae angekufuata na labda hata hawa kina sefue naoo wangekufuata nyuma kujiuzulu,afu hoja iletwe bungeni ya kuubadili mfumo wetu wa usalama wa taifa wa kweli unaowajibika kama aliouacha baba wa taifa
 
nyie bwekeni tu. ila mkiwagusa ndo mtajua kuwa hii nchi wenyewe wapo hai. kama hatutawanyotoa matumbo yenu kabla hata ya 2015.
 
nyie bwekeni tu. ila mkiwagusa ndo mtajua kuwa hii nchi wenyewe wapo hai. kama hatutawanyotoa matumbo yenu kabla hata ya 2015.

Usalama wa taifa hakuna Tz bali usalama wa ccm upo. Sefue na kundi lake wapo kulipa fadhila kwa boc wao maana mifano ipo waz wanavyowatetea wavunja amani ili mradi wapo ktk ccm na c rahic kuitofautisha serkal na ccm. Ila yana mwisho
 
Taifa lipi linalolindwa maslahi yake la uswiss? au la mafisadi, je kuruhusu ndege za mataifa mengine kutua na kubeba twiga wetu ni maslahi ya nchi ipi...serikali iache usege wasifiki watanzania wote bado mapoyoyo..Kwanini mlitaka kumuua Dr. ulimboka, kwanini mlitaka kumuua Mwakyembe walikuwa na nini? au mnao wauwa kama mlivyo muua karume na Nyerere walikuwa na nini? au yalikuwa maslahi ya nchi ipi....


ama kweli wewe ndio MAPOYOYO haswa, hebu rudia mwenye usome uliyoya andika. NONSENSE and UN INTELIGENT,
 
Wana JF, Hivi huyu Sefue anatofauti gani na Juliana wakufyonzwa? Eeee kwani nchi hii ina usalama wa taifa? Nijuavyo mimi usalama wa taifa alizikwa nao mwl.Nyerere, na waliopo kwa sasa ni usalama wa CCM. Sefue asitufanye wote ni mamburula kama magambaz.
Ni usalama wa wahuni na majangili/mafisadi ya CCM....
 
ama kweli wewe ndio MAPOYOYO haswa, hebu rudia mwenye usome uliyoya andika. NONSENSE and UN INTELIGENT,
Mimi siyo poyoyo kwasababu najitambua pimbi wewe, rudia kosoma wewe mimi nilishaandika tangu mwaka jana..
 
Nchimbi sasa unatutatiza?Mbona Mwigulu alisema ana CD ya mpango wa CDM kufanya mauaji hatujasikia ukisema lolte?Ni kweli hata sisi wananchi hatuna imani na JEshi la Polisi.Hakuna linachofanya.Kama Dr Ulimboka alimuona mtu wa usalama wa Taifa na anamjua mbona mpaka leo jeshi lako la jikono halijamhoji?Na wewe Sefue kama kweli kuna usalama wa taifa mbona hatusikii lolote kuhus Meremeta?Usalama gani mnaouzungumzia?Rushwa imetapakaa,usalama mpo wapi kuwasaidia TAKUKURU walioshindwa?Mwakyembe alisema aliwekewa sumu hamjaweza kufuatilia lolote.Naweza kuongea kwa kujiamini kwa sasa hakuna usalama wa taifa maana hata hao mliowaajiri kindugu hawana sifa wanaishia kijisisfu tu mitaani na Rais amethibitisha hilo kwa kuita wapelelezi toka nje.usalama wa taifa na Jeshi la Pollisi aibu tupu
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"][/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Monday, 09 July 2012 20:53
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
dr-slaa.jpg




Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Willibrod Slaa

POLISI KUWAHOJI KWA MATAMSHI KWAMBA WANATISHIWA MAISHA, DK NCHIMBI ASEMA WANASABABISHA CHUKI
Neville Meena na Florence Majani, Dodoma
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema huenda wakajikuta matatani kutokana na madai waliyoyatoa juzi kwamba wanatishiwa kuuawa na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa.Kutokana na matamshi hayo, jana Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ameliagiza Jeshi la Polisi kuwahoji viongozi hao ambao walidai kuwa mauaji hayo yamepangwa kufanywa kwa kuwekewa sumu kwenye chakula au kwa kutumiwa makundi ya ujambazi.

Akizungumza na waandishi wa mjini hapa jana, Dk Nchimbi alisema licha ya kudai kwamba wanatishiwa, ameshangazwa na msimamo wa viongozi hao kukataa kupeleka suala hilo polisi kwa madai ya kuhofia suala hilo halitafanyiwa kazi.

Alisema watawahoji viongozi hao kwa sababu suala la usalama wa Mtanzania yeyote si la hiari, bali ni la kikatiba na la kisheria hivyo, ni lazima polisi watimize wajibu wao.

“Ni lazima tuwahoji ili tujue ni nani amewatisha na kwa sababu zipi. Hatutamuomba mtu ruhusa ya kumlinda kwa sababu huo ni wajibu na kazi yetu kuwalinda raia, hilo halina mjadala. Hatua zitachukuliwa endapo itabainika kuwa madai yao yana ukweli,” alisema Dk Nchimbi.

Aliwataka viongozi wote wa kisiasa wakiwamo wa Chadema wanapohisi kutishiwa usalama wao, watoe taarifa polisi ili vyombo vya dola viyafanyie uchunguzi malalamiko yao ili utaratibu ufanyike kuhusu usalama wao kama sheria inavyotaka.

Alionya tabia ya viongozi kuzungumza nje ya utaratibu akisema haikubaliki kwani inaweza kuwa ni mbinu za kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

Dk Nchimbi alisema jambo hilo si jema kwani linajenga hofu miongoni mwa Watanzania na kuwafanya wasiviamini vyombo vyao vinavyowalinda kwa mujibu wa sheria.
“Ni kweli kuwa kila mwanasiasa anataka kukubalika na umma lakini, akubalike katika taratibu zinazokubalika,” alisema Dk Nchimbi na kuongeza:

“Ingekuwa Serikali inataka kukubali umaarufu kama huo, basi ingetumia mwanya wa haohao Chadema wakati mitandao ya kijamii iliposambaza taarifa kuwa Chadema ilihusika na kifo cha marehemu, Chacha Wangwe.”

Alisema Serikali haikukurupuka na kuwakamata, badala yake ilifanya uchunguzi kwanza na matokeo yake alikamatwa dereva wake ambaye ameshachukuliwa hatua.
Alisema kama Serikali ingekuwa inatafuta umaarufu, ilikuwa ni fursa nzuri kwake kujipatia umaarufu na kukivuruga chama hicho kwa kuwakamata viongozi wa Chadema hasa baada ya kuwapo kwa uvumi kwamba wamemuua kiongozi huyo.

“Viongozi wetu wa kisiasa ni lazima wafanye mambo ambayo kesho na keshokutwa watakiri mchango wao, ama katika ujenzi au uharibifu wa nchi yetu. Kila siku wakilalamika kuwa wanataka kuuawa basi ni lazima watu watawashangaa kwani badala ya kutatua matatizo ya wananchi wanabaki wakilalama wanataka kuuawa. Watu kama hawa wanafanya hivi kwa masilahi yao, wanaweza kuwagombanisha wananchi.”

Waziri Nchimbi aliwataka wananchi na viongozi wa kisiasa kuondoa hofu kwani Serikali ina wajibu wa kuwalinda na hakuna mtu atakayenufaika kwa mauaji ya wanasiasa hao.

Kuhusu madai kwamba polisi wamekuwa wakipuuza malalamiko ya wapinzani, Dk Nchimbi alikiri kuwapo kwa baadhi ya polisi wenye kasoro katika utendaji wao lakini akasema wengi ni waadilifu.
Alisema ikiwa kuna mtu haridhishwi na utendaji wa polisi kwa kutopata huduma kama inavyostahili, ana uhuru wa kutoa taarifa katika ngazi za juu hata ikiwa ni kwake.

Ikulu nayo yatoa tamko

Katika hatua nyingine, Ikulu imesema hakuna mpango wowote unaoratibiwa na Idara ya Usalama wa Taifa kwa lengo la kuwaua viongozi hao wa Chadema.
Jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alihoji sababu za Serikali kutaka kuwaua viongozi hao wakati si tishio lolote kwa nchi.

Balozi Sefue alisema Idara ya Usalama wa Taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi, bali kulinda masilahi ya taifa na kuhoji: “Sasa kwa nini wauawe? Wana nini hasa hadi Idara ya Usalama ifanye hivyo?”

Alisema ni vyema wakati mwingine kukawa na umakini kwa kuangalia namna siasa zinavyoweza kufanya kazi... “Hii inaweza kuwa siasa tu. Sisi serikalini hatuna mambo ya vyama, tunafanya kazi kwa ajili ya watu wote.”

Alisema Idara ya Usalama wa Taifa na Serikali hazifanyi kazi kisiasa, bali kwa kuangalia masilahi ya Watanzania wote: “Huku serikalini sisi hatuna ugomvi na wanasiasa. Tunafanya kazi na watu wote.”
Alisema wanaoweza kufikiria kuwa kuna siasa katika Serikali na vyombo vyake wao ndiyo wanaweza wakawa wanafanya siasa.

Tuhuma za Chadema
Kauli hizo za Serikali zinatokana na tuhuma za Chadema kwamba kimebaini njama za kuwaua viongozi wake hao waandamizi ambazo zinaratibiwa na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa na kwamba nyendo zao zimekuwa zikifuatiliwa kwa saa 24.

Tuhuma hizo za Chadema zilitolewa juzi na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni akisema: “Sisi Chadema hatuna mambo ya siri tunayotaka kufanya katika nchi hii. Matatizo ya Watanzania yapo wazi na yanajulikana na kila mmoja, Serikali ya CCM itekeleze sera na ahadi zao kwa wananchi na si vitisho.”

Chanzo: Mwananchi
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Sefue anaongea nini upuuzi mtupu, anajua usalama ni siri siku hizi? usalama ushateketeza wangapi?nani asiyejua kisa hasa cha Nchimbi kuwepo kwenye system? ameshasuka mikakati mingapi ya kuondoa watu au unafikiri ni siri?tunawaangalia tu. alafu sefue mbona we akili yako ndogo sana?Silaa si tishio, Mnyika na Lema hujui mpact zao katika taifa?kwani wewe unaklaa wapi na unafatilia nini?ama kweli matumbo yenu yanawadharirisha.
 
waTZ hawana imani na PolisiCCM na UWT. Kwanza wameshindwa kudhibiti masuala ya kidini yanayo endelea yaliyo kinyume na katiba.
 
Jamani anesema anataka kuuawa na asemaye ni cd wa wauaji .Nchimbi muhoji kwanza Nchemba kisha wahoji na Slaa na wenzake. Toa kwanza bariti ndani ya jicho lako.....
 
huko ni kuishiwa sera. slaa anatapatapa. jana moro mjini kulikua na mkutano wa hadhara wa ccm. nilipitia kusikiliza nini wanasema. siyo siri mabomu yaliyorushwa na juliana shonza pamoja na wenzake kuhusu uendeshaji wa chdm, yaliniacha mdomo wazi. wananchi walifurahi hadi wakaamua kuwabeba!
6.jpg

juliana akibebwa kama mtoto mdogo
2B.jpg

mwampamba akibebwa.
9.jpg

wanachama wapya kutoka chadema na cuf wakila kiapo jana 3/3/2013 mjini morogoro
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom