Sukununu
Member
- Feb 23, 2008
- 23
- 5
Dr. Slaa, mimi nakuunga miguu na mikono yote juu ya hili.
Nampongeza Dr. Slaa kwa uamuzi wa busara aliofanya, na ninamuombea mafanikio katika kuhakikisha kuwa malipo ya wabunge yanakuwa fair na siyo kuwanyonya wananchi. Hata hivyo nina masuali machache:
- Dr. Slaa mwenyewe amekuwa mbunge (na hivyo kupokea marupurupu hayo) tangu mwaka 1995. Yaani baada ya kuwa mbunge kwa miaka 13 sasa hivi ndio amegundua kuwa wabunge (including himself) wanalipwa fedha nyingi sana? Kwa nini miaka yote hiyo alikuwa hajagundua hili?
- Baada ya kugundua kuwa malipo hayo ni makubwa sana, yeye binafsi amefanya nini na fedha hizo "excess" kwa manufaa ya wapiga kura wake?