Dk Slaa amkumbuka Sitta

Dk Slaa amkumbuka Sitta

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

KITAIFA
Posted Jumanne,Marchi12 2013 saa 20:36 PM
KWA UFUPI

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu wabunge wa chama hicho kutakiwa kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema Spika Makinda amekuwa akipindisha kanuni na ndiyo maana kumekuwa hakuna utulivu bungeni.

Mvutano uliopo hivi sasa kati ya Chadema na Bunge ulianza Februari 4 katika kikao cha Bunge mjini Dodoma baada ya wabunge wa Chadema kupinga msimamo wa kiti cha Spika wakieleza unapendelea

Boniface Meena na Mussa Juma, Mwananchi

Kutokana na mvutano ambao umekuwapo mara kwa mara kati ya Chadema na Spika wa Bunge, Anne Makinda, chama hicho kimemkumbuka aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Samuel Sitta kikieleza kuwa alikuwa hapindishi sheria na kanuni za Bunge na ndiyo maana lilikuwa limetulia.

"Spika Sitta aliyekuwepo kabla ya Makinda alikuwa hapindishi sheria na alikuwa anajirekebisha pale anapokosea na tulikuwa tukishauriana kwamba asijihusishe na mambo ya vyama," alisema Dk Slaa.

Alisema Sitta, ambaye hivi sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alikuwa hafuati mambo ya vyama kwa kuwa alitakiwa kuwa ni mtu ambaye hapendelei upande wowote. Sitta, ambaye alikuwa Spika kuanzia mwaka 2005-2010, alikuwa anajinadi kwa kuendesha Bunge kwa spidi na viwango.

"Makinda aachane na ushabiki wa CCM kwani anajua kabisa kanuni ya nane inamtaka Spika asifungamane na upande wowote hivyo aache kufanya hivyo," alisema Dk Slaa.

Alisema ni muhimu Spika akawaeleza kimaandishi amepata wapi mamlaka ya kuruhusu kamati iendelee wakati zote zilivunjika rasmi katika Bunge lililopita.
"Spika kama hajui kanuni aende shule kujifunza kuliko kututia aibu, wanasheria, wabunge wamsaidie ili aweze kuelewa."

Dk Slaa alisema katika mabunge ya kidemokrasia, kupongeza ni jambo halali na kuzomea pia ni jambo halali hivyo kitendo cha wabunge wao kuzomea ni sawa kwa kuwa ni njia yao ya kufikisha ujumbe. Akizungumzia suala la wabunge wake kuhojiwa na kamati hiyo ya Bunge, alisema hawatakwenda kuhojiwa na kamati hiyo na kama Bunge litaamua kuwafukuza lifanye hivyo ili wananchi waelewe.

"Hawawezi kwenda kuhojiwa na kamati ambayo haipo kisheria, nilipokuwepo bungeni nilishiriki kuandaa kanuni hizi za Bunge, Spika hana mamlaka anayojipa ya kuongeza muda wa kamati, hivyo aache kulidhoofisha Bunge na badala yake alisaidie," alisema Dk Slaa.

Akizungumzia suala hilo, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema anashangazwa na Naibu Spika, Job Ndugai kusema kuwa kuna kamati ambazo huwa zinaendelea wakati nyingine zinapokuwa zimemaliza muda wake.

Lema aitisha maandamano

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, ametangaza kuandaa maandamano makubwa yatakayoshirikisha wanawake na watoto katika Jiji la Arusha ili kushinikiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA) kuwasambazia maji.

Akizungumza jana, Lema alisema ameamua kuandaa maandamano hayo ya kudai maji kwani kwa zaidi ya miezi sita sasa asilimia 70 ya wakazi wa Jiji la Arusha hawapati maji safi.

"Nimewaandikia barua AUWSA wiki mbili sasa nikiwataka wanipe mipango yao ya muda mfupi na mrefu ya kuondoa tatizo la maji Arusha, kwani mimi kama mbunge ninaweza kushirikiana nao kupunguza tatizo hili, lakini hawajajibu sasa tutawashinikiza kwa nguvu wa umma," alisema Lema.

tunakokwenda spika atatakiwa kuwa mwanasheria pia, au mtaalam wa sheria.
 
maranyingi huwa najiuliza hawa watu wanaofanya kazi zao kwa kukiuka uheredi kuisadia ccm,nakutupa ugumu wakuiondoa,wataficha wapi nyuso zao siku shuka la ukombozi likifunika anga ya nchi hii.
 
SItta nae alikubali kutumiwa na CDM japo yeye CCM
So wakamuondoa ameletwa mama anafanya haki sana ila mnataka kulifanya bunge sawa na lile la ukraine

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
anachefua yule mama. Huku k'nyama kaziba njia kwa sababu ya uwepo wa nyuma yake. 2015 lazima tuwang'oe makoko hawa.
 
anachefua yule mama. Huku k'nyama kaziba njia kwa sababu ya uwepo wa nyumba yake. 2015 lazima tuwang'oe makoko hawa.
 
Hapa spika makinda ni KIHIYO wa sheria..'eti tunafuata kanuni' Makinda kanuni hizo unazijua?
 
bunge lilikofikia sasa ni dhahili livunjwe kabisa tubaki bila mhimili huu make hautusaidii kabisa.
 
tunakokwenda spika atatakiwa kuwa mwanasheria pia, au mtaalam wa sheria.

Mkuu kwa ninavyoona huyu mama siyo kwamba hajui sheria kwa muda wote aliokaa bunge issue ni kuwatetea waliomweka madarakani kwa kupindua hivyo vifungu. Kumbuka ile nafasi kataftiwa kwa maslahi ya kuondoa usawa bungeni wakidhani usawa uliowekwa na spika aliyetangulia ulikidhoofisha ccm
 
Rais mtarajiwa Dr.W.P.Slaa umenena na umesikika.

Ukweli ni kwamba kwa sasa Tanzania haina Spika wa Bunge wala Naibu wake.
Bi Mkora Anne Makinda na Job Ndugai ni JANGA ndani ya Bunge letu. Mimi nashauri ule mpango wa kupiga KURA ya kutokuwa na imani na Spika na Naibu wake ifanyike mara tu Bunge litakapoanza kikao kijacho.

Watanzania tumechoka,tumechoka.
 
maranyingi huwa najiuliza hawa watu wanaofanya kazi zao kwa kukiuka uheredi kuisadia ccm,nakutupa ugumu wakuiondoa,wataficha wapi nyuso zao siku shuka la ukombozi likifunika anga ya nchi hii.

watakuja kwa kujitetea tulijua tu chama flani kwa uongozi wao imara wangeichukua nchi na kumwaga sifa kibao
 
SItta nae alikubali kutumiwa na CDM japo yeye CCM
So wakamuondoa ameletwa mama anafanya haki sana ila mnataka kulifanya bunge sawa na lile la ukraine

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

umeangalia kigezo gani kusema bi kiroboto anatenda haki? Maana kuna wakati bunge linamshinda kwa kugeuza vifungu anaamua kukimbia na kumwachia ndungai ambae nae baadae hakufua dafu
 
Kwani hao wabunge wanaohojiwa ni CDM peke yake? Kama ni hivyo kweli bora wagome 7bu kuna maccm yalitoa kauli chafu dhidi ya upinzani kitu ambacho spika alikinyamazia
 
SItta nae alikubali kutumiwa na CDM japo yeye CCM
So wakamuondoa ameletwa mama anafanya haki sana ila mnataka kulifanya bunge sawa na lile la ukraine

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Upenzi,ushabiki wa ki-vyama iskufanya ukapofuka,hakuna speker katika historia ya Tanzania ambaye ameliendesha bonge kwa viwango na uhuru mkubwa kama Mh Sitta.
 
tunakokwenda spika atatakiwa kuwa mwanasheria pia, au mtaalam wa sheria.

Anne Makinda ni Mzuri sana tatizo wasira, lukuvi na werema ndio wanaompoteza kabisa katika mahamuzi yake na usimamia yao.
 
maranyingi huwa najiuliza hawa watu wanaofanya kazi zao kwa kukiuka uheredi kuisadia ccm,nakutupa ugumu wakuiondoa,wataficha wapi nyuso zao siku shuka la ukombozi likifunika anga ya nchi hii.

Uheredi ndo mdudu gani mkuu?
 
KITAIFA
Posted Jumanne,Marchi12 2013 saa 20:36 PM
KWA UFUPI

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu wabunge wa chama hicho kutakiwa kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema Spika Makinda amekuwa akipindisha kanuni na ndiyo maana kumekuwa hakuna utulivu bungeni.

Mvutano uliopo hivi sasa kati ya Chadema na Bunge ulianza Februari 4 katika kikao cha Bunge mjini Dodoma baada ya wabunge wa Chadema kupinga msimamo wa kiti cha Spika wakieleza unapendelea

Boniface Meena na Mussa Juma, Mwananchi

Kutokana na mvutano ambao umekuwapo mara kwa mara kati ya Chadema na Spika wa Bunge, Anne Makinda, chama hicho kimemkumbuka aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Samuel Sitta kikieleza kuwa alikuwa hapindishi sheria na kanuni za Bunge na ndiyo maana lilikuwa limetulia.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu wabunge wa chama hicho kutakiwa kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema Spika Makinda amekuwa akipindisha kanuni na ndiyo maana kumekuwa hakuna utulivu bungeni.

“Spika Sitta aliyekuwepo kabla ya Makinda alikuwa hapindishi sheria na alikuwa anajirekebisha pale anapokosea na tulikuwa tukishauriana kwamba asijihusishe na mambo ya vyama,” alisema Dk Slaa.

Alisema Sitta, ambaye hivi sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alikuwa hafuati mambo ya vyama kwa kuwa alitakiwa kuwa ni mtu ambaye hapendelei upande wowote. Sitta, ambaye alikuwa Spika kuanzia mwaka 2005-2010, alikuwa anajinadi kwa kuendesha Bunge kwa spidi na viwango.

“Makinda aachane na ushabiki wa CCM kwani anajua kabisa kanuni ya nane inamtaka Spika asifungamane na upande wowote hivyo aache kufanya hivyo,” alisema Dk Slaa.

Alisema ni muhimu Spika akawaeleza kimaandishi amepata wapi mamlaka ya kuruhusu kamati iendelee wakati zote zilivunjika rasmi katika Bunge lililopita.
“Spika kama hajui kanuni aende shule kujifunza kuliko kututia aibu, wanasheria, wabunge wamsaidie ili aweze kuelewa.”

Dk Slaa alisema katika mabunge ya kidemokrasia, kupongeza ni jambo halali na kuzomea pia ni jambo halali hivyo kitendo cha wabunge wao kuzomea ni sawa kwa kuwa ni njia yao ya kufikisha ujumbe. Akizungumzia suala la wabunge wake kuhojiwa na kamati hiyo ya Bunge, alisema hawatakwenda kuhojiwa na kamati hiyo na kama Bunge litaamua kuwafukuza lifanye hivyo ili wananchi waelewe.

“Hawawezi kwenda kuhojiwa na kamati ambayo haipo kisheria, nilipokuwepo bungeni nilishiriki kuandaa kanuni hizi za Bunge, Spika hana mamlaka anayojipa ya kuongeza muda wa kamati, hivyo aache kulidhoofisha Bunge na badala yake alisaidie,” alisema Dk Slaa.

Akizungumzia suala hilo, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema anashangazwa na Naibu Spika, Job Ndugai kusema kuwa kuna kamati ambazo huwa zinaendelea wakati nyingine zinapokuwa zimemaliza muda wake.

Lema aitisha maandamano

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, ametangaza kuandaa maandamano makubwa yatakayoshirikisha wanawake na watoto katika Jiji la Arusha ili kushinikiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA) kuwasambazia maji.

Akizungumza jana, Lema alisema ameamua kuandaa maandamano hayo ya kudai maji kwani kwa zaidi ya miezi sita sasa asilimia 70 ya wakazi wa Jiji la Arusha hawapati maji safi.

“Nimewaandikia barua AUWSA wiki mbili sasa nikiwataka wanipe mipango yao ya muda mfupi na mrefu ya kuondoa tatizo la maji Arusha, kwani mimi kama mbunge ninaweza kushirikiana nao kupunguza tatizo hili, lakini hawajajibu sasa tutawashinikiza kwa nguvu wa umma,” alisema Lema.

Pamoja nawe sana kamanda..
 
SItta nae alikubali kutumiwa na CDM japo yeye CCM
So wakamuondoa ameletwa mama anafanya haki sana ila mnataka kulifanya bunge sawa na lile la ukraine

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
kwani bunge la ukraine na la tanzania lipi lina tija?
 
Back
Top Bottom