Dk. Slaa awaangukia walimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa awaangukia walimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kupelwa, Aug 25, 2012.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  • AWAAMBIA ADUI WAO NI RAIS KIKWETE, CCM


  na Abdalla Khamis na Ghisa Abby

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewasihi walimu nchi kutomaliza hasira zao za kutolipwa vizuri kwa kutowapa elimu bora wanafunzi wao.

  Dk. Slaa alisema adui mkubwa wa walimu ni Rais Jakaya Kikwete, CCM na serikali yao ambao mara kwa mara wamekuwa wakiongeza mishahara, marupurupu na posho kwa wabunge lakini hawawajali walimu.

  Kauli hiyo aliitoa juzi kwenye mikutano ya hadhara kwenye vijiji na kata mbalimbali za Jimbo la Morogoro Kusini, akiwataka wafanyakazi wasihamishie hasira zao kwa wananchi na badala yake hasira hizo wazielekeze kwenye serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

  "Juzi nimesoma kwenye mtandao, naona walimu wanatumiana meseji, ujumbe mfupi kwenye simu zao na kama kweli wataufanyia kazi, maskini watoto wetu hawa walioko shuleni na taifa lote tumekwisha," alisema.

  Alisema ujumbe huo unaowaelekeza walimu kuwafundisha uongo wanafunzi, jambo ambalo linatoa ishara kuwa wana kinyongo na serikali inayopuuza madai ya nyongeza za mishahara, posho na stahiki nyinginezo.

  "Chonde chonde walimu wangu naombeni hasira zenu msizihamishie kwa watoto wangu hawa wasiokuwa na kosa lolote, kila mtu mwenye akili timamu anatambua madai yenu ni ya ni ya msingi, mnapaswa mjue adui yenu ni Kikwete na serikali yake.

  "Ikabeni koo hiyo serikali lakini timizeni wajibu wenu kwa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora," alisema.

  Alisema kitendo cha serikali kuongeza mishahara ya wabunge na kufikia milioni 11 huku ikishindwa kutatua madai ya msingi ya kada nyingine kinaonesha inavyowatumia wananchi wake kama makarai ya ujenzi.

  Dk. Slaa alisema kada nyingine za utumishi wa umma wakiwamo askari na madaktari zinafanya kazi katika mazingira magumu na wanadharauliwa na serikali licha ya kuwa na mchango mkubwa kwa taifa.

  alibainisha kuwa serikali inavyoendelea kuidhinisha marupurupu na mishahara ya wabunge huku ikiendelea kukandamiza masilahi ya makundi mengine ndiyo chanzo kikubwa cha wananchi kupunguza ari ya kujiletea maendeleo.

  Katibu Morogoro ajiuzulu

  Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro, Abel Luanda, amejiuzulu nafasi yake na kuahidi kuhamia CCM ndani ya saa 48 zijazo. Luanda alisema Agosti 21 mwaka huu alimkabidhi barua ya kujiuzulu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, yenye kumbukumbu namba AEL/KCDM/KINK/MC/O12.

  Katika barua yake hiyo Luanda alitaja sababu zilizomfanya avue ‘gwanda' kuwa ni kupisha upepo mbaya wa kisiasa ndani ya CHADEMA kuanzia ngazi ya mkoa hadi taifa, kukosa ushirikiano na Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa pamoja na kile alichokiita dharau kutoka kwa viongozi wa chama hicho taifa.

  Sababu nyingine ni kupisha alichokiita agenda ya siri aliyodai imejificha katika mchakato mzima wa ziara ya CHADEMA mkoani humo kuwa inalenga kuwaondoa viongozi ndani ya wilaya na mkoa wanaodaiwa kukubalika kwa wananchi.

  Wakati Luanda akieleza sababu hizo, taarifa za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata zinaeleza kuwa katibu huyo alishindwa kusimamia chama mkoani humo, hali iliyomlazimisha Dk. Slaa kusimamia chaguzi mbalimbali kwa lengo la kuimarisha chama.

  Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, amethibitisha chama kupokea barua ya kujiuzulu kwa Luanda na kueleza kuwa kilichomfanya ajiuzulu ni hofu ya kujulikana kuwa alikuwa hakijengi chama katika mkoa, hasa katika Wilaya yake ya Morogoro Vijijini.

  "Huyu bwana mbali ya kuwa katibu wa mkoa pia alikuwa ndiye Mwenyekiti wa Wilaya ya Morogoro Vijijini, yenye majimbo mawili, kwa sababu ya kushindwa kazi na wajibu wake amesababisha majimbo yote mawili hayana akaunti benki kwa muda wote ambao amekaa madarakani, hivyo yameshindwa kupata mgawo wa ruzuku kutoka makao makuu kama inavyotakiwa," alisema.

  Makene alieleza kuwa hata taarifa ya ukaguzi iliyokuwa ikifanywa na timu ya chama hicho mkoani Morogoro imeshindwa kupata taarifa muhimu kutokana na katibu huyo kushindwa kujua majukumu yake.
   
 2. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Good.dr slaa
   
 3. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mzigo ndani ya chama
   
 4. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,589
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ni kweli watoto wetu hawana kosa ila wazazi na watanzania kwa ujumla ndio wenye makosa kuichagua ccm isiyowajali watoto wetu.
   
 5. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,773
  Trophy Points: 280
  Huo ndio ukweli wasioujua baadhi ya watz kuwa magumu ya nchi hii yanasababiswa na ccm
   
 6. hendeboy

  hendeboy JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Cdm angalieni kama kuna hasara iliyotona na katibu huyo ili sheria ichukue mkondo wake
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Inasikitisha sana kwa watoto wetu wanaosoma St Kayumba.
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Funguka zaidi!!!! nani?
   
 9. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Huyo katibu anawafaa sana ccm na asione kama yuko peke yake kuna wengi sana wa aina yake watamfuata kabla hatujaingia ikulu
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Alitoka kwa mavumbi amerudi kwa mavumbi
   
 11. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Safi sana bora kakiri japo viceverser kuwa agenda ya CDM nikuondoa viongozi wabovu viva CDM.....na achunguzwe Kama kala Ada za wanachama
   
 12. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si Kama huyo katibu aliyeshindwa Hata kufungua account ya chama ndio mizigo Iyo.
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sa docta utawalipa ngapi walimu ??? Ikiwa umekiri serikali ya CCM inawalipa wabunge milioni kuminamoja ,kuna polisi kuna jeshi na sehemu kibao za serikali ambazo mishahara haifiki hata nusu ya hao wabunge.

  Pindipo 2015 CDM ikiukwaa utawala wa Tanzania ,Je Serikali yako Mheshimiwa Slaa inatuambiaje na imejipanga vipi ??? Je itashusha mishahara ya wabunge au itawaongeza wengine walingane au kukaribiana na wabunge
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Bora Ameondoka na ahamie mwabepande mapema!

  Adui wa watz ni ccm!
   
 15. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hilo ndilo neno. Lakini walimu hawa hawa wakija kupewa sh5000 wakati wa uchaguzi wanawatetea hao hao nyinyiem.
  Hao watoto ni wetu ikiwa ni pamoja na wa walimu, kama mnafikiri mnamkomoa kikwete imekula kwetu na ufinyu wenu. Mnaandaa kuja kutawaliwa na watoto wa akina kikwete wanaofundishwa na kusoma bila stress kwa kodi zetu.
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,493
  Trophy Points: 280
  Kuanzia awamu ijayo mambo yatakuwa safi tu.
   
 17. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuache utani walimu ni taa katika jamii nashangaa sasa wameamua kuwa giza!! Kama kweli ni taa basi waelewe adui wao ni nani na wamkabili siyo kuwamalizia watoto wasio na hatia hasira zao. Kwa kufanya hivyo wana tofauti gani na "magamba" ambayo hayajali jamii?
   
 18. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,309
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa hapo umenena kweli.
   
 19. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Safi sana Dr slaa 2015 unaingia magogoni bila vipingamizi.
   
 20. l

  lonka Member

  #20
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  siyo busara hata kidogo kuwafundisha watoto uwongo cha msingi nikupambana na ccm hadi kieleweke
   
Loading...