Ni jambo lililo wazi kabisa kwamba Dr.Slaa anaweza kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015.Kinachotakiwa sasa hivi ni CHADEMA kuhakikisha kuwa wanaweka au TUNAWEKA wagombea wanaokubalika katika nafasi zote za ubunge.
Pia Slaa aendeleze nguvu zake bungeni na kuweka mikakati mizito kipindi hiki 2010-2015. Pamoja na umaarufu wa CHADEMA wa sasa,bdo tunahitaji pyramid-like structure katika kujiandaa kukabiliana Vilivyo na CCM mwaka 2015.ni lazima tuahkikishe tunajikita vijijini kwa nguvu zote na kutoa alternative solution kwa matataizo yanayotokana na uongozi wa kata hadi ngazi za mitaa.CHADEMA ihakikishe kuwa viongozi hata kama ni wa mtaa,wana uwezo au wawezeshwe kuonyesha tofauti na wananchi waone ni kwa nini CHADEMA ni mbadala.
Kwa BAVICHA.Hili ni Baraza la vijana la CHADEMA,ni sawa na UVCCM...simaanishi kimtazamo au kitabia,kimaadili nk.Hili ni Baraza ambalo kwa kweli kama CHADEMA tukiweka mikakati,hili baraza litasaaidia kuunganisha vijana wote Tanzania na linaweza kuwa powerfull sana ktk kujenga ushawishi kwa vijana.Hili ni baraza ambalo linatakiwa kujitangaza na kujitandaza nchi nzima.Asilimia zaidi ya 65% ya population ya Tanzania ni vijana.Kwa hiyo kama tunataka kujenga ushawishi ni lazima tuwe karibu na vijana na tujenge mtandao,tuhakikishe tunawashawishi kujiandikisha na kupiga kura.Vijana walio na miaka 15-17 saba mwaka huu ni wengi,hao watakuwa wapiga kura wa mwaka 2015.
Pia BAVICHA ni lazima ijitahidi kutumia mbinu kali na kuhakikisha wanajitahidi kuingiza puppet governments ktk vyuo vikuu vyote vya umma ambao watakua wana-pose kama watu ambao wako above partisan politics.viongozi wa hizo serikali ni lazima wawe na ushawishi mkubwa kwa wanafunzi
Pia BAVICHA lazima waanzishe kitengo au idara maalumu ya kushughulikia ajend za wamachinga,vijana jobless nk ili kujenga matumaini na kutafuta uungwaji mkono.Zaidi ya yote,BAVICHA ihakikishe inajitafutia vyanzo vya mapato na vitega uchumi ,raslimali ambazo zitazidi kuwapa nguvu ya kupambana na UVCCM
Pia,Wabunge wa CHADEMA wajitahidi bungeni,wajenge hoja zaenye mshiko na kusaidiana kutafuta resources kwa ajili ya uwekezaji majimboni mwao.
Mwaka 2015,CCM kutakua na jnga kubwa la uongozi na hasa kuanzia mpasuko utokanao na uchaguzi huu hadi 2015,kuna kazi.Lazima tujitahidi kuvuna katika huu msiba.Sina huruma nao hata kidogo.
Pia,kama CCJ watapata usajili wa kudumu,basi CHADEMA iangalie jinsi ya kufanya nao strategic alliance pamoja na CUF.Nina uhakika ikifika mwaka 2015,Dr.Slaa au mgombea wa CHADEMA akisimama huku run mate wake akiwa mtu wa CCJ au CUF vs mgombea wa CCM,basi upinzani utaingia madarakani.
Sasa hivi viti vingi vitakavyopatikana bungeni vitasaidia kuanzisha vuguvugu la kudai Katiba mpya.Msukumo wa hii movement utaleta radical Reform.Nje ya bunge CHADEMA itumie wanaharakati,wanahabari,na powerfull department BAVICHA kudai haki kwa kutumia new approach kama maandamano ya amani na migomo mizito yenye misimamo bila kujali vitisho.Bado nitaendelea