Dk Slaa Aitesa CCM Manyara! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa Aitesa CCM Manyara!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Buchanan, Sep 30, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Joseph Lyimo, Simanjiro

  MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa kuwa gumzo kwa wakazi wa Mkoa wa Manyara imezidi kuwapa maumivu makali viongozi wa CCM mkoani humo na kusababisha kufanya vikao vya ndani hadi saa 7:00 usiku.

  Viongozi hao wa CCM Mkoa wa Manyara wakiongozwa na katibu wake, Avelin Mushi, Katibu wa Wazazi Mkoa, George Kijaji, Katibu wa UWT Mkoa,Grace Maholelo na wabunge wateule wa viti maalumu mkoa huo, Dorah Mushi na Martha Umbulla na mgombea ubunge katika Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka wanakutana muda huo, kujadili hilo ni jinsi gani watakabiliana na Chadema.

  Wengine wanaokutana katika mkutano huo ni kamati ya siasa ya Wilaya ya Simanjiro,wagombea udiwani wa CCM na wajumbe wa Halmashauri ya CCM katika Kata ya Mererani.

  Katika vikao hivyo vilivyofanyika juzi kuanzia saa 11:00 jioni hadi saa 7:00 usiku kwenye ukumbi wa Manyara Inn uliopo mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro, pia ulihudhuriwa na mkuu wa wilaya hiyo Khalid Mandia ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM wilayani humo.

  Mmoja kati ya wajumbe wa vikao hivyo ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa vile siyo msemaji wa chama hicho, alisema kuwa upepo wa kisiasa siyo mzuri mkoani Manyara kwa CCM, hivyo uongozi wa mkoa huo umejadili hilo ili kunusuru hali hiyo.

  Alisema nyota ya kisiasa mkoani Manyara kwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Slaa ipo juu, hivyo wanapanga mikakati mbalimbali ya kukinusuru chama hicho.

  Alidai kuwa kuna baadhi ya wanachama wa CCM mkoani humo walipandikizwa mbegu chafu kwamba wawachague diwani na mbunge wa CCM, lakini kura ya urais wampe Dk Slaa, hivyo kutokana na hilo uongozi wa mkoa unafanya vikao hivyo, ili kunusuru hali hiyo.

  Katibu wa CCM mkoani Manyara, Avelin Mushi alisema kura za wakazi wa mkoa huo, hazitatosha kumfanya Dk Slaa kuwa rais wa Tanzania kwani wananchi wengi wana imani kubwa na Rais Jakaya Kikwete.

  "Nimekutana na kamati ya siasa ya wilaya,wagombea udiwani na wajumbe wa Halmashauri ya CCM Kata ya Mererani ili kujadili na kupanga mikakati ya ushindi kwenye uchaguzi mkuu," alisema Mushi.

  Katibu huyo aliwaasa wakazi wa mkoa huo kutopoteza kura zao kwa kutambua mazuri yaliyofanywa na chama hicho kwa kumpa kura nyingi za ndiyo mgombea urais wa CCM.


  Japokuwa CCM mkoani Manyara imefanikiwa kumpitisha Ole Sendeka bila kupingwa kwenye ubunge Simanjiro na madiwani 24, wamepita bila kupingwa,bado inawakati mgumu kwenye majimbo mengine matano, kwa kuwa mapokezi ya mgombea urais wa chama hicho, hayakuwa mazuri na kwamba alizomewa alipokuwa akijinadi wilayani Mbulu.


  Source: MWANANCHI.
   
 2. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  the time for change has come...! CHADEMA GOOOOOOO...!

  THNK U GOD FOR GIVING US ANOTHER NYERERE..!
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,231
  Trophy Points: 280
  "Alisema nyota ya kisiasa mkoani Manyara kwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Slaa ipo juu, hivyo wanapanga mikakati mbalimbali ya kukinusuru chama hicho." MWISHO WA KUNUKUU

  TATIZO LETU HATUJIFUNZI KUTOKANA NA HISTORIA.....................................WAMWULIZE NYERERE ALIPOSHINDWA KUMBWAGA MGOMBEA BINAFSI WA JIMBO LA MBULU ALIPOSHINDANA NA MGOMBEA WA TANU MIAKA ILE YA KUTAFUTA UHURU..........FUNZO NI KUWA WAMBULU HUSUSANI WANA MSIMAMO SANA...........NA HATA MAFANIKIO YA DR. SLAA PALE KARATU BAADA YA CCM ILIPOMTEMA NA KUMTEUA PATRICK QORRO JITIHADA KIBAO ZILIFANYIKA LAKINI WAKAAZI WA HUKO WAKISHA CHAGUA MTU WAO WEWE WAHESHIMU TU VINGINEVYO.........UTAKIONA CHA MOTO..............................
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,231
  Trophy Points: 280
  Historia hujirudiarudia yenyewe.

  Nyerere mwenyewe alishindwa kule Mbulu alipokuwa anamnadi mgombea wa Tanu kwa jimbo la Mbulu wakati chaguo la wapigakura lilikuwa ni mgombea binafsi ambaye hata hivyo jina lake lilikuwa "Sarawati" Sina uhakika na spellings.

  Halafu ikaja karatu CCM na hasa Mkapa alikuwa ana mtu wake aitwaye Patrick Qorro wakati wapigakura chaguo lao lilikuwa ni Dr. Slaa mwaka 1995. CCM ilikiona cha moto na huo mzuka bado leo ndiyo unawasumbua sasa kupitia Chadema. Tatizo la viongozi wa CCM ni kulewa madaraka kwa kufikiria ya kuwa wanaweza kuwachagulia watu kiongozi.

  Hoja kama za na ninanukuu Katibu wa CCM mkoani Manyara, Avelin Mushi alisema kura za wakazi wa mkoa huo, hazitatosha kumfanya Dk Slaa kuwa rais wa Tanzania kwani wananchi wengi wana imani kubwa na Rais Jakaya Kikwete." Mwisho wa kunukuu.

  Sana sana kauli hizo zinawachefua wapiga kura tu na wala siyo vinginevyo. Hummpi kura mgombea yoyote kwa kufuata mkumbo wa wengi au hisia za wengi wanasemaje unammpa kura mgombea ambaye wewe unaona yupi anafaa ashinde au asishinde
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Haya yanayotokea Manyara ni sehemu tu ya maeneo ndani ya mikoa 15 ambako ccm wana hali mbayaaaaaaaaaaaaaaaaaa kuliko. Manyara IS JUST A REFLECTION OF 15 MIKOA
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Sep 30, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mkoa mmojawapo Mbeya, CCM hali yake iinazidi kutia shaka kadri siku zinavyoenda!
   
 7. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  [B
  Wednesday, 29 September 2010 18:52

  Joseph Lyimo, Simanjiro

  MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa kuwa gumzo kwa wakazi wa Mkoa wa Manyara imezidi kuwapa maumivu makali viongozi wa CCM mkoani humo na kusababisha kufanya vikao vya ndani hadi saa 7:00 usiku.

  Viongozi hao wa CCM Mkoa wa Manyara wakiongozwa na katibu wake, Avelin Mushi, Katibu wa Wazazi Mkoa, George Kijaji, Katibu wa UWT Mkoa,Grace Maholelo na wabunge wateule wa viti maalumu mkoa huo, Dorah Mushi na Martha Umbulla na mgombea ubunge katika Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka wanakutana muda huo, kujadili hilo ni jinsi gani watakabiliana na Chadema.

  Wengine wanaokutana katika mkutano huo ni kamati ya siasa ya Wilaya ya Simanjiro,wagombea udiwani wa CCM na wajumbe wa Halmashauri ya CCM katika Kata ya Mererani.

  Katika vikao hivyo vilivyofanyika juzi kuanzia saa 11:00 jioni hadi saa 7:00 usiku kwenye ukumbi wa Manyara Inn uliopo mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro, pia ulihudhuriwa na mkuu wa wilaya hiyo Khalid Mandia ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM wilayani humo.

  Mmoja kati ya wajumbe wa vikao hivyo ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa vile siyo msemaji wa chama hicho, alisema kuwa upepo wa kisiasa siyo mzuri mkoani Manyara kwa CCM, hivyo uongozi wa mkoa huo umejadili hilo ili kunusuru hali hiyo.

  Alisema nyota ya kisiasa mkoani Manyara kwa mgombea urais wa Chadema - Dr. Slaa.

  SOURCE: Mwananchi
   
 8. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hawa viongozi wa CCM wanapaswa wasiingilie demokrasia ya watu, kama Mwalimu Nyerere alivyosema, :Ujamaa kama demokrasia ni moyo
  (attitude of mind)" Wawaache watu waendelee na uhuru wao.
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Sep 30, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mwaka huu watakesha sana!
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Some Weeks ago a friend from Manyara (Babati) just called and told me how hard ccm will win in constituencies of that Region. Now I can see the truth.

  Vote for Dr Slaa, and Vote for Chadema. We are need changes.
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  baadhi ya wtz wameamka mpaka siamini masikio na macho yangu..........Mungu atusaidie ccm wakubali matokeo na wasijeilazimisha ti=ume kuwatangasza wao.....
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa nchi anazomewa kila mahali, ni vyombo vya habari vichache vinathubutu kuandika hayo, kweli Jamaa isingekua nguvu ya dola, mwaka huu out......akalime mananasi kule kwao Chalinze .
   
 13. Bally B

  Bally B Senior Member

  #13
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 11, 2010
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapa kuna swala inakuaje watendaji wa serikali wanaingilia mambo ya kisiasa wakati sekta nyingine wamepigwa marufuku kujihusisha na mambo ya siasa @Mbulu pia kumekuwa na vikao vinavyokaa hadi saa sita usiku kupanga mbinu na kufanya juu chini wampitishe yule kibaraka wa waziri mkuu Bwana MARMO ambapo wananchi wa wilaya ya Mbulu hawamtakiii,CHADEMA CHONDECHONDE MTUWEKEE WASIMAMIZI WASIYO DANGANYIKA KWA VITU VIDOGO WASIJE KUTUANGUASHA JAMANIIIIIII,INANIUMA SAAANA KUONA WATU WANANG'ANG'ANIA MADALARAKA INGALI HAKUBALIKI HATA KATIKA FAMILIA YAKE
   
 14. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mwaka huu kibarua ni kigumu zaidi kwa mafisadi wote.

  Uzuri ni kwamba hata humo humo ndani ya CCM wako vipande vipande, kachumbali inakolezwa sasa na huu uswahili wa uraisi kuwa swala la kifamilia! kampeini kushikiliwa na baba, mama, na wana!

  Tulinde tu kura zetu, October 31! Watanzania si mandondocha tena!
   
Loading...