Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

Nimeshajua kwanini waganda-kyaka(mojawapo ya jamii za kihaya) wa Nkenge kule wilayani Misenyi walimkataa Kamala...... Ni mbumbumbu saaaaana..... Naamini wataalamu wa CHADEMA watamjibu utumbo wake........
 
leo, waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki, dk diodorus kamala, alisema dk slaa katika uchumi ni mbumbumbu na inaonekana anazungumza asichokijua na kudanganya wananchi.

dk kamala alisema ahadi hiyo ni ya uongo kwani sh 5,000 ni gharama ya usafirishaji wa mfuko kutoka dar es salaam hadi mwanza kwa njia ya reli na tani moja ya saruji ya mifuko 20 ni sh 100,000 hivyo gharama kwa mfuko kuwa sh 5,000 sawa na bei anayowaahidi watanzania. alisema gharama za uzalishaji si chini ya sh 7,000 kwa mfuko na kabla ya kuongeza gharama nyingine, mfuko wa saruji unapofika mwanza gharama inakuwa zaidi ya sh 12,000, hivyo kwa bei yake kuwa kubwa.

Dk kamala alisema hoja hiyo ni ndoto ambayo hata viongozi wa nchi tajiri duniani hawatarajii kuiota mbali na kuitekeleza na huko ni kudanganya wananchi. Akizungumzia hoja ya makubaliano ya jumuiya ya afrika mashariki (eac) kwamba yanaumiza watanzania, alisema dk. Slaa anapotosha kwani msingi mkuu wa makubaliano hayo ni ushirikiano huo kujengwa hatua kwa hatua kulingana na ridhaa ya wananchi. “serikali imekuwa ikizingatia msingi huu kikamilifu kwa kushirikisha wananchi, likiwamo bunge ambalo dk slaa amekuwamo kwa miaka mingi, mfumo huu unaziwezesha nchi wanachama kupata fursa ya kujipanga vema katika utekelezaji na kuitumia ngazi moja kuwa msingi wa kupanda ngazi inayofuata ya utangamano,“ alisema kamala.

Kuhusu mfumo wa kodi katika jumuiya, alisema si kweli kwamba aliuanzisha yeye, kwa kuwa yalianza kabla hajawa waziri na haiwezekani ushuru ufutwe bila kujadiliana na kukubaliana nchi wanachama, hivyo akasema dk.slaa hawezi kufuta ushuru huo kwani ni lazima ajadiliane na viongozi wa eac.

Kuhusu viwango vya vat alisema dk. Slaa ameonesha hajui kuwa kodi hiyo si ya afrika mashariki na kiasi cha vat anacholipa mlaji kinategemea bei ya bidhaa katika soko, huku akitolea mfano wa maji ya kunywa ya ujazo wa nusu lita, ambayo tanzania yanauzwa sh 500 na kenya sh 800 ingawa mkenya analipa vat ya asilimia 16 na mtanzania asilimia 18; mkenya analipa kiasi kikubwa kuliko mtanzania.

Alisema kabla dk. Slaa kusema tanzania imeliwa, kwa kuwa na kiwango cha juu cha vat afrika mashariki, alitakiwa kuelewa kwamba vat si kodi ya afrika mashariki na katika uchumi, huwezi kulinganisha viwango vya vat kabla ya kuangalia mfumuko wa bei kwenye nchi unazotaka kulinganisha, na kabla haujakokotoa, lazima uangalie viwango vya thamani ya kubadilisha fedha na gharama ya maisha.

alimtaka dk. Slaa kuwaomba radhi watanzania kwa kuwadhalilisha akiwaita mbumbumbu, kielimu na katika kufanya biashara, huku akitaka kura zao, jambo ambalo si kweli, kwani miaka mingi tanzania imekuwa kitovu cha elimu katika kanda hii huku viongozi wake wengi wakisoma tanzania.

sasa kama ccm imeshindwa si ikae pembeni?

kwanza kabisa dr kamala ni miongoni mwa mafisadi wa elimu waliotajwa na msemakweli. Na katika kuthibitisha kuwa yeye ndio mbumbumbu gharama za usafirshaji hapa nchini zinakuwa za juu kiasi hicho kkutokana na sera za ccm kuua reli na hivyo wasafirishaji kulazimika kutumia usafiri wa magari amabo una ghrama za juu. Haya ndio mamabo ambayo dr slaa anataka kuyaondoa akifanikiwa kupata urais. Sasa kama dr kamala anashindwa kutambua kuwa usafiri wa reli ni gharama nafuu kuliko barabara na kuishauri ccm yake hivyo, atawezaje kutushawishi watanzania tumuamini? Inabidi dr kamala arudi shule ili kujiondolea ufisadi wa elimu ndipo ajitokeze kuzungumza na wasomi wa kweli kama dr slaa.
 
.....Heko JK kwa uwezo wako wa kuzima moto unaoendelea kukuteketeza kwa kutumia makada maboya kama Dr. Kamala.....Nafuu yako ni kwamba wakati wa kujibu mapigo goodwill yako haitazidi kuporomoka (na kwahiyo hutazidi kupoteza kura) kutokana na ustadi wako kujiwekea shield kwa kutumia vilaza type ya Dr. Kamala.....maana iwapo hoja itaonekana dhaifu wa kuchafua jina zaidi ni Dr. Kamala na wala si JK!!!!!

Bob Marley aliishaimba wimbo wenye verse hii " I shot the sheriff but I did'nt shoot the deputy" ambao unaonyesha fedheha atakayopata Dr. Kamala endapo hoja zake zitagaragazwa kwa kutumiwa vibaya na wachumia tumbo wa CCM!!!!! Atakaye aibika ni Dr. Kamala(Sheriff) lakini JK(Deputy) atabaki salama.....

Wanasiasa msikubali kutumiwa kichwakichwa hivyo...... Kamala alitakiwa ajiulize kwanini Mustapha Mkulo(waziri wa fedha na uchumi) hakujitokeza kujibu mapigo hayo!!!!! Au waziri mkuu, Mizengo Pinda hashiriki wazi wazi katika kampeni za uraisi pamoja na kwamba yeye ni mojawapo ya wanasiasa wa CCM ambao walau wana usafi unaoonekana dhahiri.... Hawa wanajua vyema kusoma alama za nyakati!!!!!!!!

 
Hivi Dr Kamala ni daktari wa mitishamba au wa falsafa? Ndiyo maana alishindwa kwenye kura za maoni. Dr Slaa akiwa mkuu wa nchi anahaki ya kupendekeza mabadiliko ndani ya EAC kupitia bunge lake. Kamala anyamaze kwa kuwa mawazo ya serikali yake si mawazo ya serikali ya DR SLAA.
 
Jamani Kamala si ndio mwenye Vyeti fake vya udoctorate ? Na si ndio huko kwao wamemwaga? Sasa hajiulizi kwa nini wanachi tu wa kawaida wamempiga chini kabla ya kubwatuka batuka? Ujinga ni ujinga tuuu hata ukiwa mjanja wa macho.
 
Duh!huyu Mr kamala fisadi wa elimu naye anajipya?mara ya kwanza alimpinga Dr slaa basing on mkataba ya Jumuiya ya Afrika mashariki.Sasa amehamia kwenye gharama za usafirishaji!huyu jamaa ni mjinga sana ndiyo maana hata NKENGE walimshitukia.shame upon you Mr Kamala
 
Mimi nafikiri kamala hazimtoshi, kwanza ingekuwa busara akajiuliza kwanini kwao amekataliwa?, na isitoshe nina wasiwasi na elimu yake.
 
Umbumbumbu wa Kamala ndio mkubwa zaidi. Si ndo huyu kachakachua digrii yake na kujipa PhD feki? Hivi si alisema anakwenda mahakamani kumchitaki Msemakweli? Kaishia wapi? Nd sababu kamwagwa kwenye kura za maoni.
 
WanaJF,

Shule na vyeti haviongezi akili kichwani bali hunoa akili ilyopo!
Kama huna akili hata usome shule zote duniani na upate vyeti vyote ni BURE tu!
 
Huyu ni mtoto sana kwa Dk. Slaa na hana uzoefu wa kazi katika nyanja ya uchumi.
 
Leo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala, alisema Dk Slaa katika uchumi ni mbumbumbu na inaonekana anazungumza asichokijua na kudanganya wananchi.

Dk Kamala alisema ahadi hiyo ni ya uongo kwani Sh 5,000 ni gharama ya usafirishaji wa mfuko kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa njia ya reli na tani moja ya saruji ya mifuko 20 ni Sh 100,000 hivyo gharama kwa mfuko kuwa Sh 5,000 sawa na bei anayowaahidi Watanzania. Alisema gharama za uzalishaji si chini ya Sh 7,000 kwa mfuko na kabla ya kuongeza gharama nyingine, mfuko wa saruji unapofika Mwanza gharama inakuwa zaidi ya Sh 12,000, hivyo kwa bei yake kuwa kubwa.

Dk Kamala alisema hoja hiyo ni ndoto ambayo hata viongozi wa nchi tajiri duniani hawatarajii kuiota mbali na kuitekeleza na huko ni kudanganya wananchi. Akizungumzia hoja ya makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwamba yanaumiza Watanzania, alisema Dk. Slaa anapotosha kwani msingi mkuu wa makubaliano hayo ni ushirikiano huo kujengwa hatua kwa hatua kulingana na ridhaa ya wananchi. “Serikali imekuwa ikizingatia msingi huu kikamilifu kwa kushirikisha wananchi, likiwamo Bunge ambalo Dk Slaa amekuwamo kwa miaka mingi, mfumo huu unaziwezesha nchi wanachama kupata fursa ya kujipanga vema katika utekelezaji na kuitumia ngazi moja kuwa msingi wa kupanda ngazi inayofuata ya utangamano,“ alisema Kamala.

Kuhusu mfumo wa kodi katika jumuiya, alisema si kweli kwamba aliuanzisha yeye, kwa kuwa yalianza kabla hajawa waziri na haiwezekani ushuru ufutwe bila kujadiliana na kukubaliana nchi wanachama, hivyo akasema Dk.Slaa hawezi kufuta ushuru huo kwani ni lazima ajadiliane na viongozi wa EAC.

Kuhusu viwango vya VAT alisema Dk. Slaa ameonesha hajui kuwa kodi hiyo si ya Afrika Mashariki na kiasi cha VAT anacholipa mlaji kinategemea bei ya bidhaa katika soko, huku akitolea mfano wa maji ya kunywa ya ujazo wa nusu lita, ambayo Tanzania yanauzwa Sh 500 na Kenya Sh 800 ingawa Mkenya analipa VAT ya asilimia 16 na Mtanzania asilimia 18; Mkenya analipa kiasi kikubwa kuliko Mtanzania.

Alisema kabla Dk. Slaa kusema Tanzania imeliwa, kwa kuwa na kiwango cha juu cha VAT Afrika Mashariki, alitakiwa kuelewa kwamba VAT si kodi ya Afrika Mashariki na katika uchumi, huwezi kulinganisha viwango vya VAT kabla ya kuangalia mfumuko wa bei kwenye nchi unazotaka kulinganisha, na kabla haujakokotoa, lazima uangalie viwango vya thamani ya kubadilisha fedha na gharama ya maisha.

Alimtaka Dk. Slaa kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwadhalilisha akiwaita mbumbumbu, kielimu na katika kufanya biashara, huku akitaka kura zao, jambo ambalo si kweli, kwani miaka mingi Tanzania imekuwa kitovu cha elimu katika kanda hii huku viongozi wake wengi wakisoma Tanzania.

Sasa kama CCM Imeshindwa si ikae pembeni?

There's no other name for facts.
 
kamala si jinga la kwanza mpaka hajui wapi pa kutokea.....yeye hajui kwa nini tunataka mabadiliko richmond,EPA na mikataba hewa bado tunaumia kichwa kwa nini tuendelee kuipenda ccm majambazi....wezi kwa pesa zetu hasa kikwete na familia yake makamba,kinana,lowassa,sumaye na change,mramba......tukiwaondoa kisha tuwafunge ili iwe fundisho kwa wengine wala uchumi wa nchi...kazi wanayo tuwalinde wasikimbie nchi
 
kamala si jinga la kwanza mpaka hajui wapi pa kutokea.....yeye hajui kwa nini tunataka mabadiliko richmond,EPA na mikataba hewa bado tunaumia kichwa kwa nini tuendelee kuipenda ccm majambazi....wezi kwa pesa zetu hasa kikwete na familia yake makamba,kinana,lowassa,sumaye na change,mramba......tukiwaondoa kisha tuwafunge ili iwe fundisho kwa wengine wala uchumi wa nchi...kazi wanayo tuwalinde wasikimbie nchi
cHA AJABU CCM MPAKA LEO HAWAJAGUNDUA KWANINI WANACHUKIWA NA WANANCHI, UFISADI UMETAFUNA NCHI!
 
Si mbumbumbu kwenye uchumi tu, hata katika maisha yake binafsi amejionyesha ni mbumbumbu... Utatembeaje na mke wa mtu bila kujua?


Kibunango, Dr. Slaa angekuwa mbumbumbu mamilioni ya WATANZANIA wasingemkubali na juu ya yote nyie asingewakosesha usingizi kama mnavyohaha hovyo wakati huu!!
Huyu bwana ni makini na anajua anasema nini, huwezi kumfananisha na jamaa yenu hajui hata sababu ya nchi anayoitawala kwanini ni maskini!!
 
Back
Top Bottom