Dk. Mwele Ntuli Malecela kuachishwa kazi.

BigBros

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
1,227
2,000
Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.

Shida nchi yetu hii kila kitu kinakuwa related na Siasa. Professionals can't do their work.
 
TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,295
2,000
Jamani tuache upotoshajiiii Mh Rais alichokiamua kipo sawa kabisa hili ni taifa na taifa linaendeshwa kwa utaratibu, Huyu mama sio msemaji wa serikali hivyo hakuwa na malaka yeyote kisheria kutangaza report ambayohata hao wakuu wa serikali walikuwa hawajaiona au kuisoma, Huu ni muendelezo mwingine wa wale wachumia tumb kupotosha na kumdhihaki Rais wetu wakijuwa wanachokifanya ni kulidhoofisha taifa.

Swali zito na gumu kujiuliza nani alie mtuma Dr Malecela?
Na kwanini alisisitizia kwenye report yake either tukubali au tusikubali kuna zika hapo alikuwa ametumwa na nani? au alikuwa akijaribu vyombo vya usalama?

Yapo mengi kizani tutayaona mwisho wa mwaka huu na kuelekea 2017 lakini nina imani Mh Rais atashinda vita hii kwa nguvu za Mungu alie hai. big up tiss
 
naan ngik-kundie

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
1,771
2,000
Sidhani kama Dk Mwele alijichukulia maamuzi ya kutaarifu umma juu ya ZIKA bila kuhusisha wizara ya afya, waseme tu ukweli taarifa walikua nayo lkn hawakutaka itolewe kwa sasa.
 
BAGAMIKA

Senior Member
Jul 2, 2015
158
225
Jamani tuache upotoshajiiii Mh Rais alichokiamua kipo sawa kabisa hili ni taifa na taifa linaendeshwa kwa utaratibu, Huyu mama sio msemaji wa serikali hivyo hakuwa na malaka yeyote kisheria kutangaza report ambayohata hao wakuu wa serikali walikuwa hawajaiona au kuisoma, Huu ni muendelezo mwingine wa wale wachumia tumb kupotosha na kumdhihaki Rais wetu wakijuwa wanachokifanya ni kulidhoofisha taifa.
Swali zito na gumu kujiuliza nani alie mtuma Dr Malecela?
Na kwanini alisisitizia kwenye report yake either tukubali au tusikubali kuna zika hapo alikuwa ametumwa na nani? au alikuwa akijaribu vyombo vya usalama?
Yapo mengi kizani tutayaona mwisho wa mwaka huu na kuelekea 2017 lakini nina imani Mh Rais atashinda vita hii kwa nguvu za Mungu alie hai. big up tiss
nchi haiwezi kuwa kama Bar kila mtu akijisikia kusema anasema tu
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,884
2,000
wewe
Jamani tuache upotoshajiiii Mh Rais alichokiamua kipo sawa kabisa hili ni taifa na taifa linaendeshwa kwa utaratibu, Huyu mama sio msemaji wa serikali hivyo hakuwa na malaka yeyote kisheria kutangaza report ambayohata hao wakuu wa serikali walikuwa hawajaiona au kuisoma, Huu ni muendelezo mwingine wa wale wachumia tumb kupotosha na kumdhihaki Rais wetu wakijuwa wanachokifanya ni kulidhoofisha taifa.
Swali zito na gumu kujiuliza nani alie mtuma Dr Malecela?
Na kwanini alisisitizia kwenye report yake either tukubali au tusikubali kuna zika hapo alikuwa ametumwa na nani? au alikuwa akijaribu vyombo vya usalama?
Yapo mengi kizani tutayaona mwisho wa mwaka huu na kuelekea 2017 lakini nina imani Mh Rais atashinda vita hii kwa nguvu za Mungu alie hai. big up tiss
Hujui, alikuwa anasema kama mtafiti na utafiti wake, sio kama mamlaka ya serikali. Hajasema kuwa jeshi hiv na hivi! hajasema mipaka na malawi hiv na hivi, hajasema siasa ya nje hivi na hivi etc
 
Kibstec

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,205
2,000
Jamani tuache upotoshajiiii Mh Rais alichokiamua kipo sawa kabisa hili ni taifa na taifa linaendeshwa kwa utaratibu, Huyu mama sio msemaji wa serikali hivyo hakuwa na malaka yeyote kisheria kutangaza report ambayohata hao wakuu wa serikali walikuwa hawajaiona au kuisoma, Huu ni muendelezo mwingine wa wale wachumia tumb kupotosha na kumdhihaki Rais wetu wakijuwa wanachokifanya ni kulidhoofisha taifa.
Swali zito na gumu kujiuliza nani alie mtuma Dr Malecela?
Na kwanini alisisitizia kwenye report yake either tukubali au tusikubali kuna zika hapo alikuwa ametumwa na nani? au alikuwa akijaribu vyombo vya usalama?
Yapo mengi kizani tutayaona mwisho wa mwaka huu na kuelekea 2017 lakini nina imani Mh Rais atashinda vita hii kwa nguvu za Mungu alie hai. big up tiss
Very true...hiii ishu ina negative impact kubwa sana kwetu...watu tunakimbilia kuleta ushabiki wa kipuuuzi tu
 
eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,203
2,000
Jamani tuache upotoshajiiii Mh Rais alichokiamua kipo sawa kabisa hili ni taifa na taifa linaendeshwa kwa utaratibu, Huyu mama sio msemaji wa serikali hivyo hakuwa na malaka yeyote kisheria kutangaza report ambayohata hao wakuu wa serikali walikuwa hawajaiona au kuisoma, Huu ni muendelezo mwingine wa wale wachumia tumb kupotosha na kumdhihaki Rais wetu wakijuwa wanachokifanya ni kulidhoofisha taifa.

Swali zito na gumu kujiuliza nani alie mtuma Dr Malecela?
Na kwanini alisisitizia kwenye report yake either tukubali au tusikubali kuna zika hapo alikuwa ametumwa na nani? au alikuwa akijaribu vyombo vya usalama?

Yapo mengi kizani tutayaona mwisho wa mwaka huu na kuelekea 2017 lakini nina imani Mh Rais atashinda vita hii kwa nguvu za Mungu alie hai. big up tiss
Sawa lakini ugonjwa upo
 
VAN HEIST

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,432
1,250
Kumbe ugonjwa upo na kosa la Dr Mwele ni kutofuata utaratibu kutangaza

Huyu waziri wa Afya aliyekanusha kwamba haupo alikuwa na maana ipi ?
Atakuja kukanusha tena kwamba hakukanusha kuhusu uwepo wa ZIKA na atakiri kuwa ZIKA ilikuwepo tangu awamu ya 4
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom