Dk Sinare aula tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Sinare aula tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ngoshwe, Jul 4, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  PAMOJA NA MADAI YA MHE. ZAMBI KUWA ALITEULIWA NA RAIS KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUNGENZI YA KAHAWA "KIMTINDO MTINDO" WAKATI KAMPUNI YAKE YA UWAKILI IKIWAKILISHA BENKI YA EXIM MAHAKAMANI KWENYE KESI YA KUTAKA KULIPIGA MNADA JENGO LA KAHAWA (KAHAWA HOUSE):
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD]
  [/TD]
  [TD]
  MWANASHERIA Mtanzania ambaye kwa miaka zaidi ya 12 amekuwa akiwasilisha maslahi ya taasisi kadhaa za fedha nchini kimataifa, Dk Eve Hawa Sinare, amechaguliwa kuingia katika Bodi ya World Services Group (WSG) yenye makao makuu yake nchini Marekani. Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana mjini Dar es Salaam, Dk Sinare atakuwa katika Bodi hiyo yenye makazi yake mjini Texas nchini Marekani kwa miaka minne. Dk Sinare atakuwa anawasilisha maslahi ya Afrika na Mashariki ya Kati.

  Akizungumzia uteuzi wake katika WSG ulioanza Juni mwaka huu, Dk Sinare, ambaye ni mshiriki mwandamizi wa moja ya kampuni kubwa za sheria nchini, Rexattorneys, alisema anajisikia heshima kubwa kuteuliwa katika nafasi hiyo kubwa. Alisema uteuzi wake katika Bodi hiyo unaonesha ni kwa kiasi gani kampuni ya Rexattorneys inavyoaminika miongoni mwa kampuni zinazowakilisha maslahi ya wadau mbalimbali katika sekta ya sheria. WSG ni shirikisho la wanasheria wanaotukuka na hutoa huduma mbalimbali za kisheria kwa watu tofauti zikiwamo benki na taasisi za kifedha.

  Kwa kawaida, wanachama wa shirikisho hilo huwa wazi na husaidiana kuhudumia wateja wao popote pale duniani. WSG ina wanachama 10,000 kutoka nchi 90 na wamejikita zaidi katika masuala ya kampuni kubwa. Aidha, ina wataalamu wa kada mbalimbali wapatao 19,000 wakiwamo wanasheria, wahasibu na wataalamu wa masuala ya kibenki na wana ofisi 400 duniani kote. Kabla ya kuingia katika kazi ya sheria, Dk Sinare alikuwa mshauri wa Serikali katika masuala ya ubinafsishaji. Pia alishawahikuwa Mkurugenzi wa masuala ya kisheria katika Soko la Pamoja la Kusini na Mashariki mwa Afrika (Comesa). Pia amekuwa Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  _______________
  Mbunge CCM apinga uteuzi wa JK


  [​IMG]
  Na Mwandishi wetu - Imechapwa 15 June 2012

  MBUNGE wa Mbozi Mashariki (CCM), Godfrey Zambi amepinga uteuzi wa mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete.
  Amepinga pia uteuzi wa baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na kile alichoita "utungwaji kanuni za zao la kahawa bila kufuata taratibu."
  Februari mwaka huu, rais alimteua Dk. Eve Hawa Sinare kuwa mwenyekiti wa TCB; hatua iliyofuatiwa na waziri wa kilimo (wakati huo Prof. Jumanne Maghembe) kuteua wajumbe wa bodi.
  Hivi sasa Prof. Jumanne Maghembe ni waziri wa maji.
  Katika barua ambayo Zambi amemwandikia Waziri wa Kilimo, Christopher Chiza, ambayo MwanaHALISI imeona, mbunge huyo anachambua mjumbe mmoja baada ya mwingine na kusema hawakupatikana kwa uwiano wa kikanda.
  Zambi anasema katika barua yake kwamba Dk. Sinare "hafai kuwa mwenyekiti wa bodi" kutokana na kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi.
  "Naomba ieleweke kwamba, Dk. Eve Hawa Sinare, mwanasheria wa kampuni ya uwakili ya Rex Attorneys, ndiye alipewa kazi na Benki ya NMB kwa ajili ya kulipiga mnada jengo la Kahawa Moshi (ofisi kuu ya TCB). Hadi sasa jengo hilo lina mgogoro," anaeleza Zambi.
  Anasema, "…inashangaza kumteua mtu ambaye amepewa kazi ya kulipiga mnada jengo hilo…kuwa mwenyekiti. Atakwepaje mgongano wa kimaslahi?"
  Zambi anasema ana uhakika Rais Kikwete "amedanganywa" kuhusu mteuliwa wake. Anasema Dk. Sinare hawezi kutetea maendeleo ya Bodi kama mwenyekiti; na wakati huohuo kusimamia uuzwaji wa jengo ambamo ndipo zilipo ofisi kuu za TCB.
  Anamshauri waziri Chiza amshauri rais kutengua uteuzi wa Dk. Sinare ili kuitendea haki bodi ya wakurugenzi; na menejimenti ya Bodi ya Kahawa iweze kufanya kazi kwa uhuru zaidi.
  Barua ya Zambi ya 4 Juni 2012, imenakiliwa kwa Rais Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.
  Wajumbe wa bodi ambao kuteuliwa kwao kumepingwa na Zambi, ni pamoja na mhandisi mstaafu wa maji, Miraji Omari Msuya.
  Zambi anasema uteuzi wa Msuya haukuzingatia sheria kwa sababu hajulikani anawakilisha kundi gani.
  Mjumbe mwingine ni mwanasheria na mwenyekiti wa kampuni ya Lima anayosema inahusika na ununuzi wa kahawa, Eric Ng'maryo.
  Anadai vyama ambavyo vinatambuliwa na vinaweza kuwakilishwa kwenye bodi ni Tanzania Coffee Association na Association of Coffee Growers, lakini siyo Lima anakotoka Ng'maryo.
  Zambi ameituhumu pia Lima "kushawishi wakulima kuuza kahawa mbichi (mbivu) au red cherry kwa bei ndogo sana."
  Kuhusu Prof. James Teri, ambaye ni mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kahawa (TaCRI), Zambi anasema "Taasisi yake siyo ya serikali na hivyo kumteua mtendaji wake mkuu kwenye bodi kama mwakilishi wa serikali, si sahihi hata kidogo…"
  "Mheshimiwa waziri, sababu nyingine kubwa ya kupinga uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Kahawa ni kutozingatia uteuzi wa wajumbe kwa kuzingatia maeneo makubwa ya uzalishaji kahawa nchini," anaandika Zambi katika barua ya kurasa nane.
  Anataja kanda ya Kaskazini, yenye mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga; Mbinga (mkoani Ruvuma), Mbeya, Kagera, Kigoma na Tarime (mkoani Mara), kuwa ndiyo maeneo makubwa ya uzalishaji kahawa.
  Analalamika kuwa Mbeya ambako inalimwa kahawa nyingi, hawakupata mwakilishi kwenye bodi.
  Anasema, "…inashangaza sana kuona kwamba kati ya wateuliwa wote kumi (10) kwenye Bodi, watano (5) wanatoka mkoa mmoja wa Kilimanjaro…"
  Tuhuma za upendeleo kwa misingi ya ukanda, ziliwahi kutolewa mwaka jana wakati wa mkutano wa bajeti.
  Zilikuwa zikilenga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo. Alikuwa akidaiwa kuwa chanzo cha watu kutoka sehemu moja kujazana idara ya wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii iliyokuwa ikiongozwa na Waziri Ezekiel Maige.
  Kabla ya kwenda ikulu kuwa katibu mkuu kiongozi, Luhanjo alikuwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  Alihamia huko akitokea Wizara ya Maliasili na Utalii anakodaiwa alishawishi uteuzi wa watendaji kwa misingi ya ukabila katika Idara ya Wanyamapori.
  Aidha, kanuni mpya za zao la kahawa ambazo Zambi anadai kupinga ni zile zilizojadiliwa kwenye mkutano wa wadau wa kahawa tarehe 24 na 25 Mei mwaka huu, mjini Morogoro.
  Zambi anadai mkutano wa Morogoro uliambiwa kuwa kanuni mpya tayari zimesainiwa na waziri husika tangu 18 Aprili mwaka huu.
  "Mheshimiwa waziri, napenda ufahamu kuwa kanuni hizo zimwetungwa kinyemela kwa sababu wadau wa kahawa hawakushirikishwa kabisa," anaeleza Zambi.
  Anadai kuwa kikao cha TCB mjini Moshi mwaka 2011, ambacho inadaiwa ndiko zilitungiwa kanuni, hakikuwa na ajenda hiyo na kwamba yeye mwenyewe alikuwepo.
  Anasema, hata hivyo, kikao hicho hakikuwa cha wadau kwani kilikuwa cha wajumbe 30 tu. Amemweleza waziri kuwa kikao cha wadau kina wajumbe zaidi ya 200.
  Zambi anasema hajaona kanuni hizo lakini anadai "…zitakuwa kanuni mbaya. Kanuni ambazo hazina faida kwa mfanyabiashara."
  Akiandika kwa niaba ya "Wanambeya (wakulina wa kahawa)," anasema wana imani na waziri.
  "Tunatumaini masuala haya mawili mazito sana, moja uteuzi wa wajumbe wa bodi bila kufauta sheria na utungwaji kanuni za zao la kahawa bila kufuata taratibu, utayafanyia kazi kama ambavyo nimeshauri," anahitimisha barua yake.


  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Mbunge CCM kuburutwa kortini[/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 17 June 2012 09:28[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  0digg
  Daniel Mjema, Moshi
  MBUNGE wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM), ameingia matatani baada ya kampuni moja ya ununuzi wa kahawa kumshtaki mahakamani ikimdai fidia ya Sh2.4 bilioni.

  Kesi hiyo namba CC.7/2012 ilifunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi na Kampuni ya Lima Ltd inayonunua kahawa maeneo mbalimbali nchini ikiwamo Mbozi.

  Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa kortini na Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Lima Ltd, Eric Ng'maryo, Zambi amewasababishia hasara ya Sh1.8 bilioni kutokana na matamshi ya kuikashifu.

  Katika hati hiyo ambayo Mwananchi Jumapili imeona, Ng'maryo analalamika kuwa katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo Zambi ameanzisha kampeni chafu dhidi ya Lima Ltd.

  "Mdaiwa ameanzisha kampeni za kuchafua kampuni yetu ili kuua ushindani ili vikundi vya wakulima anavyodai kuviwakilisha visiweze kupata ushindani," amedai Ng'maryo.

  Ng'maryo ambaye ni wakili mashuhuri nchini, amedai kuwa lengo la Zambi ni kuwakandamiza wakulima wa Mbozi na Mkoa wa Mbeya ili wasipate bei nzuri ya kahawa.

  Msingi wa kesi hiyo ni makala yaliyochapwa katika gazeti moja chini ya kichwa cha habari "Mbunge CCM apinga uteuzi wa JK".

  Katika makala hayo, Zambi amekaririwa akipinga uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Dk Eve Hawa Sinare na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo. Ng'maryo pia ni mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo ya wakurugenzi.

  Kupitia taarifa hiyo, mbunge huyo anadaiwa kuituhumu Kampuni ya Lima Ltd yenye makao yake mjini Moshi kushawishi wakulima kuuza kahawa mbivu kwa bei ndogo.

  "Uhalisia na tafsiri ya kawaida ya kauli hiyo ya Zambi ni kwamba Lima Ltd ni walanguzi wanaopata faida kubwa kwa kuwanyonya wakulima wa kahawa," amelalamika Ng'maryo.

  Kutokana na kauli hizo za kashfa za mbunge huyo, heshima ya kampuni hiyo imedaiwa kushuka machoni mwa wakulima na inatarajia kupata hasara ya Sh600 milioni mwaka huu.

  Katika kuthibitisha uhalali wa fidia hiyo, Kampuni ya Lima Ltd itaegemea ushahidi kuwa Zambi ni Mbunge anayetumia nafasi yake kuanzisha vita binafsi na kampuni hiyo.

  Kampuni hiyo inadai kuwa katika kesi hiyo itathibitisha kwamba mbunge huyo ana masilahi katika biashara ya kahawa na anaua ushindani ili kuvipa faida vikundi vya wakulima alivyo na masilahi navyo.

  "Zambi ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri, lakini anafanya mambo kinyume na sheria za nchi anazopaswa kuzilinda zikiwamo kanuni zinazosimamia sekta ya kahawa," amedai.
  Kampuni hiyo inaiomba Mahakama kumwamuru mbunge huyo awalipe Sh2.4 bilioni, kama fidia na iwe fundisho kwa wengine.

  Pia kampuni hiyo inaiomba Mahakama Kuu kutoa zuio dhidi ya mbunge huyo kuendelea kuchapisha taarifa za kuikashifu kampuni hiyo.

  Zambi alipoulizwa alisema hajapata taarifa ya kushtakiwa, lakini kama ataarifiwa rasmi na Mahakama, atakaa na wanasheria wake kujua nini cha kufanya.

  Kesi hiyo iliyofunguliwa Jumatano wiki hii na kupewa nambari CC.7/2012, sasa iko kwenye mchakato wa kupangiwa Jaji atakayeisikiliza.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Mbunge CCM kuburutwa kortini

  NI FAMILIA ILIYOJAALIWA:

  H.E. Mrs. Mwanaidi Sinare Maajar
  [TABLE="width: 95%, align: center"]
  [TR]
  [TD="width: 20%"][​IMG][/TD]
  [TD="width: 80%"]H.E. Mrs. Mwanaidi Sinare Maajar is a leading lawyer in Tanzania with exceptional expertise in mining law. Her pioneer work in the field of reviewing regulatory regimes was the review of the Mining Sector Policy and the drafting of the Mining Act, 1998. Another similar assignment was the review of the business licensing regime and the drafting of the now proposed new business licensing law. Mrs. Maajar is now serving as the Tanzanian Ambassador to the United States of America after having served for four (4) years as the Tanzanian High Commissioner to the United Kingdom from 2006. Mrs. Maajar still retains her seat as a partner at the Firm and is still involved in the activities and the development of REX. She imprinted on REX her expertise in reviewing regulatory legal frameworks by setting up and leaving behind a powerful and well-manned portfolio in this regard, which is now headed by Dr. Eve Hawa Sinare.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 848
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  du huyu mama anatisha, naomba cv yake tafadhali.
   
 3. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  kuna utata kuhusu huyo sinare kwani kampuni yake ya uwakili ndiyo ilikuwa inaitetea Tanesco na wakati huo huo kuidhamini Dowans kupata mkopo kwenye mabenki kutokana na maelezo yako kuna mchezo unafanywa na watu makusudi kwa sababu kwa issue ya Tanesco nilitegemea serikali wangeichukulia hatua kampuni hiyo kwani ndio walioshauri mkataba uvunjwe na baadae wakasema Tanesco haina jinsi inabidi ilipe madeni
   
 4. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Mbona mnafuatilia sana mambo ya watu huyu mama ni kichwa na anatembea kwenye reli za opportunity sasa ukiwana akili kubwa katikati ya akili ndogo unategemea nini ??mama ana akili kubwa na magamba yote yana akili ndogo huyo zambi sio mzima hata akiongea anaonekana ana kautindio ka kichwa
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  JK huwa anaziona familia ya Sinare na Migiro tu. Udini mtupu!
   
 6. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu,
  Yaani Serikali ya magamba kweli ni dhaifu. Kampuni ya Rexattorney ndo mawakili wa TANESCO mpaka leo. Kama ulivyosema, hawa ndo walishauri TANESCO wavunje mkataba na Dowans wakisema hakuna tatizo kufanya hivyo kwa kuwa Dowans ilikuwa ni kampuni feki. Hao hao ndo waliwapigia chapuo Dowans kwa mabenki kuwa ni kampuni nzuri tu na inastahiki kupewa mkopo. Hao hao ndo walipeleka ushahidi dhaifu kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa masula ya biashara ili TANESCO washindwe kesi na ikawa hivyo. Hao hao ndo walisema hamna haja ya kuka rufaa na hmna jinsi inabidi TANECSO tu walipe. Cha kushangza ni kuwa pamoja na hayo maovu yote kuwa wazi bado kampuni hiyo inaendelea kuwa wakili wa TANESCO lol! Hii nchi imeuzwa kwa kweli.
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Dr Hawa Sinare ni msomi mzuri na naamini ana uwezo wa kufanya kazi nzuri (kama system iko clean). Hata hivyo promotion yake haijatokana na uwezo wake peke yake, naamini 'techinical know who?" nayo imembeba sana. After all huko Marekani ndiko aliko ndugu yake kama Balozi Majaar.
   
 8. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Sio kila habari ni habari
   
 9. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Katika kusakamwa sana kwa Rexattorneys hata website yao huwezi ku access! Huii firm inabidi ichukuliwe hatua kali sana manake wamejipatia pesa nyingi sana kwa ushauri wao mbaya wa kisheria.
   
 10. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2015
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,561
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Karibu UKAWA mama tunahitaji uwepo wako
   
 11. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2015
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Msaada wake ni mdogo kwa UKAWA...
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2015
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Na Zambi akapata uwaziri...
   
 13. lucky sabasaba

  lucky sabasaba JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2015
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 1,672
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 145
  Hawezi kukosa watu 100 nyuma yake !!wanatosha saaaanaaaa
   
 14. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2015
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  bado makandokando ya lowasa yanazidi kukimbia ccm naona ccm mpya inakuja kwa mbali ingawa bado kuna virusi vingi
   
 15. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2015
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,561
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  UKAWA mnaota kupata urais ni kura si maneno matupu watanzania wameamua kuibakiza CCm kwa iaka mingine 5. CCM HAPA KAZI TU POROJO PELEKA UKAWA
   
 16. Lancanshire

  Lancanshire JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2015
  Joined: Sep 20, 2014
  Messages: 13,775
  Likes Received: 7,925
  Trophy Points: 280
   
 17. Lancanshire

  Lancanshire JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2015
  Joined: Sep 20, 2014
  Messages: 13,775
  Likes Received: 7,925
  Trophy Points: 280
  Na huyu mwenye kampuni hii ya uwakili leo kajiunga rasmi na lowassa.teh teh teh
   
 18. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2015
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  hawa ndio wanadai wanataka kuleta mabadiliko wakati wameifikisha nchi hii pabaya na chadema wanawafurahia
   
 19. Muyobhyo

  Muyobhyo JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2015
  Joined: Oct 9, 2014
  Messages: 6,543
  Likes Received: 4,401
  Trophy Points: 280
  Hajasema anajiunga na ukawa
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2015
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Sizitaki mbichi hizi.
   
Loading...