BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,332
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]Dk. Slaa: Baraza la Mawaziri livunjwe
Amshangaa Rais Kikwete kuendelea na ziara nje
na Waandishi wetu, Dodoma na Dar
Tanzania Daima
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelitaka Baraza lote la Mawaziri la Rais Jakaya Kikwete, kujiuzulu kwa madai kuwa limeshindwa kuona dharura ya tatizo la umeme nchini na kulitafutia ufumbuzi.
Pia chama hicho kimemtaka Rais Kikwete kujiuzulu nafasi yake kwa kudharau na kuendelea na ziara yake nchini Afrika ya Kusini wakati akijua fika kwamba Bunge limekwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, anakabiliwa na tuhuma za ufisadi.
Kauli hiyo nzito, imetolewa jana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbroad Slaa, wakati akitoa maoni yake baada ya juzi wabunge wote bila kujali itikadi zao, kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Dk. Slaa alisema Rais Kikwete na mawaziri wake wanatakiwa kupima uzito wa tatizo lilipo na kuchukua hatua za kuwajibika wao wenyewe bila kuambiwa kwani wote wanahusika kuliingiza taifa katika hali hii ya giza totoro.
Dk. Slaa ambaye amepata kuwania urais katika uchaguzi mkuu uliopita kwa tiketi ya CHADEMA, alimshangaa Rais Kikwete kuendelea na ziara hiyo wakati uchumi wa Mtanzania mmojammoja na ule wa taifa ukiporomoka kutokana na tatizo la umeme linalolikabili na kulifedhehesha taifa kwa sasa.
Akitoa mfano wa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, Dk. Slaa alisema amekatiza ziara yake nchini Afrika ya Kusini kutokana na kashfa ya gazeti moja nchini humo kuingilia mawasiliano ya simu za siri za watu.
Rais Kikwete anawezaje kuendelea na ziara wakati nchi iko kwenye matatizo makubwa ya umeme, lakini kibaya zaidi Bunge limekwamisha bajeti ya Wizara nyeti ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anakabiliwa na tuhuma nzito zinazopaswa kuamuliwa na Rais mwenyewe? alihoji Dk. Slaa.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, tafsiri ya kukataliwa kwa bajeti ya wizara hiyo ni ishahara kwamba Waziri Ngeleja na watendaji wake, wameshindwa kazi na hawana uwezo wa kupanga mikakati na utekelezaji wake.
Haiwezekani viongozi walewale wakarudishiwa bajeti ile na kuendelea kuaminika kwa Watanzania katika kuongoza wizara. Kama wameshindwa kuandaa mikakati ya wizara zao, basi wafukuzwe, waje wengine, alisema Dk. Slaa.
Katibu mkuu huyo wa CHADEMA alijigamba kuwa kilichotokea Bungeni ni kielelezo cha kujibu hoja nzito ambazo zimekuwa zikitolewa na kambi ya upinzani kupitia bajeti zao mbadala, kuanzia ile ya Waziri Mkuu Kivuli (Freemani Mbowe), Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi (Zitto Kabwe) na sasa ya Waziri kivuli wa Nishati na Madini, (John Mnyika) ambazo zimeonyesha dhahiri kuwa kilichoandaliwa na wizara za serikali, hakiendani na bajeti yenyewe.
Kuhusu kashfa ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, David Jairo, Dk. Slaa alipendekeza kuwa Bunge liunde kamati maalum kuchunguza tuhuma zinazomkabili za kuandika barua katika taasisi na idara zilizo chini ya wizara hiyo, alizozitaka zichangie sh milioni 50 kila moja kwa ajili ya upitishaji wa bajeti hiyo.
Alisema kamati itakayoundwa, inapaswa kumchunguza Jairo, mawaziri wake na maofisa waandamizi katika wizara hiyo waliohusika kuandaa bajeti kuanzia hatua ya mwanzo hadi mwisho ili kupata mwenendo mzima wa namna bajeti hiyo ilivyoandaliwa.
Kwa hili la Jairo, napata wasiwasi kuwa mchezo huu umekuwa ukifanywa na wabunge wa CCM kwa kushirikiana na mawaziri wao kupitisha bajeti mbalimbali za serikari, huu ni wizi wa mchana kwa Watanzania, alisema Dk. Slaa. Dk. Slaa alilitaka baraza jipya litakaloundwa baada ya mawaziri wote kujiuzulu nafasi zao, kufumua upya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ili iwasilishwe upya bungeni na kuruhusu marekebisho kufanyika ili kulipatia suluhissho la kudumu tatizo la umeme.
Lema ambana Ngeleja, naibu wake
Wakati jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa akitaka Baraza zima la Mawaziri livunjwe, ndani ya Bunge la Muungano, mkoani Dodoma, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), amehoji kwa nini Jairo anayehusishwa na vitendo vya rushwa katika upitishwaji wa bajeti ya wizara hiyo atolewe kafara peke yake wakati Waziri Ngeleja na naibu wake, Adam Malima, wakilifahamu suala hilo?
Alisema mawaziri hao, wanapaswa kuwajibishwa kwa kuwa si rahisi maamuzi hayo kuyatoa Katibu Mkuu pekee bila mawaziri hao kuhusika.
Mheshimiwa Spika, jana wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, anazungumzia ushauri wa wabunge kuhusu tatizo la umeme nchini kabla ya kuomba kusitishwa kwa mjadala wa bajeti hiyo, alisema Katibu Mkuu amejihusisha na vitendo vya rushwa.
Naomba mwongozo wako Mheshimiwa Spika inawezekanaje Katibu Mkuu apitishe suala hilo bila waziri na naibu wake kujua? Je, anayepaswa kuwajibishwa ni Katibu Mkuu peke yake? alihoji Lema. Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema mjadala huo umekwishawekwa pembeni na kwamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda anakwenda kulishughulikia suala hilo kiutawala.
Askofu Kakobe naye atema cheche
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gossiple Bible Fellowship, Zacharia Kakobe, alisema kitendo cha Bunge kuikataa bajeti ya wizara hiyo, kimetokana na laani ya Mungu baada ya viongozi wa wizara hiyo kuamua kuvunja mabango ya kanisa lake, lililoko jijini Dar es Salaam.
Askofu Kakobe alisema Waziri Ngeleja na wenzake wanapaswa kutubu juu ya dhambi hiyo kwa kutumia mabavu kupitisha waya katika kanisa hilo kinyume na matakwa ya Mungu.
Alisema tabia ya baadhi ya watendaji wa wizara hiyo kudaiwa kutoa hongo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini si jambo la kushangaza kwani walifanya hivyo hata wakati wa kuundwa kwa tume iliyochunguza athari watakazopata waumini walio chini ya waya hizo.
Mtakumbuka jinsi Askofu Kakobe alivyopambana katika suala la upitishaji wa waya na hata ile tume iliyoundwa ya chuo kikuu (BICO), aliituhumu waziwazi jinsi ilivyopindisha taarifa ile kutokana na rushwa ili wapitishe waya kanisani, alisema.
Katika ibada moja, Askofu Kakobe alisema wazi kuwa Mungu ndiye Mungu wa mianga na ndiye aliyetoa vipaji kwa wanadamu vya kugundua umeme, hivyo kitendo cha wizara hiyo kujiona ipo juu zaidi ya Mungu, sasa tunaona matunda yake, alisema.
Waumini wa kanisa hilo waliwahi kupiga kambi kanisani hapo na kupeana zamu kwa kupangiana makundi ya kuikabili TANESCO usiku na mchana isipitishe waya za umeme juu ya kanisa lao.
Aidha waliandaa na ujumbe mzito kwa ajili ya shirika hilo la umeme uliowekwa wazi katika fulana maalumu walizovaa zilizokuwa na maandishi ya maonyo na kejeli yasomekayo: TANESCO muogopeni Mungu (mbele) na Baada ya Richmond mmegeukia kanisa (nyuma). Hata hivyo hatua hiyo haikusaidia kwani TANESCO waliamua kupitisha nguzo katika eneo hilo ambapo hadi sasa haijafahamika iwapo kama umeme unapita katika njia hiyo.
Wananchi Dar wachachamaa
Wananchi mbalimbali jijini Dar es Salaam, wametoa maoni tofauti baada ya wabunge kukataa kupitisha bajeti ya ofisi ya Wizara ya Mishati na Madini.
John Paul, mkazi wa Temeke, alisema kitendo cha wabunge kuikataa bajeti hiyo ni kizuri na aliwataka wabunge kuendeleza ukali huo kwa wizara nyingine.
Pia alimtaka Waziri Ngeleja ajiuzulu nyazifa zake kutokana na wizara yake kutotimiza matakwa ya wananchi.
Magreth John wa Ilala, alisema bajeti nyingi za Tanzania ni za kuandaa na sio za utekelezaji kwani mawaziri wengi wameziandaa wakati wakijua hazitekelezeki.
Tatizo la umeme limekuwa pigo kwa nchi yetu na mipango sahihi ya kulimaliza ilibidi ionekane kwenye bajeti lakini badala yake waziri ameweka fedha nyingi kwenye mipango isiyo na faida, alisema Magreth. Wanaharakati wataka JK akatize safari
Wanaharakati wamemtaka Rais Kikwete akatize ziara yake nchini Afrika Kusini aje kukabiliana na tatizo hilo.
Mmoja wa wanaharakati hao, Deus Kibamba, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Maarifa kwa Wananchi, akichangia mada katika sakata hilo kwenye kipindi cha keki ya taifa kinachorushwa na kituo cha Mlimani, juzi, alisema anashangaa kumuona Rais akiendelea na ziara wakati huku nyumbani mambo sio shwari.
Kibamba alisema yote haya yanatokana na tabia ya viongozi waliyojijengea ya kutowajibika hivyo hata suala la kutopitishwa kwa bajeti wanaona ni jambo dogo.
Akitolea mfano, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, wa kukatiza ziara yake katika nchi za Afrika alizopanga kuzitembelea kutokana na mkuu wa jeshi la polisi nchini humo kujiuzulu.
Naye Rais wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Lawrence Mwantima, alisema hii ndiyo kazi hasa wananchi waliyowatuma wabunge na kuongeza kuwa huko nyuma walikuwa hawafanyi haya.
Mimi binafsi sula hili limenifurahisha sana na ndio kazi tunayotaka wabunge watufanyie sio blaablaa na isiishie tu kwa Wizara ya Nishati na Madini hata bajeti nyingine zinazogusa maslahi ya wananchi zinatakiwa zifanywe hivi bila kujali mbunge ametoka chama gani, alisema.
Naye mwandishi wa habari, Tumaini Makene, alisema muda wa wiki tatu uliotolewa kwa ajili ya kuangalia bajeti hiyo upya haitoshi ukizingatia kwamba bajeti huanza kuandaliwa kila inapoisha kupitishwa kwa bajeti ya mwaka husika.
Pia Makene alisema haingii akilini kwamba kutaletwa kitu kipya katika bajeti hiyo ya wiki tatu kwa kuwa watendaji wa kuipitia watakuwa walewale na kushauri kwamba ingeundwa timu maalumu ambayo itaangalia mambo ya msingi katika bajeti hiyo na kupeleka kitu kinachoeleweka bungeni.
Juzi Bunge lilikataa kupitisha bajeti hiyo kutokana na msimamo wa wabunge wa pamoja kati ya wale wa CCM na wa upinzani hasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa bajeti hiyo kwa maelezo kuwa haikuonyesha suluhisho la tatizo la umeme nchini.
Kutokana na wabunge wengi kuikataa bajeti hiyo, Waziri Mkuu Pinda aliliambia Bunge kuwa serikali itaondoa bajeti hiyo na kuifanyia marekebisho na kuiwasilisha upya wiki tatu zijazo.
Pia uamuzi huo wa Bunge umekuja baada ya mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo, kusoma bungeni barua ya katibu mkuu huyo iliyozitaka taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo sh milioni 50 kila moja kwa nia kulainisha wadau katika kupitisha bajeti hiyo.