Dk. Slaa Ajibu Mapigo ya CCM

mwissho wa ubaya aibu, imefika wakati lazima ccm wajue kuwa mwisho wao umefika, kwani hakuna mwanzo uso na mwisho, kazeni kamba cdm bado kidogo tu watangoka, tayari washaregea wanaanza kupayuka na kuongea mambo ambayo hayapo. big up sanaaaaa.
 
narudia tenna kusema, slaa dr slaaaaaaaaaa hawez kukamatwaaaaa na siroakali hiiiii ya kifisadi.

laslaa faya kazi yako ya kuamsha watznznania kwwnye usingizi wa pono.

nasema tena akunan qwa kumkataw slaa dr wilbroads pita

s*e*z type
 
Mh. Raisi,

Salaam.

Nasikitika sana ukikosea na wengine wote wanakosea. Siamini wanakosea kwa bahati mbaya ila ni kwa sababu umewasabisha wakosee.

Umeongelea maandamano ya Chadema kwenye hotuba yako. Wengine wamekurupuka wanazungumza pia. Wanalaani.

Kama umeshasema nilitegemea kitu cha kufuata ni utekelezaji wa amri yako (najua hukutoa) au maagizo yako. Sasa wote mnatoa kauli, mnatuchosha kutuambia ambayo sisi tunayajua.

Ni nani amekwambia kuna mtu anapenda kutembea juani kilomita 10? Je Mh. Raisi unafikiri watu wanapenda kutumia mafuta yao ya pikipiki na kuacha vibarua vyao watembee tu barabarani?

Mnawaita wazururaji, je umesikia Bank au mwajiri yeyote amelalamika mfanyakazi ameacha desk akaenda kwenye maandamano? Hujiulizi kwanini wanazurura?

Mheshimiwa Raisi, na hao waliofeli kidato cha nne kwa maelfu wataacha kuzurura? Au unafikiri wameenda wapi baada ya kufeli? Yakitokea maandamano wakae nyumbani kisa amani na utulivu?

Mnatoa kauli za kejeli badala ya kujibu hoja na kuongoza nchi. Waziri Mkuu anapotoa kauli 'hao chadema wenyewe waoga wakipigwa mabomu wanakimbia' anaitakia hii nchi amani? Kuanzia sasa polisi wakipiga mabomu hatutakimbia, tutajibu kwa mabomu ya petroli si ndicho anachotaka?

Anayechochea hapa ni nani? Anayekejeli wananchi wakikimbia au anayekimbia? Kwa sababu anataka watu wasikimbie basi asubiri aone. Wapige tena mabomu.

Mh. Raisi, umezungukwa na watu wasiofikiri wala hawana msaada kwako. Mbona hawakuongea kabla hujaongea wewe? Wassira, Vuai nk walikuwa wapi? Tendwa alikuwa hajui kuhusu hili mpaka sasa? Acheni kutuona wajinga. Mkituheshimu tutawaheshimu.

Mnataka kusujudiwa na kuogopwa. Hapana. Nchi ina matatizo na matatizo ni yaliyopo sasa hivi sio historia ya 'oooh tumeitoa nchi mbali'. Mbali wapi?

Mheshimiwa Raisi, hao wakina Wassira, Tendwa na Jumuiya ya Wazazi nk ni wanafiki na hawana maana. Hawakwambii ukweli na ukikosea wanazidi kukupoteza.

Mh. Raisi, waandamanaji ni wananchi. Ni watanzania. Wanaipenda amani yao. Wao ndio sababu ya amani na utulivu. Sio ccm wala chadema.

Wananchi ndio wanailinda amani hiyo. Sio ccm wala chadema.

Wanapokimbia ili amani na utulivu viendelee Waziri Mkuu anawaita waoga. Take it from me, hawatakimbia tena halafu tuone.

Mh. Raisi, tafadhali waongoze viongozi wako. Wafundishe adabu na heshima kwa wananchi wa taifa hili. Dharau na kejeli zao zitaleta majuto.

Mh. Raisi, jitahidi kutatua kero za wananchi. Yote yanayozungumzwa yapo. Ndio maana wananchi wanaandamana. Hawalazimishwi kushiriki. Ni shida zao ndio zinawafanya waamue kueleza kilicho moyoni mwao.

Mh. Raisi, nashindwa kukuelewa. Wananchi wanakwambia hatuna kazi, maisha magumu, tunafeli mitihani, nchi yetu inaibiwa nk wewe unasema wanatishia amani!! Kweli umeshindwa kuona kwamba kinachotishia amani ni hizo sababu na sio wananchi wala chadema?

Mh. Raisi, narudia kusema, wanaoandamana ni wananchi. Sio chadema. Wengi wa waandamanaji hao walikupigia kura 2005 na 2010. Tafadhali wewe na viongozi wako msiwadharau.

Kama waliwachagua wakiwa wanazurura basi msiwatupe baada ya kuwachagua kisa eti ni wazururaji.

Chadema ni waandaaji. Washiriki ni wananchi, watanzania.

Huna wa kukwambia, ukikosea wewe wamekosea wote. Hilo ni tatizo.
 
Nyie bwana kwa mikwara, Slaa akikamatwa mtabaki mnaongea kwenye keyboard tu siku tatu nne na baada ya hapo mtasahau wala hamtaifanya kitu chochote serikali.

Wakoloni wa ccm hawaogopi kumtia slaa kolokoloni kwa sababu za wananchi waoga kama sie, wao wanachoogopa ni kupoteza reputation yao na madili yao kimataifa.
Slaa akiingia kwenye 18 zao ambayo ktk darubaini ya kimataifa itaonekana OK , na watamtia na uhakika hamtafanya lolotee wapiga mluzi.
 
Mafisadi wa EPA, Rada, Kagoda, Ndege ya Rais, helicopters za jeshi, Meremeta, Richmond/Dowans, mikataba feki ya madini, Wezi wa Kiwira Coal Mining wote hawa wameshindwa kuwakamata! ila sasa hivi wanataka kuwakamata watetezi wa maslahi ya Tanzania na Watanzania!
 
Mbona Pro. Lipumba walishawahi kumuweka Ukonga kinachowashinda nini kwa Dr. Slaa na Mbowe! Tena basi sheria inamruhusu rais kumuweka mtu yoyote kizuizini kwa muda anaoutaka, mbona hatumii fursa hii kwa makosa ya wazi ambayo ni uchochezi, uhaini n.k
CCM wanajua kabisa wanachokifanya akina Dr. Slaa na wenzake ni haki yao lakini indirect ni kama kuwaambia wapunguze. Serikali ikishindwa nguvu ya dola itatumika, huu ni uoga wa maamuzi.
 
Akamatwe kwa kosa lipi? labda la kupoka mke wa mtu? na hilo kisha lipanguwa kwa kulipa ugoni!
 
moto wa mageuzi umeshawaka hakuna anayeweza kuuzima olewake atakaejaribu kuuzima atajuta kwanini alizaliwa dk kaza buti vijana tuko pamoja Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Chadema
 

Nadhani watakuwa wameupata ushauri huu... na waufanyie kazi>>>Kwani, wanawindwa sana!!!
 

Ndiyo maneno tunayopaswa kuyasikia kutoka kwa makamanda. Aluta continuuuuuuaaaaaa!!
 

Endelea kuwaza kama mlevi wa mataputapu! Unadhani dunia ya jana ndiyo ya leo. Wamkamate Dr. Sla waone cha moto. Unadhani kwa nini hawamkamati pamoja na kuwalipua mara kwa mara?? Miaka mitano yote ya uongozi wa serikali yako ya kifisadi mmekuwa mkishughulikia kashfa nzito anazolipua Dr. Slaa. Mtake msitake Dr. Slaa hawezi kukamatwa kipuuzipuuzi tu. Sahauni kabisa!!
 

mbona unaandika kwa woga...si uweke majina kamili. RS ndo nani?
 
Chadema wa Jf mtachoga saaaaana. Lakini nchi itaongozwa na wengine. Si slaa wala Mbowe. Kelele zote hizi ni kwa vile walikosa kura. Kaza buti wana Jf kwa kupiga debe humu ukichanganya na kelele za slaa mtakuwa matajiri wote. Bravo kwa matusi wanachadema humu jf na Slaa kwenye maandamano. Keep it up mwisho wa siku wananchi watawaelewa na kufanya maamuzi. Kwa sisi ambao tayari tunaona majibu yenu humu jf hayana tofauti na mikutano ya Chadema(kwa matusi) ni dalili tosha kabisa kuwa Milembe inawasubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…