MMASSY
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 290
- 193
Hakuna kosa kubwa kwenye siasa kama kumfunga mwanasiasa.Ukifuatilia historia ya mataifa mengi utagundua kuwa kila aliyesweka ndani kwa ajili ya kutetea umma alitoka na kuwa rais,sijui kama ccm watamudu wimbi la kitakachotokea hapa kama watafanya hivyo.Tulisema juzi kuwa hawa ccm na serikali yao wasiwakamate wala kuwatesa akina Dr.Slaa bali wakamate roho zao manake tayari zimetapakaa miongoni mwetu watanzania.HUWEZI ZUIA MAFURIKO KWA VIGANJA!!