Dk. Nchimbi, Mr. Sugu warushiana vijembe bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Nchimbi, Mr. Sugu warushiana vijembe bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Mr. Sugu.


  Ukumbi wa Bunge juzi uligeuka kuwa ulingo wa kutupiana vijembe kati ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi, na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu “Mr. Sugu”.

  Tukio hilo lilitokea wakati wabunge walipokuwa wakijadili Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Vijana wa Afrika, kabla ya baadaye kupitisha azimio hilo.

  Aliyeanza kurusha vijembe kwa mwenzake alikuwa ni Mr. Sugu, ambaye wakati wa kujadili hoja alimshutumu Dk. Nchimbi kuwa ameteua marafiki zake katika Kamati ya Kutafuta Vazi la Taifa na kuwaacha watu wenye ujuzi na uzoefu wa masuala ya mavazi na mitindo.

  “Nampongeza waziri kwa kuanzisha mchakato wa kutafuta vazi la taifa na hii itaacha legacy (urithi) na hata Bunge hili litaacha legacy katika suala hili, lakini Mheshimiwa waziri umeacha vijana ambao wana nafasi katika hili, unawaacha badala yake umechagua washikaji zako, unawaacha watu kama Hassannali na Khadija Mwanamboka ambao wana uzoefu katika mambo ya mavazi,” alisema.

  Akijibu kijembe hicho, Dk. Nchimbi alijitetea kuwa mchakato wa kuteua wajumbe wa kamati hakuufanya peke yake bali kwa kushirikiana na maofisa wengine wa wizara.

  Alisema wajumbe waliochaguliwa ni watu makini ambao wanaweza kuifanya kazi hiyo vizuri.

  “Walioteuliwa ni watu makini hakuna rafiki yangu, hivi sasa imezuka tabia kama unataka kuteua kamati unaanza kujiuliza nani ana adui maana lazima yatazuka maneno,” alisema Dk. Nchimbi.

  Aliongeza: “Hivi Joseph Kusaga, Mustafa Hassanal, Joyce Mhavile, Ndesambuka Merinyo, Angela Ngowi, Habib Gunze na Kuhenga Makwaiya siyo watu makini kweli?” Tuache chuki kama kuna mtu mmekoseana msameheane, tuache visasi, kiongozi mzuri ni yule anayeacha visasi.”

  Awal, wakati akisoma maoni ya kambi ya upinzani kuhusiana na azimio hilo, Mr. Sugu, alisema muswada huo ulitakiwa kwanza kupitia kwenye Kamati ya Bunge ya Ustawi wa Jamii, lakini umepelekwa moja kwa moja bungeni kinyume cha taratibu.

  Hata hivyo, Dk. Nchimbi alisema kwa mujibu wa taratibu za Bunge, maazimio huwa hayapitii kwenye kamati kwa ajili ya kusomwa na wabunge kujadili.

  “Kama mtu hujui kitu ni vizuri kutafuta ushauri wa wanasheria kabla ya kuongea. Chadema ina wanasheria waliobobea kama Tundu Lissu na Halima Mdee hata mimi nikikwama huwa naomba ushauri wao. Sasa siyo vibaya Sugu na wewe ukaomba ushauri kabla ya kuongea bungeni,” alisema Dk. Nchimbi.

  Kabla ya hapo, Dk. Nchimbi alirusha kijembe kingine kilichoonekana kumlenga Mr. Sugu, pale alipodai kuwa kuna mbunge ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook akiwaalika wasichana kwenye shughuli yake ya muziki aliyoaandaa wakiwa wamevaa vimini.

  “Hii siyo sawa, ukishakuwa mbunge unatakiwa uwe na busara. Mimi nazungumza hapa halafu unaniangalia,” alisema Dk. Nchimbi huku akiangalia upande aliokaa Mr. Sugu.

  Hata hivyo, baada ya kutupiana vijembe hivyo, Dk. Nchimbi na Mr. Sugu walionekana nje ya ukumbi wa Bunge wakiwa pamoja wakizungumza kwa furaha.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  dah kama movie vile ....
   
 3. A

  Amani Ndelwa Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi chai za kawaida hazijengi we need hot topics
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red tu mie tatizo... sijui kigezo ni kofia au nini

  he falls short of the minimum requirements
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Yaani Sugu nae ni shabiki wa vazi la taifa? Tena kwa kisingizio cha kuacha legacy!
   
 6. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Hivi nchimbi anaongea kusameheana leo!!!
  Kweli CCM wamejaa unafiki! Nchimbi alimsamehe lini Amina Chifupa? Alimsamhe lini Ipi Male..?
  Awaambie kina Kikwete, Lowassa, n.k walioshindwa kumsamehe Mwakyembe..............
   
 7. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Joseph Kusaga ni mshikaji wake Nchimbi! Hata afanye nini ukweli ni huo.
   
Loading...