Dk. Slaa afanyiwa njama kufungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa afanyiwa njama kufungwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JoJiPoJi, Jan 18, 2011.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Lengo ni kuwanyamazisha viongozi wengine wa upinzani


  NJAMA nzito zinasukwa ndani ya Jeshi la Polisi, Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake ili kuhakikisha Dk. Willibrod Slaa anafunguliwa mashtaka mapya na kuhukumiwa adhabu ya kifungo jela kwa makosa yanayohusiana na vurugu zilizotokea jijini Arusha hivi karibuni, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka polisi, vigogo wa CCM na serikali wameamuru kuwatisha wapinzani na wananchi kwa jumla, kwa "kumtoa kafara kiongozi mkubwa wa upinzani, kwa mara ya kwanza" kama njia pekee iliyobaki kuinusuru serikali ya CCM madarakani.

  Vyanzo hivyo, vinasema njama hizo ni kuhakikisha Dk. Slaa anatiwa gerezani ili kuwatisha na kuwanyong'onyeza viongozi wengine wa chama chake wanaodaiwa kuisumbua CCM na serikali yake kwa kufanya kile kilichoitwa "siasa mpya za kuhamasisha umma kuichukia na kuipinga CCM na serikali ili nchi isitawalike."

  Hatua ya Jeshi la Polisi kushirikiana na Idara ya Habari (MAELEZO) kutengeneza na kutangaza video kupitia vyombo vya habari, yenye picha na ujumbe wa kikituhumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya uchochezi, imetajwa kama njia ya jeshi hilo kujikosha kwa mauaji, na vile vile kujenga mazingira ya kuwatia hatiani viongozi wakuu wa CHADEMA kwa kupalilia propaganda chafu dhidi yao, zisizoeleza chanzo cha kauli zao kali.

  Hatua hiyo imekifanya chama hicho kutayarisha mkanda wa video utakaaoonyesha hali halisi ilivyokuwa ili kusahihisha kile ambacho chama hicho kimeita "uchakachuaji wa polisi."

  Hata hivyo, baadhi ya wafuatiliaji na wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini wameliambia gazeti hili kuwa serikali "ikifanya kosa la namna hiyo la kufunga Dk Slaa, inaweza kujikuta nchi ikiwaka moto na kulazimisha wananchi kuing'oa serikali madarakani kwa nguvu kama ilivyotokea Tunisia katika siku chache zilizopita.."

  "Yeyote aliyewashauri serikali na polisi kufanya hivyo haitakii mema serikali na CCM. Upepo wa sasa kisiasa ni mgumu na mbaya kwa serikali, hivyo inapaswa kufanya maamuzi makini, si kukurupuka; sasa hivi mabavu na dhuluma si mbinu nzuri ya kutumiwa na serikali; vinginevyo yatatokea yasiyotarajiwa," kilisema chanzo kimoja kutoka serikalini.

  Katibu mkuu huyo wa CHADEMA pamoja na viongozi wenzake na wafuasi wao 31, walifunguliwa kesi Januari 6 mwaka huu, wakikabiliwa na shtaka la kukusanyika kinyume cha sheria Januari 5 jijini Arusha, siku ambayo chama hicho kilifanya maandamano ya amani kushinikiza kurudiwa kwa uchaguzi wa meya.

  Maandamano hayo hata hivyo yalivurugwa kwa nguvu ya silaha na vipigo kutoka kwa Jeshi la Polisi, hatua iliyozusha vurugu na mashambulizi zaidi ya risasi zilizoua watu watatu.
  Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena keshokutwa katika Mahakama ya Mkoa wa Arusha.

  Taarifa zaidi za uchunguzi zinasema vigogo wa CCM na serikali kwa kulitumia jeshi hilo la polisi na mawakili wa serikali, wataongeza mashtaka mapya dhidi ya Dk. Slaa na baadhi ya viongozi wengine wa chama hicho ili mwishowe wahukumiwe adhabu ya kifungo kwani shtaka moja lililopo sasa katika kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, halina nguvu ya kuwapeleka gerezani kama watatiwa hatiani.

  Wakati Dk. Slaa akiwa ndiye mlengwa mkuu, njama hizo zinalenga kutumia taratibu za kawaida za kisheria katika kuongeza mashtaka mapya ya kumtuhumu kufanya ‘uchochezi' yeye na wanasiasa wengine watatu ambao alihutubia nao mkutano wa hadhara katika Uwanja wa NMC jijini Arusha jioni ya siku hiyo ya maandamano.

  Wanasiasa hao ni mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo, mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, na kada wao maarufu, John Heche, kutoka Tarime.

  "Watadai kuwa Dk. Slaa na wenzake hao watatu walitoa kauli za uchochezi katika viwanja vya NMC na wataishawishi mahakama ione kwamba kauli zao zilikuwa chanzo kikuu cha vurugu zilizotokea Arusha na kusababisha watu wauawe ….na kwa hiyo watajaribu kuwahusisha moja kwa moja na vifo hivyo ili mwishowe waje wahukumiwe kwenda jela kwa kufanya uchochezi uliosababisha madhara makubwa kwa jamii," alisema mtoa taarifa wetu mwingine aliye karibu na baadhi ya wajumbe wa kamati maalum iliyodaiwa kuundwa siku mbili tu baada ya tukio la Arusha ili kufanikisha mkakati huo.

  "Hivi sasa wanajaribu kuwaandaa vizuri wananchi kwa kuonyesha picha za video na kutoa machapisho mbalimbali kwenye magazeti ili waamini kuwa Dk. Slaa na viongozi wa CHADEMA ndiyo chanzo cha yote yaliyotokea Arusha," aliongeza.

  Hatua ya Jeshi la Polisi kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuwaeleza kile ilichokiita "taarifa ambazo wananchi hawajaambiwa kuhusu vurugu za Arusha zilizotokea Januari 5 mwaka huu" imeelezwa kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa njama hizo ili kuuandaa vema umma uje unyamazie kile kitakachowafika viongozi hao wa CHADEMA.

  Katika mkutano huo, Kamishna Paul Chagonja anayehusika na operesheni na mafunzo katika jeshi hilo, alitumia maelezo ya mdomo, maandishi na picha za video kutoa tuhuma dhidi ya viongozi wa CHADEMA kuwa ndio chanzo cha vurugu zilizotokea Arusha na kusababisha mauaji.

  Tukio hilo lilifuatiwa na kurushwa zaidi kwa picha hizo za video katika vituo vya televisheni na redio na kuchapwa kwenye magazeti taarifa nzima ya polisi yenye maelezo hayo ya tuhuma dhidi ya viongozi wa CHADEMA.

  Hata hivyo, picha za video zilizoonyeshwa kwa wanahabari wiki iliyopita na hata kurushwa kwenye vituo vya televisheni zilionekana dhahiri kupingana kwa kiasi kikubwa na maelezo na sababu zilizotolewa kama kigezo cha kuyasambaratisha maandamano hayo kwa silaha.
  Picha hizo zilionyesha kundi moja tu la viongozi na wafuasi wa CHADEMA lililoanza maandamano kwa amani kutoka eneo ilipo Hoteli ya Mount Meru likitumia njia moja kuelekea Sanawari Mataa na hakukuonekana makundi mengine yaliyokuwa yakitumia njia nyingine kuandamana ambayo yangeleta bughudha na kuwapa polisi shida ya kulinda kama alivyodai kamishna huyo.

  Aidha, picha hizo za video pia hazikuonyesha waandamanaji walioanza kufanya fujo au kuashiria kufanya fujo mpaka walipofika eneo la Sanawari Mataa ndipo Jeshi la Polisi lilipovuruga hali ya amani kwa kuanza kufyatua mabomu ya machozi.
  Kwa upande mwingine, sinema hiyo iliyorekodiwa na Jeshi la Polisi kuhusu matukio yaliyotokea Arusha ilionekana kuchakachuliwa au kuhaririwa sana kwa kukatwa baadhi ya vitendo vya kikatili vilivyofanywa na askari polisi kama vile vya kumpiga sana na kumdhalilisha kijinsia Josephine Mushumbusi, ambaye ni mchumba wa Dk. Slaa.

  Matukio mengine ambayo yalirushwa kwenye picha za vituo vya televisheni hapo kabla lakini hayakuonekana katika kanda hiyo ya polisi ni pamoja na tukio la polisi kuvunjavunja vioo na kuliharibu gari lililokuwa limewabeba Josephine na Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Owenya.

  Wakati picha hizo, ambazo polisi hawakuzitumia, zilionyesha kuwa vurugu zilianza baada ya polisi kuanza kuyatawanya maandamano hayo kwa mabomu na kuwakamata baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wapatao 31, Jeshi la Polisi limekuwa likitumia zaidi picha za video za mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya NMC jioni ili kuhalalisha hoja kwamba chanzo kikuu cha vurugu na mauaji yaliyotokea Arusha ni kauli za Dk. Slaa, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, na wanasiasa wengine waliohutubia mkutano huo.

  Picha hizo zilimwonyesha Dk. Slaa na Ndesamburo wakilalamikia kusambaratishwa kwa maandamano yao kwa mabomu, risasi na vipigo vya polisi pamoja na kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho, akiwemo mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, hivyo kuwasisitizia wananchi kuendelea kudai haki ikiwa ni pamoja na kuwatoa viongozi hao polisi walikokuwa wakishikiliwa.

  "Kipande hicho cha mkanda wa Arusha ndicho watakachokitumia zaidi katika kuijengea nguvu kesi yao dhidi ya Dk. Slaa na wenzake kwamba walitoa kauli za uchochezi," alisisitiza mtoa habari wetu.

  Mwanasiasa mwingine aliyewahi kushtakiwa na kuhukumiwa adhabu ya kifungo kwa kukutwa na hatia ya kutoa kauli za uchochezi ni mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila.

  Mtikila alifungwa jela katika gereza la Ukonga, Dar es Salaam Desemba 14, 1999 kwa hatia ya uchochezi na kutumikia kifungo cha mwaka
  mmoja.


  Mwaka huo alipatikana na hatia ya kutoa kauli chafu na za uchochezi dhidi ya viongozi wa CCM na serikali yake juu ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Horace Kolimba.

  Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kinondoni, Gabriel Mirumbe, alimtia hatiani kwa maelezo kwamba mwanasiasa huyo alitoa maneno ya chuki dhidi ya viongozi wa CCM na serikali kwamba walimuua Kolimba na ni mashetani.


  SOURCE: Tanzania Daima
   
 2. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hamna kitu, acha hizo maneno yako yote hana ukweli bali ni kuisingizia Serikali uongo
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Taratibu mkuu; Jamaa ameweka kabisa Source : Tanzania Daima..... Sasa uongo wake umetoka wapi? kwamba Source Sio Tanzania Daima au?
   
 4. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  imekula kwenu ccm na arafat.ndo utajua inteligensia ya chadema ni ishu tofauti.pipooozzz!
   
 5. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Katika mazingira ya sasa hivi,habari hii ni ya kutuondoa kwenye hoja zetu za msingi. Tuliomakinika,hatudanganyiki.
   
 6. S

  Shiefl Senior Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninachokubali ni kuwa majamaa sasa hata wakilala usiku wanamulikwa. Yaani we acha na kurukakara yao mcc lazima wakazeeke na makaamba wao. Hiki kizazi hata kuloga wazee wamekoma:frusty:
   
 7. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  hoja ya msingi kwako ni ipi?patachimbika mkimgusa rais wetu dr slaa, na mie ntaweka phd yangu kushoto, patavyochimbika ndio mtajua kuna namba nyingine noma!
   
 8. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  ukishaona ID tayari unaelewa mtu uyo atachangia nini.eti arafat.
   
 9. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pongezi Mhe Kikwete, Lowassa na Rostam Aziz kwa ubunifu huu mpya.

  Kwa kweli jitahidini kuitekeleza haraka sana na bila kusahihisha japo hata nukta mle ndani. Hii itakua ni njia ya mkato zaidi ya kuwasaidieni kupata nauli kama rais wa Tunisia kukimbilia Uarabuni.

  Wala msirudi nyuma kwani tunawasubirini kwa hamu kubwa haina mfano wake. Vijana mpoooooo?????????? Jakaya ataka NAULI YA MAPEMA mnaona vipi tukamchangishie upesi???????
   
 10. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  tunasubiri kwa hamu sana hiyo hukumu! Nadhani sasa utawala huu wanataka waishie 2011. Kufungwa kwa dr slaa mbona ndo mwanzo wa ukombozi wa watanzania wala siyo shida, shida ni wao je wako tayari kuachia ngazi pale pale watakapo toa hiyo hukumu?
   
 11. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Saa ya ukombozi inanukia.......good strategy JK maana viza ya Saudi Arabia inakusubiri.
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mhahariri wa Tanzania Daima nani Kibanda!! kibanda siyo mtu wakuamini hata kidogo, Kibanda ni Mdomo wa EL, RA na Gazeti la Uhuru, angalia anavyo mshamburia Sitta! kama hujui jiulize mimi sivyo kama unavyofikiri ila sio kila kitu ni cha kuamini tena uongo wa wazi kama huo duh! Magazeti hayawezi kuwa mojamoja reliable source ya mambo kama hayo wewe umeona hilo gazeti?
   
 13. V

  VKEY Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
 14. Abigree

  Abigree Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Let them try,and see wat happened. Thithim c wanajidai wanajua kucheza karata 3? Hebu tuone sasa. Watz wako frustrated na thithiem,they dont ve 2bet wat ll happen
   
 15. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Watubhutu waone moto wake yatakuja yale ya Chacha wangwe walivyo mfunga alivyo toka akachukua jimbo na Mandela kule bondeni wamepotea
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Afadhali tumegundua njama zao mapema hazitafanikiwa tena, jamani oneni jinsi intelijensia ya chadema inavyofanya kazi. mwema akitaka kufanikiwa kiintelijensia tunamkaribisha chadema wapo vijana wa kazi.
   
 17. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,064
  Trophy Points: 280
  Mbona mkali ndugu yangu? Wangapi wako jela leo hii? Kwanini Slaa asipelekwe? Ccm haishindwi kitu, ila kumfunga Slaa ni kumfanya awe shujaa wa pili wa Afrika baada ya Mandela
   
 18. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  False Alarm!
   
 19. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mfungeni Silaa, muzidi kjipotezea 2015, japo najua hiyo mbinu italenga kumuweka ndani mpaka uchaguzi wa 2015 utakapopita
   
 20. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Bad strategy. What is happening now in Tz is not about Slaa or CDM, it is about what people want?
  I wonder why CCM dont get it ?
   
Loading...