Dr. Slaa, mimi nakuunga miguu na mikono yote juu ya hili.
Dk Slaa kuanika hadharani nchi nzima posho za wabunge
Na Mussa Juma, Arusha.
MBUNGE wa jimbo la Karatu, Dk Willibrod Slaa (Chadema) amewataka?baadhi ya wabunge wanaomshutumu kwa kutangaza hadharani mishahara na posho za wabunge, kukaa kimya kwani amepanga kutembea nchi nzima na kutangaza mishahara hiyo ili wananchi wajue jinsi ambavyo nchi yao inaliwa na wachache.
Dk Slaa pia alisema licha ya kutangaza malipo hayo ili wananchi wayapinge kwa nguvu pia anapinga kutokatwa kodi mishahara na marupurupu yote ya wabunge jambo ambalo kwa mwezi linalipotezea taifa mabilioni ya fedha ambayo yangeweza kusaidia huduma za jamii.
"Nchi hii wanasema ni masikini, fikiria kuna wabunge 320 walipwe posho wakiwa Dodoma 135,000 kwa siku, mwisho wa mwezi milioni saba ambazo ni kiasi kidogo tu kinakatwa kodi. Hili ni jambo la ajabu?Ebu tazama maisha ya Watanzania vijijini na wamuogope Mungu," alisema Dk Slaa.
Akizungumza katika mikutano ya hadhara katika jimbo lake la Karatu, Dk Slaa alisema nia yake ya kutangaza posho, mishahara pamoja na marupurupu ya wabunge ni kuibua mjadala wa kitaifa ili malipo hayo ya wabunge na maofisa wengine wa serikali kupunguzwa.
Kwa kutumia mikutano ya 'Operation Sangara' nitatembea nchi nzima kufafanua jambo hili hata kama wakinifukuza bungeni sintojali kwani mimi nina dhamira ya kweli ya kuwatetea Watanzania wote," alisema akifafanua:
"Hawa wanaonipinga kwanza wanaishi Dar es Saalam, kwenye majimbo yao hawaendi, wanaogopa kutoa misaada kwa wapiga kura wao.?p> ?p> Alisema Rais Jakaya Kikwete aunde tume maalum ya kupitia maslahi ya wabunge na watumishi wote wa umma kwani sasa kuna tofauti kubwa sana ya mishahara jambo ambalo ni hatari kwa taifa.
Sasa jaribu kufikiria mishahara ya walimu wetu, madaktari, polisi ni sawa na posho ya siku ya mbunge au posho ya siku moja ya kiongozi anayehudhuria kikao cha bodi?Hili jambo hatari sana?na tusijifananishe na wabunge wa Kenya na Uganda, wao wana uchumi na taratibu za malipo tofauti na sisi,?alisema Dk Slaa.
Dk Slaa ambaye pia ni Katibu mkuu wa Chadema, alisema lazima tume au kamati maalum iundwe sasa kabla hali haijakuwa mbaya zaidi, ili kila mtumishi wa umma alipwe kutokana na ujuzi wake na uzoefu wake, sio sasa kundi moja linanufaika zaidi.
Akizungumzia tuhuma za baadhi ya wabunge kuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya bunge iliyopitisha nyongeza ya posho na marupurupu ya wabunge, Dk Slaa alikanusha na kudai kamati ya bunge inayotajwa haikuwahi kujadili suala la posho na malipo ya wabunge.
Ile kamati wanayoitaja ilikuwa inaongozwa na Job Ndugai ilikuwa ni ya kujifunza kanuni za bunge ambazo zinatumika katika nchi mbali mbali.
Kuna wabunge wanataka kupotosha hoja yangu, jambo hili lina msukumo wa watu wachache na lilijadiliwa katika Kamisheni ya bunge na mimi na wenzangu Chadema tunalipinga,?alisema Dk Slaa.
Alisema tangu mwaka 2006 amekuwa akilalamika bungeni juu ya malipo manono ya wabunge na watumishi wa kada za juu wa serikali, lakini amekuwa haeleweki isipokuwa amefarijika sasa Watanzania wameanza kumuelewa.
Alisema katika kikao kijacho cha bunge pia atalizungumza suala hilo la mishahara na posho za wabunge kupunguzwa na kukatwa kodi bila ya kificho na bila kumuogopa mtu yeyote.

Dk Slaa alipinga utetezi wa wabunge kuwa wana majukumu makubwa jimboni na kudai wengi wa wabunge wanaishi jijini Dar es Salaam na hakuna taarifa ya mahesabu ambayo wanatoa jinsi wanavyotumia fedha zao.