Na ikiwa ni ndio itakuaje... na ikiwa ni la itakuaje?"Sisi hatumchukii ila tunataka kujua ukweli, kama alipokuwa Ikulu, akiwa Rais wa taifa hili alifanya biashara na kuuza mali ya Watanzania. Tunataka atueleze kama kampuni iliyonunua Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira ni yake, mkewe, watoto wake na rafiki yake Yona au la?" alihoji Dk Slaa.
Mkapa aache kujificha na kutumia nyumba za Ibada ili kutaka kuficha madhambi yake. .
Mh. Dr.Slaa mkuu kaza uzi hadi huyu jamaa tumfikishe asipotaka..Hayo ni mawazo ya mtu mmoja tu kwani hata Bush ana watu wanaomkubali na ikasemekana kuwa ni chuki dhidi yake.
Pia nakuomba sana usitumie sana jina na imani ya dini kufikisha ujumbe wako kwani kimsingi (Kisiasa) huyo kiongozi wa dini ni raia wa Tanzania..Aliyozungumza huyo mchungaji hayahusiani hata kidogo na mafundisho ya dini yake...Ni wakati wetu sisi kuwaonyesha watu kama hawa kuwa tunaifahamu dini na tunaweza kuchambua mchele toka ktk pumba..
Ni kweli Mkapa amefanya maamuzi mengi maovu lakini ya maamuzi hayo, ameyafanya kama rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ana kinga dhidi ya kushitakiwa.
Uamuzi wa kuanzisha kampuni ya AnnBen aliufanya kama Benjamin Mkapa ambayo ni haki yake kama raia mwingine yoyote wa Tanzania.
Uamuzi wa kufanya biashara akiwa Ikulu, haya siyo majukumu ya rais kwa mujibu wa katiba, hivyo ile kinga ya kutoshitakiwa haihusiki. Kitendo cha kujiuzia Kiwira kwa bei poa, huku ni ukiukwaji wa maaadili ya uongozi ambayo nayo hayana kinga kwa mujibu wa katiba.
Kwa kifupi, kifungu kile kile kilichompa rais kinga ya kutoshitakiwa, pia ni kifungu hicho hicho kimeiondoa kinga hiyo endapo rais atavunja katiba ama atakiuka maadili ya uongozi.
Kutofikishhwa mbele ya vyombo vya sheria kwa Mkapa ni staha na heshima kwa rais mstaafu lakini sio kwa sababu ya kinga ya urais.
Asante kuniwekea vifungu vya katiba, umenirudisha mbali enzi za kudesa.Mkuu, kwa taarifa tu, Katiba inasema katika Ibara ya 46.-(1) "Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai." Ibara ya 46. -3, inatoa mamlaka kwa Bunge kama ifuatavyo. "Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii."
Pia ifahamike kuwa kila kipengele ndani ya Katiba hiyo kinajitegemea na hakuna kipengele kinachopinga kipengele kingine. Ndio maana hutumika maandishi kama "Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo,....."
Ukizingatia Katiba hiyo hiyo, nadhani ndio maana hakuna mtu aliethubutu kufungua mashitaka hayo mpaka sasa.
Asante kuniwekea vifungu vya katiba, umenirudisha mbali enzi za kudesa.
Japo jukumu la kutafsiri katiba na sheria ni la Mahakama kuu pekee, hebu naomba ionyeshe Ibara ya 46A kifungu (2)(a) na unitafsirie kama unamtafsiria mwananchi wa kawaida.
Mkuu, kwa taarifa tu, Katiba inasema katika Ibara ya 46.-(1) "Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai." Ibara ya 46. -3, inatoa mamlaka kwa Bunge kama ifuatavyo. "Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii."
Pia ifahamike kuwa kila kipengele ndani ya Katiba hiyo kinajitegemea na hakuna kipengele kinachopinga kipengele kingine. Ndio maana hutumika maandishi kama "Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo,....."
Ukizingatia Katiba hiyo hiyo, nadhani ndio maana hakuna mtu aliethubutu kufungua mashitaka hayo mpaka sasa.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amesema hakuna Mtanzania anayemchukia Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ila malalamiko yao dhidi yake ni kutaka kujua ukweli kuhusu mambo yanayomhusu.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana, wakati akitoa maoni kuhusu kauli ya Mkapa aliyotoa mkoani Iringa Jumapili iliyopita, akiwaonya wanasiasa kuacha fitina, chuki, majungu, udini na ukabila kwa hofu kwamba nchi inaweza kuingia katika machafuko.
Mkapa alinukuliwa na vyombo vya habari jana akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Walolesi la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa alipokaribishwa na Askofu Dayosisi hiyo, Dk Owdenburg Mdegella kuwasalimia waumini.
Dk Slaa pia alimtaka Askofu Mdegella kuwaomba radhi Watanzania kwa kitendo chake cha kumtetea na kumsifu Mkapa. Alisema kwa kitendo kama hicho makanisa yanaweza kufika pabaya, kwa kurukia mambo na kusifu watu wakimezea mate michango ya fedha.
"Hatumchukii Mkapa, hakuna mtu anayemchukia, yeye ni rais mstaafu, tunachotaka ni kuwa aache blaablaa za kupotosha hoja. Anachofanya ni kujaribu kupoteza muda na kuwapamba wananchi wasahau hoja ya msingi iliyopo sasa," alisema Dk Slaa.
Dk Slaa ambaye pia ni mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema alisisitiza kuwa, hakuna chuki dhidi ya rais huyo mstaafu zaidi ya kutaka kujua iwapo alifanya biashara alipokuwa Ikulu kama rais wa Tanzania.
"Sisi hatumchukii ila tunataka kujua ukweli, kama alipokuwa Ikulu, akiwa Rais wa taifa hili alifanya biashara na kuuza mali ya Watanzania. Tunataka atueleze kama kampuni iliyonunua Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira ni yake, mkewe, watoto wake na rafiki yake Yona au la?" alihoji Dk Slaa.
Aliongeza kuwa, wananchi wa Tanzania wanataka kusikia kauli ya rais huyo mstaafu, kwa kuwa mgodi wa Kiwira ulikuwa ni mali yao kabla ya kuuzwa.
"Hayo ndiyo tunayotaka kusikia kwa faida ya wananchi, kwani ni haki kujua," alisema Dk Slaa.
Alifafanua kuwa Mkapa anapaswa kuwaambia wananchi kama tuhuma zinazomkabili ni kweli au uongo na kwamba, akithibitisha ni uongo ni vema, lakini ikiwa ni kweli basi sheria ichukue mkondo wake badala ya kuendeleza maneno aliyoyaita blaablaa ambazo hazitamsaidia.
Alisema kuwa siasa za chuki, majungu, fitina, ukabila na udini anaozungumzia Mkapa utaisha pale atakapowaweka wazi Watanzania kuhusu tuhuma zinazomkabi.
"Hizo siasa za chuki, majungu, fitina, ukabila na udini zitaisha akiwaweka wazi Watanzania juu ya umiliki wa Mgodi wa Kiwira. Zaidi ya hayo nashangaa kwa nini azungumzie hayo wakati huu anapokabiliwa na tuhuma za kufanya biashara Ikulu," alisema Dk Slaa.
Akizungumzia hatua ya Askofu Mdegella kumtetea Mkapa na kueleza kuwa anazushiwa uongo na vyombo vya habari, Dk Slaa alisema askofu huyo amewakosea Watanzania na anapaswa kuwaomba radhi.
"Yule Askofu wa Iringa aliyemtetea Mkapa kuwa anazushiwa, lazima awaombe radhi Watanzania, kwa sababu amewakosea," alisema Dk Slaa.
Alifafanua kuwa anayepaswa kujisafisha mwenyewe mbele ya watu aliowaongoza ni Mkapa na si askofu huyo.
Alisema hatua ya askofu huyo na viongozi wengine wa dini hasa makanisa si sahihi, kwani inaendeleza utaratibu wa zamani wa kutomwonya au kumwambia ukweli mkubwa anapokosea.
"Baba kutoambiwa akikosea hiyo ni tabia ya zamani na mbaya, haifai katika ulimwengu wa leo. Tabia ya baba kutosahihishwa ndiyo imetufikisha hapa tulipo," alisema Dk Slaa.
Alisema anawaheshimu viongozi wa dini, lakini akaonya kuwa wasiingie mahali pabaya kwa kusifu watu kwa sababu ya kuhitaji michango makanisani.
"Viongozi wa dini tunawaheshimu, wasiingie mahali pabaya na kusifu watu kwa sababu ya kutaka michango ya harambee. Kama hawajui kitu bora, wanyamaze, vinginevyo watalifikisha kanisa pabaya. Sisi tunawategemea wao wawe safi, lakini hii inatia hofu juu yao," alisema Dk Slaa
Source:Mwananchi
Mkuu Recta, asante. Hapa sasa nimekukubali na darasa limeeleweka. Tafsiri yangu ilikuwa kwa Ben kufanya biashara akiwa Ikulu, niliitafsiri kama ukiukwaji wa maadili ya uongozi. Lakini sasa nakubaliana na wewe. Pia nilitafsiri kinga ya rais, ilihusu utekelezaji wa majukumu yake ya urais kwa mujibu wa katiba, mimi nikahesabu deal ya Kiwira sio sehemu ya majukumu ya rais. Baada ya kunielimisha kuhusu madaraka makubwa aliyonayo rais wetu, sasa nimekubali na nimeelewa kwa nini kuna wakati sauti ziliwahi kupazwa rais apunguziwe madaraka.Haya Mkuu, hii hapa;
46A.-(1)
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
inadaiwa kwamba Rais-
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja
Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
Tafsiri:
Bila kuathiri masharti mengineyo...: Ina maana mashitaka yote ni lazima hazingatie kuwa kuna kinga iliyotangulia hapo juu (katika Ibara ya 46).
hoja itatolewa isipokuwa kama Rais atavunja Katiba au sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.: Maana yake ni kwamba, Rais atakapovunja Katiba ama Maadili ya Viongozi wa Umma, Bunge linaweza kumuondolea kinga ya kushitakiwa. Maadili ya Viongozi wa Umma hayamkatazi Rais au kingozi mwingine yeyote kufanya biashara (sharti la kizuizi cha kufanya biashara liliondolewa kwenye Azimio la Zanzibar). Na vile vile, Katiba hamzuii Rais wala kiongozi mwingine yeyote kufanya biashara. Kwahiyo, kama shutuma ni kufanya biashara, Rais hawezi kuondolewa kinga kwa kuzingatia kifungu hiki.
Kwa kuwa kuna tuhuma nyingine zinazomuhusu Rais mstaafu, kama kununua mgodi wa Makaa ya mawe wa Kiwira, inachotakiwa ni kuangalia taratibu zilizotumika katika kufikia maamuzi ya ununuzi huo. Kama akigundulika kuwa alitumia nguvu zake kama Rais, ama alitumia Rushwa ama alipata umiliki huo kinyume cha sheria, anaweza kufunguliwa mashitaka baada ya kuondolewa kinga. Uchunguzi haujafanywa kufikia uamuzi kama huo. Izingatiwe pia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano anayo mamlaka makubwa sana kisheria na kikatiba. matumizi hayo yakitumiwa kwa namna yoyote haiwezi kuwa uvunjaji wa sheria zilizopo. Kinachotakiwa ni kuangalia namna ya kuweka controls katika uwezo huo mkubwa.
Mambo aliyoyafanya yeye kama Rais ndio yanayohusika, sio WIZI MTUPU alioufanya kama mjasiriamali Benjamini William Mkapa na mkewe, mtoto na wakwe zake
Asha
Mambo aliyoyafanya yeye kama Rais ndio yanayohusika, sio WIZI MTUPU alioufanya kama mjasiriamali Benjamini William Mkapa na mkewe, mtoto na wakwe zake
Asha
hapa mkuu tupo ukurasa mmoja kabisaaaaaaa.hutuhitaji longolongo kamata mkapa piga pingu ,pandisha mahakamani kwa kutumia ofisi na madaraka vibaya..hivi Zambia waliweza wana nini na sisi tushindwe tuna niniMh. Dr.Slaa mkuu kaza uzi hadi huyu jamaa tumfikishe asipotaka..Hayo ni mawazo ya mtu mmoja tu kwani hata Bush ana watu wanaomkubali na ikasemekana kuwa ni chuki dhidi yake.
Pia nakuomba sana usitumie sana jina na imani ya dini kufikisha ujumbe wako kwani kimsingi (Kisiasa) huyo kiongozi wa dini ni raia wa Tanzania..Aliyozungumza huyo mchungaji hayahusiani hata kidogo na mafundisho ya dini yake...Ni wakati wetu sisi kuwaonyesha watu kama hawa kuwa tunaifahamu dini na tunaweza kuchambua mchele toka ktk pumba..